WANAUME!! USISHANGAE MWANAMKE WAKO AKAFANYA MAAMUZI YA KUOLEWA NA KIBABU AKAKUACHA SABABU HUWA NI HII.
WANAUME
Usishangae kumuona binti amechukua Maamuzi MAGUMU ya kuolewa na mwanaume ambaye karibu ni mara 2 ya umri wake. (JAPO SIJASEMA SASA NDIO MKAOLEWE NA WAZEE NO)
Unaweza Ukamuona hana akili, au ukasema amefuata Pesa na sio mapenzi ya dhati, huu ni upande mmoja ambao wengi mnaweza mkafikiria. Lakini upo upande wa pili ambao nitaenda kuuzungumzia... 👇
Hivi sasa kuna WAVULANA wengi lakini Wanaume ni Wachache, Ninaposema Wavulana namaanisha watu ambao wana jinsia /maumbile ya kiume lakini wana
IMMATURE Mind (akili za kitoto /zisizo komaa).* Unakuta kijana anakaribia miaka 30 bado yupo nyumban, bado analelewa na Wazazi.
Kazi kunyoa Viduku, Kuvaa Milegezo na kupaka Poda. Aise, unataka kugombania mashindano ya
UREMBO*? Unataka usifiwe Uzuri? Unataka kuolewa au❓
Anashinda kupiga
SELFIE* na kupost picha Instagram, Anashinda na remote Kazi kubadilisha channel za TV. Ukimuuliza vipi anakuambia anasubiria AJIRA siku Kazi Ngumu.
_Hivi ni kweli Kazi hakuna au unachagua Kazi❓ Hivi Kulima sio Kazi? Kwanin usiende kijijini kwa bibi yako uchukue hata heka moja ulime Vitunguu kuliko kubaki ukijaza foleni mjini._
_Kwanini usiuze hiyo smart phone yako yenye thamani zaidi ya laki moja na nusu, na hiyo Pesa huifanye #MTAJI wa kufuga Kuku? Kuliko kushinda online ukicomment na kupost UJINGA._
_Kwanini usiende hata kufanya vibarua viwandani na kurudi hata na elfu 5 kwa siku, kuliko kukaa nyumban kugombania vitafuno na wadogo zako?_
Unajiona msomi wa chuo Kikuu huwezi kufanya vibarua, Weka degree yako Kabatini, wewe Ingia Mtaani. KAZI NI KAZI, VIBAYA mwanaune KUOMBA.
_Kwanini usifanye hata volunteer's Work (Kazi za kujitolea)? Kazi humfuata aliye na Kazi na si asiye na Kazi. Waswahili wanasema mgaa-gaa na Upwa, HALI wali MKAVU na MTEMBEA bure si sawa na MKAA Bure._
Sasa kwa mwanamke anayejitambua anaanzaje kuwa na mwanaume *_bongo lala_* kama huyu? Labda awe AMELOGWA. Hivi hapo nani Atakuwa AMEOLEWA?
Mkiitwa
_WANAUME SURUALI_ mnakasirika, Lakini mpaka hapo hilo jina ni HALALI YAKO kama haulitaki *BADILIKA.* Hauna HAKI ya kuitwa MWANAUME kama HAUWEZI
KUWAJIBIKA.
VIJANA ACHENI UJINGA MUDA HAURUDI NYUMA
@maisha_halisitz
Imepenya naamini hata kama ukinuna
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: