Nikiwa Kitandani Kwangu Leo Asubuhi Nikawa Natafakari Na Kujiuliza
Nikiwa Kitandani Kwangu Leo Asubuhi Nikawa Natafakari Na Kujiuliza "Ni Nini Siri Ya Mafanikio, Nifanye Nini Nifanikiwe?" Majibu Ya Kufanikiwa Nikayapata Mulemule Chumbani Kwangu.
Kale Kaubaridi Kaasubuhi Kakaniambia Niwe Cool Nisikurupuke, Dali Ikaniambia "Fikiri Juu Zaidi", Madirisha Yakaniambia "Tizama Nje Uone Fursa Zilizopo Ulimwenguni", Saa Ya Ukutani Ikaniambia "Kila Sekunde Ina Thamani Sana Katika Maisha, Muda Ni Mali."
Kioo Kikaniambia "Jitizame Na Ujiamini Kabla Hujafanya Jambo". Kalenda Ikaniambia, "Mwaka Wako Wa Mafanikio Ndio Huu." Mlango Ukaniambia "Sukuma Kwa Nguvu Kwa Ajili Ya Malengo Yako." Choo Kikaniambia "Flash Tabia Zako Zote Mbaya Zinazokufanya Uendelee Kuwa Chini." Kitanda Kikaniambia "Inuka Bwana Mkubwa Umenilalia Vya Kutosha Nimechoka"
Na Nilipokiona Kitabu Cha Dini Kikacheka Na Kuniambia "Nisome Mimi Kwa Ajili Ya Kuenenda Njia Zilizonyoka, Ili Mwovu Shetani Asikupate."
Nikaamka Nikiwa Na Nguvu Mpya Pamoja Na Matumaini Mapya!
Mwenyezi Mungu, Abariki Kazi Halali Za Mikono Yetu, Sisi Ni Vichwa Na Wala Si Mikia.
**AMEN**
Dr 🅱❤
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: