NATAMANI MKE WANGU ANIAMINI TENA, HAKUNA TENA RAHA YA KUCHEPUKA KAMA HANIFUATILII!

UTAMU KITANDANI APP
Habari, sikufahamu lakini kuna kitu kimetokea ikabidi nikutafute. Katika miezi miwili hivi mke wangu alibadilika sana, mimi kweli nilikua nachepuka na ilikua ni ya waziwazi, alikua anajua na kama wanaume tunavyojisemea haendi popote basi hata mimi nilijua hivyo. Sikujua sababu ya kuchepuka lakini nilikua najiambia tu siwezi kuwa na mwanamke mmoja.
Nadhani kitu kingine kilichokua kikinifanya kutokua karibu na mke wangu ni kisirani chake, kila siku tulikua tunalumbana na kugombana hasa kuhusu X wangu ambaye hata nilikua sitembei naye lakini yeye alijua kua natembea naye. Nilishazoea huo usumbufu na sikuona haja ya kubadilika kwani kusema kweli nilikua sipati raha yoyote kurudi nyumbani, mke wangu hakua rafiki yangu.
Lakini miezi kama miwili iliyopita alianza kubadilika, alikua halalamiki tena, hata nikirudi usiku hanuni tena, kuna kipindi nilifanya makusudi hata kurudi asubuhi lakini hakujali. Nilishtuka kwani nilihisi kua anachepuka, ingawa tulishaacha kufanya mapenzi muda mrefu mimi ndiyo nilikua sitaki kwani nilikua si enjoy lakini nilimuonea wivu.
Nilimuuliza kama ana mtu lakini alibisha na kuniambia kua ameamua kuwa na furaha, sikumuelewa, nilizidi kumfuatilia na sikuona chochote. Niliamua kumuomba game lakini aliniambia haniamini, aliniambia kama nataka kumgusa basi tukapime kwanza au tutumie kinga kwani ulishapita muda mrefu nafanya mambo huko nnje na yeye haniamini tena.
Nilikasirika, si kumpiga lakini nilikasirika na kujua ni lazima atakua na mwanaume anampa kiburi. Nilichunguza sana, nika hack simu yake ya Whatsapp, Facebook yake na kila kitu lakini sikujua. Mke wangu aliacha kuwa na kisirani, akawa na furaha na mimi ndiyo nikaanza kuwa na kisirani kwanini yeye ana furaha, niliwaambia rafiki zangu na wote waliniambia kua anachepuka niwe makini.
Ni miezi ambayo ilinisumbua sana kwani nilikua naamini anachepuka lakini sikujua na nani. Juzi ndiyo niliona kakutumia meseji katika Whatsapp, alikua anakushukuru kuhusu Kitabu chako na kukuambia kua sasa hivi ana furaha kwani ameamua kujipa raha mwenyewe. Ulimtumia Kitabu kwa E-mail hivyo sikukiona Whatsapp, niliamua kuongea naye na kumuuliza kuhusu wewe kabla ya kukupigia.
Alinieleza kuwa amechoka kulia kila siku, kachagua kuwa na furaha kwakua maisha ni mafupi, kweli nikiangalia mke wangu aliacha kuishi kwaajili yangu na kuishi kwaajili yake. Hata watoto nao walikua na furaha kwani Mama yao aliacha kuwa kisirani. Nilikua mkali na kumuambia sitaki akusome tena aliniambia yeye ashapona na hawezi kuwa na huzuni tena kwani ndoa si kuvumiliana mateso bali ni kuvumilia shida.
Aliniambia kabisa kama nikifukuzwa kazi atanivunamilia, kama nikiumwa atanivumilia na nikipata matatizo yoyote atanivumilia lakini kamwe hatavumilia manyanayso, vipigo na usaliti. Kweli alisimamia msimamo wake, akawa na furaha na mimi nikawa na kisirani, nimejikuta na mimi narudi nyuma kwani sina furaha tena, sioni tena raha ya kuchepuka kama mke wangu hanifuatilii, nimekubali tukapime na tutatumia condom mpaka tukipima mara ya pili.
Nilishakupigia simu tukaongea ila naomba uandike kisa changu hiki kwani mke wangu anasoma ukurasa wako naomba umuandikie ili ajue kuwa nimedhamiria kubadilika kwani hakuna chochote nilichokua napata huko nnje. Naamini akisoma kupitia ukurasa wako ataniamini kwani nilishamfanyia mengi mabaya ambayo hata kunisamehe nimeshangaa. Nashukuru kwa muda wako na nashukuru kuwa umekua ukiandika na kuwaamsha watu.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.