*MAKOSA YA MWANAUME YANAYOSABABISHA MKE AMSALITI*
.... _Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:_
*1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI*
...... _Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya... atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla..._
...... _Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia..._
...... _Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume... mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa._
*2. UKOSEFU WA MAHABBA*
...... _Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa... Mwanamke anahitaji kupendwa... mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono... ukimpa ngono tu basi, anaridhika... mwanamke anahitaji kuengaengwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu... mwanamke anataka hivyo.. anataka aone kama anapendwa... anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake... ampe lugha ya kimajnun... mwanamke anamtaka Majnun... sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu... mnanipata hapo?_
*3. USALITI WA MUME*
...... _Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti... Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa... Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi..._
*4. KUTOJIAMINI*
...... _Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini... iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza Kutokea mengine kabisa... Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya..._
🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰 *MAFUNZO YA NDOA*🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰🌰
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: