Hakuna dharau kubwa kwa mwanamke kama Hii.
Kutoka kwa Brayton official❤
Hakuna dharau kubwa kwa mwanamke kama vile mwanaume ambaye alikua mpenzi wako halafu akaoa mwanamke mwingine halafu anarudi kwako anakuambia bado anakupenda anataka kufanya tena mapenzi na wewe. Hapa naamanisha bila kujali sababu za yeye kukuacha kama alikuacha na kwenda kuoa mwingine halafu bado anakutumia kingono basi jua kuwa sio kwamba anakupenda na anashindwa kukusahau hapana ni kwamba amekudharau na anakuona mpumbavu.
Hata kama alikuacha kwakua mmetofautiana Dini, hata kama alikatazwa na wazazi wake hata kama ni wewe ulimuacha, lakini kama mliachana na akarudi kutembea na wewe baada ya kuoa basi jua kuwa kakudharau. Kwanza kabisa anajua kabisa hujithamini ndiyo maana kwako anakua kimwili na kwa mkewe anaenda kutengeneza maisha. Lakini ni kama anajihakikishia kuwa huyu si mwanamke wa kuoa kabisa na alifanya maamuzi sahihi.
Iko hivi moja ya wanawake ambao wanaume huwadharau ni wanawake ambao wanatembea na waume za watu tena bila malengo. Lakini atakua amekuona mpuuzi kabisa kama wewe utakua umeolewa na mwanaume mwingine halafu ukarudiana na yeye, huyu mwanaume hatakuheshimu na kwani anajau kua huithamini ndoa yako.
Hata kama ikitokea ukaachika kwa mume wako basi jua kuwa kama livyokuacha mara ya kwanza na kuoa mwingine hatamuacha mkewe kwaajili yako. Hii ni kwasababu anajua kuwa wewe si mtu wa kuaminika ni kicheche. Wanaume tunapenda sana kusaliti lakini si kusalitiwa. Anajua kuwa kama ulimsaliti mumeo na X wako basi hata yeye unaweza kumsaliti na X wako hivyo ni vigumu sana kuendelea na mahusiano baada ya kuona umeachika.
Najua unadhani unamkomoa mke wake, tena kwakua anaonyesha kukujali kuliko mkewe, hata wakati mwingine kutumia muda mwingi na wewe na kumtukana au kumnyanyasa mbele yako ukafikiri wewe una thamani zaidi. Hapana anajifanya nikua anakuridhisha tu, anajua mkewe hawezi kuondoka hivyo ili kukushikilia wewe na kuendelea kukutumia nilazima aonyeshe kama vile anakujali wewe zaidi kuliko mkewe ili usiondoke!
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: