DADAZANGU SOMENI HAPA CHINI HALAFU MUONE AKILI ZA WANAUME ZILIVYO🤣🤣🤣
wanaume msiwe kama huyu mpumbavu.
Naomba ushauri wako, mimi sijaoa nina miaka 37, nina watoto wanne ambao niliza ana dada mmoja, tuliishi naye kwa miaka 10 kwenye mahusiano nikajaga kupata mwanamke mwingine nikamuacha, mimi nilipata uhamisho wa kikazi. Sikumuacha kwa kumuambia hapana, nilikaa tu kimta akawa ananitafuta sijibu mseji zake wala nini?
Si kwamba nilikua simpendi hapana, nilipata mwanamke mwingine ambaye tulianzisha mahusiano hivyo kwakua nilishamzalisha ana watoto wanne nikajua kuwa hawezi kuniacha. Yeye ana kazi hivyo watoto alihudumia mwenyewe na mimi nilikua najenga hivyo nikaona haina shida siku nikiwa tayari nitamrudia tutaendelea. Tulikua na miaka mitatu ya bila mawasiliano.
Kusema kweli nilikosea lakini bado nampenda kwakua najua ni mwanamke anajituma, watoto wanaosma shule nzuri alikua anasomesha na hata kuna kipindi Mama yangu alikua anaumwa alimsiadia sana ingawa hakua akiishi kwetu, yote hayo niliambiwa na Mama mwenyewe, kabla ya kufariki aliniambia kuwa huyo ndiyo mwanamke, alikua ananisisitiza san akumuoa ila nilikua sijawa tayari.
Sababu ya kuja kwako ni hivi, juzi niliona kapost kwenye instagram anavalishwa pete, nilishtuka sana nikaamua kufuatilia. Niliambiwa kuwa amepata kija anamuoa, yaani nilishangaa kwani yeye ni mtu mzima ana watoto wanne na sasa hivia an miaka 33. Mwanzo nilijua labda ni kija a mdogoa anamlea lakini baadaye nimechunguza huyo Kaka yuko vizuri na kwao wako vizuri.
Sasa nashindwa kuelewa hivi kuna mwanaume kweli anaweza kuoa mwanamke wa watoto wa nne? Nampenda sana lakini nashindwa kujua nifanye nini ili kurudiana naye. mimi nina miaka 37, siwezi pata mwanamke mwingine nakuanza familia nyingine, sina uwezo huo, nataka kurudiana na mke wangu ili kutengeneza familia na tuishi na watoto wetu, natamani kumuambia kama anaolewa anipe watoto ili aachane na huyo mtu lakini sijajua kuwa kisheria imekaaje?
Najua hawezi kukubali kuniachia watoto hivyo kama nikikomaa anaweza kunirudia, sifanyi kwa ubaya ila nafanya kwa mpenzi, najua ananipenda na mimi nampenda nilifanya makosa, naomba nishauri nitumie njia gani ili nikienda kuongea naye niweze kumshawishi asifunge hiyo ndoa kwani naona kama anafanya makosa, anaolewa kwakua anadhani nimeshamuacha kumbe mimi bado nipo naye na nampenda.
NB;Kuzaa sio kushuka thamani wanaume wengi huwa wanapenda kuwakomoa wanawake hasa wakiona wameanza kufanikiwa ishini nao kwa tahadhali
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: