Je, Ni sahibi Baba kumnunulia binti yake Pedi???


Siku hizi nimekuwa nikiwaona baadhi ya akina Baba ambao binafsi nawaita wa ' hovyo hovyo ' wakija na Mabinti zao tena wakubwa tu Madukani na hasa katika Supermarkets mbalimbali na kuwanunulia ' Pedi ' tena kuna wakati unakuta ' Li Dingi ' hilo hilo bila hata chembe ya aibu linamchangulia ' Bintiye ' aina ya ' taulo ' za kutumia.

Kama hii haitoshi hivi punde tu wakati na Mimi nikipanda Mti wangu nilioubatiza ' Le Mathematicien GENTAMYCINE ' niliweza kumsikia ' mubashara ' kabisa Baba mmoja akiongea na Simu na Mtu mwingine kuwa akimaliza tu kupanda Mti anataka kupitia dukani kumnunulia ' Bintiye ' taulo za Kike ' Pedi ' kwani alipotoka tu nyumbani kwake asubuhi hii alivyomuona tu alihisi kuwa ameanza safari yake ya kwenda ' Moon '.

Najua humu kuna akina Mama zetu na Wazee wenye MAADILI kabisa hivi haya mambo ya ' hovyo hovyo ' wayafanyayo Wazazi wa siku hizi hasa wa Kiume kwa Mabinti zao hususan kuwanunulia ' Pedi ' na kujua kuwa wapo ' Moon ' wamerithi kwenu nikimaanisha kuwa na nyie huko nyuma mlikuwa mkifanyiwa hivi au ni ' Uzungu ' tu umetuharibu na tunakosa maadili na kujua mipaka ya Baba juu ya Binti yake ambaye ni mkubwa na ameshavunja Ungo?

Badilikeni Wanaume wenzangu na akina Baba na jifunzeni kujua mipaka yenu hasa kwa Mabinti zenu.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.