ISHA MASHAUZI AELEZA SABABU YA KUPEWA TALAKA


Muimbaji wa muziki wa Taarabu na BongoFleva Isha Mashauzi, amesema sababu zilizofanya aachane na aliyekuwa mume wake ni kutokana kuchezea kichapo kwenye ndoa.

Akiieleza EATV & EA Radio Digital Isha Mashauzi amesema, endapo mtu atampiga wakiwa kwenye mahusiano hataweza kuendelea naye, na hiyo ndiyo sababu ilimfanya aombe talaka kwa mume wake.

"Mtu akinipiga kwenye mahusiano hawezi kuendelea na mimi, yaani mtu akishanipiga jua kabisa tumemalizana hapo, nilishawahi kupigwa na nikamalizana hapohapo na aliyekuwa mume wangu wa ndoa, nikamwambia aandike talaka na akaandika akanipa" ameeleza.

"Kitendo cha mtu kunipiga kwenye mapenzi jua hapo ni shubiri tena mahaba yanakuwa  yameshakufa. Kumpiga mkeo au mchumba wako inamaanisha mapenzi hakuna tena, mtu anayetakiwa kupigwa ni mtoto tena na mzazi wake kwa sababu wanajua kuna mafunzo wanampa"  ameongeza


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.