USIMFICHE MKE WAKO MALI ZAKO LAKINI MFICHE PESA ZAKO!
Najua hiki kichwa ha habari tu kishaanza kuwapanikisha watu na kuwatoa povu. Lakini ukweli nikuwa, mwanaume ukishaoa hakikisha kuwa unakua na pesa ya ziada ambayo mwanamke haijui. Hii ni pesa ya dharura, kwamba hata kama mishahara yenu wote mnaweka mezani lakini mtoto hawezi kuumwa ukamgeukia Mama na kumuambia “Pesa yote nilikupa wewe ushike!” hakuna kitu kama hicho, hata kama ulimpa ila hatakuelewa.
Iko hivi, kuna tofauti ya Mali na Pesa, mali ni vitu kama nyumba, magari, mashamba, Biashara na uwekezaji vingine. Hivi mke wako anapaswa kuvijua kwani ni mke wako na likitokea la kutokea yeye ndiyo anatakiwa kusimamia kwa niaba ya wanao. Lakini pesa ni kipato cha mpito, leo una elfu kumi kesho una laki. Sasa mwanaume yeyeote ni lazima uwe na akiba flani ambayo mke wako haijui kabisa, narudia haijui kabisa si nyingi kihivyo lakini akiba ambayo unajua kuwa likitokea tatizo la ghafla huendi kuangaliana na mke ndani na wote kulia.
Kiasilia wanawake huamini kuwa wanaume wakati wowote wana pesa, hivyo akiziona atataka kuzitumia zote kwakua tu anaamini una nyingine huko umeficha, sasa akizitumia na wakati huna nyingine jua kuwa hata kama ni msahahara wote ulimpa, ikitokea shida basi atakuja kwako. Lakini wanawake wanaendeshwa kwa hisia na wanapokutana na matatizo hupaniki na hushindwa kitu cha kufanya hivyo kumgeukia mwanaume.
Kwa mfanp mtoto anaumwa yuko mahututi, Mama kwanza ataanza kulia, kapaniki hajui chakufanya. Sasa hapa ndipo mwanaume unatakiwa kusimama, wakati yeye analia wewe unapambana lakini sio anakugeukia unamuambia pesa yote si nilikupa. Nikuambie ukimpa jibu hilo yeye kuokoa mtoto hatajali, anaweza kukopa na hata X wake akimpigia hatajali, akili haitafanyakazi haraka. Ni lazima kama mwanaume kujua kuwa wewe ndiyo unapaswa kuwa na majibu, hivyo hakikisha unakua na akiba ambayo ipo tu.
Sio kwamba hata unamficha, hapana, humuambii, sio mke wako kafiwa unaanza kumuambia msahahara wote si nilikupa. Ubaya nikuwa ukishampa mwanamke pesa basi jua kuwa anajua zote ni zakutumia wewe una nyingine. Kwa maana hiyo hata kama huna yeye anaamini kuwa mwanaume huwezi kutoa pesa zote, liklija tatizo kubwa basi anajua utalibeba. Hivyo weka akibal mfiche kuhusu pesa lakini si mali, mali ajue lakini pesa asijue mpaka shilingi kumi yako yote!
#SHARE
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: