SIO KWELI KWAMBA WANAUME BORA HAWAPO SIKU HIZI, UKWELI NI HUU.
Sio kweli kwamba wanaume bora hawapo. Wanaume bora wapo ila ni ngumu mno kuwavutia. Kama mwanaume nafahamu fika wanaume bora sio tabu kuwapata, ila tabu kubwa ni jinsi ya kuwavutia.
Sio tabu kuwapata kabisa, ila tabu ipo kwenye ku-win attention yao. Ukweli ni kwamba, wanaume bora wanao ubora kwa sababu wapo kwenye ligi yao inayothamini ubora pekee. Hata siku moja hawadanganyiki kirahisi na urembo wa dukani na ushawishi wa kingono ambao baadhi ya wanawake wanafanya.
Nisieleweke vibaya hapa. Wanaume hao sio kwamba hawaoni hayo mambo kwa wanawake wanaofanya hivyo, la hasha, wanaona sana lakini hawafanyi maamuzi ya kua katika mahusiano au kuoa kwa ku-base kwenye hayo mambo. Hivyo basi;
-Kuvaa vimini na nguo za mitego, Kubusti maziwa, na kupost drama drama kwenye mitandao ya kijamii kutafanya upate wavulana ambao ni sex-oriented..yaani wanaowaza ngono basi. Ila itakuwa ngumu kuwavutia wanaume wanaojielewa.
Kuwavutia wanaume bora na wanaojielewa unatakiwa ufanye kazi zaidi ya hiyo. Uonyeshe tabia yako njema badala ya drama za mitandao ya kijamii, akili yako badala ya sura na shepu yako..na muhimu zaidi upendo wako kwa Mungu kuliko kupenda zaidi fashion.
Kupata attention ya mwanaume aliye bora ni lazima uwe kimkakati zaidi kuliko kuwa kimaslahi zaidi.
Muda mwingine, mwanaume wa ndoto yako yupo katika ngazi za juu ambapo wewe kama mwanamke unatakiwa uwepo.
Ni mpaka utambue hilo na kupanda ngazi kiimani, thamani, kiroho, emotionally na vilevile kitabia, vinginevyo utakua umejifunga na huyo mwanaume hataweza kugundua kuwa wewe ni wife material.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: