ALIANZA KWA UPENDO NA KUKUJALI ILA SASA HIVI HATA SMS KUJIBU NI SHIDA UNAJUA KWANINI?

UTAMUKITANDANI APP

Alianza na upendo wa hali ya juu kwako, anakupigia kila wakati, anakutumia ujumbe mfupi kila mara, anatamani kuonana na wewe karibu kila siku, ukimwambia kwa suprise baby nataka kuja kwako saizi anakwambia hakuna tatizo njoo tu my love, hajawahi kukuchoka, hata ulipomgia simu sanane za usiku alimka na kupokea na aliongea kwa furaha na amani sababu alikupenda. Muda wowote ulipomtumia ujumbe mfupi alikujibu kwa haraka sana wala hakutoa kisigizo kuwa saizi ana kazi nyingi.

Aliona wewe ni muhimu kuliko kazi ndiyo maana aliweza kutumia dakika moja kujibu au kupokea simu yako, hakukata simu yako wala hakupitisha siku bila kukupigia bali pale alipokuwa busy sana alikwambia baby nitakupigia na kweli alipomaliza kazi zake alikupigia sababu alikupenda.

Saizi unapiga simu hapokei, akipokea anaongea kama umemlazimisha kuongea hana furaha tena na wewe, hataki kuiona simu yako, yaani anaona umekuwa msumbufu kwake. Hataki kabisa ufike kwake hata moto ukiwa unawaka akiambiwa wewe unakuja kumsaidia yupo tayari vitu viungue wewe kwake usikanyage, saizi ukituma ujumbe mfupi unaweza kujibiwa baada ya mwezi au usijibiwe kabisa, huijui hata sura yake maana hujaonana naye muda mrefu.

Ukiona hivi hapo penzi limefika mwisho na hiyo unayopewa ni ishara kuwa hautakiwi tena na huenda nafasi yako ameshachukua mtu mwingine, yale mapenzi yaliyokuwa kwako yamehama na upepo na kwenda kwa jirani. Hupaswi kuumia kwanini imetokea hivi bali jiulize kwanini amekufanyia hivi?

Unakosea wapi, kitu gani umepunguza, kwanini umeshindwa kumridhisha. Watu wanasema kugundua tatizo ni nusu ya kulitatua tatizo hilo sasa kama umeachwa, au mpenzi wako amebadilika na ukashindwa kugundua ni kwanini amekuwa hivyo basi jiandae kuachwa tena kwani huenda ukarudia makosa yale yale yaliyomfanya mpenzi wako akukimbie, akuache au abadilike kitabia.

Msome mwenzako anapenda nini na nini hapendi, kuwa mbunifu katika mapenzi yenu usiweke mazoea, lakini kikubwa mjengee imani kwani mapenzi ya kumuamini mpenzi wako ni tatizo jingine.
Na uwe makini ukiona wewe ndio umekua mwenyekiti wa hayo mapenzi hebu kaa pembeni uone kama yatendelea ua la! Maana unaweza Dhani mnapendana kumbe wewe ndio unapenda
@maisha_halisitz

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.