Simulizi : Penzi La Mfungwa Sehemu Ya Tano (5) MWISHOOOO


"Naam. Dawa ya mzizi tayari sina mwilini,dawa ambayo ingenifanya nipotee katika mazingira yoyote. Sasa nimebaki na hirizi,hii ni dawa ambayo itanipatia nguvu nyingi katika mwili wangu. Laiti kama ile dawa ningekuwa nayo,basi nisingetumikia jela mimi. Mimi ni Zabroni, hata hivyo sitokubali. Kupitia hirizi hii hii nitatoroka humu nikalipe kisasi,kamwe mwanamke hawezi kushindana na mimi. Kamwaga mboga acha mimi nikamwage ugari", yalikuwa ni mawazo ambayo Zabroni alikuwa akiyafikiria ndani ya kichwa chake, muda huo akiwa amelala usiku na wafungwa wenzake.
Kesho yake palipo pambazuka,Zabroni alikuwa mtu wa kwanza kuamka kabla hata kengere haijagongwa. Bluyner alikuwa mtu wa pili kuamka,ambapo alishangaa sana kumuona Zabroni kadamka sana kuliko siku zote tangu aanze kutumikia kifungo chake cha maisha jela. Bluyner aliachia tabasamu la kebehi kisha akasema "Naona leo umekuwa mtoto mtiifu,bila shaka shauri ya kipigo ndio imekufanya leo uwe mtiifu",alicheka kidogo halafu akaendelea kusema "Kwa muendelezo huu utafaa kuwa mke wangu kwani mimi napenda sana mwanamke mtiifu hasa kama wewe,sawa?..",alisema Bluyner akimdhihaki Zabroni ilihali wakati huo Zabroni aliishia kumtazama bila kujibu chochote. Bluyner baada kuona Zabroni yupo kimya alizipiga hatua kumsogelea ,alipo mfikia aliusogeza uso wake jirani kabisa na uso Zabroni kisha akambusu. Kitendo ambacho kilimkera Zabroni,alipandwa na hasira moyoni mwake. Alikunja ngumi nzito Kwenye mkono ule aliovaa hirizi kwa nia ya kumpiga Bluyner. Lakini kabla hajairusha ngumi yake,ghafla alishikwa mkono. Hapo aligeuka nyuma akamtazama aliyemshika mkono, ni moja ya wafungwa wenzake mule gerezani anaitwa Steve swahiba wake sana Zabroni gerezani. "Zabroni braza, na braza Bluyner. Tunafahamu fika nyie ni miamba ndani ya hii jela,ingawa Zabroni bado hujaonyesha umwamba wako lakini simulizi fupi ya maisha yako inajidhihirisha kuwa wewe ni mwamba. Aamh Kaka Bluyner. Wewe ni mwamba pia,kila mmoja ndani ya hili gereza anafahamu kimbembe chako. Hivyo basi haina maana kutunushiana misuri asubuhi yote hii,heri mpange siku moja mkutane ndipo muanze kuonyoshena umwamba",alisema Steve huku akiwaamulia vijana hao ili wasipigane. Ukweli ni kwamba Zabroni safari hii alipania avunje ukimya lakini baaada kupewa maneno hayo na swahiba wake aliona bora atulize hasira zake ili siku moja amuadabishe mbele ya wafungwa wenzake.
Na mara baada Steve kuwaamulia wanaume hao,punde si punde kengere ya kuawamsha wafungwa iligongwa. Ndipo wafungwa wote walipotoka vyumbani haraka sana wakawahi mstarini kuhesabu namba. Amabapo zoezi hilo lilichukua dakika kadhaa likawa limekamilika,hatimaye walipewa uji waakanywa kwa muda mfupi sana wakawaa wamemaliza. Shughuli ikawa imebaki kwenda shambani kulitumikia taifa kwa nguvu bila kubembeleza,maisha ambayo kijana Zabroni aliyachukia sana kiasi kwamba roho ilimuuma ilihali hasira zake nyingi akiashumu ni kitendo gani atakacho mfanyia Veronica ikiwa kama njia sahihi ya kulipa kisasi juu ya kile alicho mfanyia.
"Acha kuzubaaa panda gari twende kenge wewe",ilikuwa ni sauti kutoka moja ya Askari magereza aliyekuwa akimwambia Zabroni ambaye alionekana kusweta na usongo wa mawazo. Zabroni aligeuka kumtazama huyo Askari aliyemwambia hayo maneno kisha akarudisha uso wake kunako gari lile lililosheni wafungwa,akapanda safari ikawa imeanza.
Upande wa pili,Bruno ama Mr Rasi alikuwa mtaani akitembea tembea hana hili wala lile. Hatimaye alikatiza moja ya mitaa ambapo huko alikutana na kundi la watu wakifanya dili haramu,dili hilo lilikuwa la mapigano. Umati wa watu ulikusanyika mahali hapo wakishangaa ngumi hizo huku pembeni napo vikionekana viti wakiwa wamevikalia vibopa ama kwa lugha nyepesi unaweza kusema matajiri. Ngumi zililindima ,shangwe zililipuka kutoka kwa watazamaji. Na mwisho wa pambano ilisikika sauti ikisema "Vipi Bwana Karani,unamwingine tena?..",sauti hiyo ilisikika kutoka kwa mmoja wa bosi aliyekuwa mahali hapo akipambanisha watu wake na watu wa bosi mwingine,hiyo ikiwa kama njia ya kusaka pesa. Bosi huyo aliitwa Derick. Karani alishusha pumzi kisha akajibu "Sina,ila siku zote usikariri maisha. Sio kila kobe akiinama basi anatunga sheria,hapana kombe wengine wanawaza akupe hukumu gani?.."
"Hahahahaah",alicheka Derick baada kusikia msamiati wa Karani,baada ya kicheko akajibu "Sawa sawa. Lakini epukana na zogo za ubunuasi kaka,tukutane SOPHIE HOTELI unipatie pesa zangu. Ukiitaji ligi tena mimi nipo tayali " alisema Derick. Mr Rasi,yote hayo aliyasikia. Hivyo aliona hapo ni mahala pakupiga pesa lakini pia ni sehemu sahihi pakujificha ili mkono wa dola usimfikie akiamini kwamba matajiri hao mpaka wanaamua kuanzisha biashara hiyo haramu basi lazima kutakuwa na kitu wao na serikali.
"Nijikosheje mbele yao? ",alijiuliza Mr Rasi wakati huo watu walionekana kusambaa baada ya mpambano kumalizika. Kabla hajapata jibu,mara ghafla kundi la vijana wasio pungua saba walimzunguka. Mr Rasi alistuka kuwekwa kati wakati huo huo kijana mmoja kati ya wale sababa akimwambia "oya! Unaonekana mgeni sana haya maeneo. Naomba utuambie umefuata nini sehemu hii?..". Mr Rasi hakumjibu. Kitendo ambacho kilimkera sana yule kijana ambapo alirudia kuhoji kwa sauti ya juu "Umefuata nini?..",bado Mr Rasi hakujibu. Hapo ndipo yule kijana alipowaamuru vijana wenzake sita wampige Mr Rasi. Ndani ya nafsi yake Bruno akasema "Naam! Ama kweli mwanaume siku zote halali na njaa ila atachelewa kula. Acha niwaonyeshe" ,kichapo kiltembezwa hapo. Tajiri Derick hakushuhudia ule mpambano ila tajiri Karani aliushuhudia namna Mr Rasi alivyokuwa akiwapa dozi wale vijana waliojifanya watoto wa mjini.
"Bosi huyu jamaa hutakiwi kumuacha",alisema mmoja wa mpambanaji wa Karani. Karani hakujibu,aliendelea kumtazama Mr Rasi huku akitabasamu. Moyoni akajisemea "Yes kijana mtamu sana huyu ananifaa kivyovyote vile. Ahahahaaa Derick umekwishaa " ,alimaliza kwa kicheko Karani,ilihali upande wa pili umati wa watu kutoka maeneo mbali mbali walikusanyika kuja kushangaa huo ugomvi,kwa maana wale walinzi waliokuwa wakilinda pembeni kuwazuia baadhi ya watu,nao waliondoka baada kusikia kwamba kuna mpambanaji anapigana na watu sita mmoja wa nyogeza. Jumla watu saba. Hivyo kitendo kile cha kuachia muanya kiliwafanya watu kuja kwa wingi sana kushuhudia hilo pambano la Mr Rasi na hao wahuni wa mjini. Ndani ya watu hao waliokuja kutazama mpambano alikuwemo na Tina,safari hiyo Tina alikuwa na shangazi yake. Tina alifurahi sana kumuona Mr Rasi kwa mara nyingine tena. Aliachia tabasamu pana huku pole pole moyo na nafsi yake ikionyesha kuvutiwa na mtu huyo. Mr Rasi ama Bruno adui yake Zabroni,wakati huo huo Zabroni na Tina ni wapenzi.
Kwingineko baada ya shuguli kumalizika, wafungwa walitulia kwanza kabla hawajapanda kwenye magari yao ili kurudishwa gerezani. Nafasi hiyo sasa Bluyner aliitumia kumchoza Zabroni ili wapigane,baada ya pambano kila mmoja ajulikane nani mwamba. Bluyner alimuita mmfungwa mmoja kisha akamtuma kwa Zabroni. "Sikia, nenda kamwambie Zabroni kuwa mumewe namuita". Upesi mfungwa huyo alimfikishia ujumbe Zabroni kama ulivyo, Zabroni akajua fika kuwa tayari Bluyner anahitaji pambano,Kwahiyo kwa kuwa hirizi anayo akaona hakuna haja ya kuogopa. Hivyo naye alimtuma mfungwa mwingine akamwambia "Kwambie Bluyner Zabroni kasema ipo siku atakulawiti",Tusi hilo lilipomfikia Bluyner alikasirika, hima akamfuata Zabroni kwa niaba ya kupigana. Zabroni kwa sauti akasema "Sikilizeni hakuna kuingilia kati", maneno hayo Zabroni aliyasema kwa hasira huku akiwa tayari kupigana huku akiwa na nia moja tu mara baada ya pambano hilo asirudi Gerezani. Moja kwa moja atoroke akalipe kisasi kwa Veronica pia akamalizane na Bruno. Mr Rasi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada Zabroni kuwataka wafungwa wenzake wasiamulie ule ugomvi,upande wa pili nako Askari waliokuwa wakiwasimamia waliambizana kwamba waache waone nani mbabe. Hivyo walijifanya wako bize kupiga zogo ilihari huku wafungwa tayari wameshaweka uzio kwa duara ili kuangalia mpambano. Mtu wa kwanza kurusha ngumi alikuwa Bluyner, alirusha kumi na mateke harakaraka yaliyomfanya Zabroni kurudi nyuma akiyakwepa mateke hayo. Lakini licha ya kurudi nyuma ila teke moja lilimpata,Zabroni akawa ameanguka chini. Nafasi hiyo Bluyner akaitumia kujirusha juu mfano wa sama soti kisha akatua moja kwa moja kwenye kifua cha Zabroni. Zabro alitema mate ya damu,wafuasi wake wakashika vichwa vyao ilihari upande wa wafuasi wa Bluyner wao walilipuka shangwe huku wakimtaja Bluyner kwa kumshangilia. Upande mwingine yule Askari aliyempatia Zabroni hirizi alionekana kusikitika pia kuingia na hofu,alihofia uwezo wa Zabroni kupigana Bluyner kijana ambaye alionyesha uwezo wa juu kupigana.
"Amka sasa nikunyooshe! Amka sasa kama unayaweza",alisema Bluyner huku akipiga kifua chake. Zabroni aliweka mikono yake kifuani kudhihirisha kwamba kaumia eneo la kifua. Baada ya hapo alinyanyuka kisha akasimama ila kabla hajakaa sawa,Bluyner aliruka juu kwa mara nyingine akiwa angani alirusha mguu wa kulia juu ya kichwa cha Zabroni, na mguu wa kushoto ukawa umempata ambapo Zabroni alianguka chini kama mzigo kisha akaanza kupumua kwa shida. Pigo mbaya sana hilo alilopigwa kichwani kiasi kwamba alihisi Malaika mtoa roho anamnyemelea. Wakati huo huo Bluyner alimsogelea akachuchumaa chini akamtazama usoni,akacheka kisha akasema "Zabroni, wewe huna uwezo wa kupigana na mimi. Amini kwamba walionichangua kuwaongoza nyinyi abadai hawakukosea,sasa iweje uthubutu kuangusha mwamba ulio shindikanika?", akacheka Bluyner kwa mara nyingine tena halafu akaendelea kusema "Umepima maji kwa kijiti pasipo kujua kuwa mahali hapa kuna kina kirefu,kwanini usizame? ", kwisha kusema hivyo alirudia tena kucheka kisha akakunja ngumi kwa niaba ya kumpiga Zabro lakini kabla hajaishusha ngumi,Steve alifika haraka sana akamshika mkono ule uliokuwa umekunja ngumi. Wakati huo upande wa pili Askari waliokuwa na jukumu la kuwarinda na kuwasimamia hao wafungwa,wao walikuwa kando wakishuhudia huo mpambano. Askari mmoja kati yao alipotataka kuingilia kati alizuiwa na yule Askari aliyemrudishia Zabroni hirizi. Hivyo ikabidi watulie waangalie nani bingwa ingawa Askari huyo aliyempa hirizi Zabroni, moyoni hakuwa na amani kama Zabroni ataweza kuibuka kidedea.
"Bluyner, tafadhali naomba umuache. Tayari umejizihirusha kuwa wewe ni nwamba. Naomba usiendelee kumpiga utamuuwa kaka nielewe tafadhali", alisikika akisema hivyo Steve huku akiwa ameung'ang'ania mkono wa Bluyner uliokunja ngumi. Bluyner alifura hasira mara dufu ambapo alinyanyuka kisha akamtazama Steve usoni,Steve aliogopa lakini hakusita kumuombea msamaha rafiki yake kipenzi. Bado aliendelea kumuombea msamaha Zabroni,kitendo ambacho kilipelekea kipigo kuhamia kwake. Alipigwa sana Steve wakati huo Zabroni pale alipokuwa amelala ghafla kumbukumbu ilimjia, ambapo alikumbuka maisha ya nyuma kidogo kabla ile dawa iliyomfanya asumbue kila mahali haijapotea mwilini. "Mimi ni Zabroni! Mimi ni Zabroni",nisauti ambayo ilikuwa ikijirudia kichwani mwake wakati huo akikumbuka baadhi ya matukio aliyowahi kufanya. Alikumbuka jinsi alivyomtumbua mama mjamzito, alikumbuka ugomvi mkubwa aliowahi kupigana na Madebe pia Bruno ambaye kwa sasa Mr Rasi. Yote hayo ikiwa ni ndani ya kulipa kisasi cha wazazi wake ingawa marehemu Madebe na Mr Rasi waliingilia ugomvi huo ukiwa hauwahusu. Basi kumbukumbu za Zabroni hazikuishia kwenye matukio hayo tu lahasha alikumbuka zaidi mpaka alivyozama kwenye penzi la Afande Veronica pasipo kutambua kwamba Veronica ni Afande na yupo kwa niaba ya kumtia katika mikono ya sheria,jambo ambalo lilikwenda sawai. Hapo sasa ndipo Zabroni alipotikisa mkono,mara ghafla akahisi kumuona mtu aliyevaa nguo nyeupe akimsogelea mahala pale alipoangukia baada kupokea kichapo kikali kutoka kwa Bluyner. Mtu huyo aliyevaa nguo nyeupe alikuwa akimfuata Zabroni huku akisema "Amka Zabroni, wewe ni mwanaume hupaswi kushindwa kizembe. Aaamka Zabroni amka babaaa ",sauti hiyo baada kulindima ipasavyo kichwani mwa Zabrini, hatimaye alijihisi kupata nguvu. Alifumbua macho yake kisha akasimama,ilihari upande mwingine kijana Steve alikuwa akichezea kichapo huku baadhi ya wafungwa wakiingilia kati kumtetea ambapo baada kuonekana bado Bluyner anakuwa mgumu kumuachia,Askari nao waliingilia kati lakini Bluyner alizidi kumganda Steve akigoma kumuachia. Hivyo hapo pakawa hapatoshi,vurumai la kutisha lilizuka sehemu hiyo ila lilikuja kutulia baada kusikika sauti ya Zabroni ikisema "Mimi ni Zabroni! ",wafungwa wote akiwemo na Bluyner waligeuka kutazama kule ilipotokea sauti hiyo. Walimuona Zabroni akiwa amesimama kidete huku mkono wake wa kulia wenye hirizi akiwa amekunja ngumi moja nzito ikiwa uso wake nao ukisweta jasho mchanganyiko na damu. Wafungwa baadhi walio mkubali Zabroni walishangilia baada kuona kidume kanyanyuka. Bluyner alizungusha shingo kuilaza kulia na kushoto,mishipa ililia mfano wa kijiti kilicho vunjika kisha akamsogelea Zabroni huku akiwa ametunisha mbavu zake.
"Naam! Hicho ndicho nilichokua nataka", alisema yule Askari aliyempatia Zabroni hirizi. Wakati huo sasa tayari wanaume hao walikuwa wameanza kupigana. Bluyner alijitahidi kurusha ngumi na mateke kwa kasi ya ajabu ila mtukutu Zabroni aliweza kuyakwepa yote,hata moja halikumpata. Bluyner alishangaa sana,alishusha pumzi kwa kasi kisha akaanza upya lakini bado mambo yalikwenda mlama. Hivyo akajikuta anachoka bila kupenyeza ngumi wala teke kwenye mwili wa Zabri. Zabroni baada kuona tayari Bluyner kawa mchovu,kalainika kama mrenda.
"Umechoka, sasa ngoja nikuadabishe mwana hidhaya mkubwa wewe", aliongea kwa hasira Zabroni na ndipo alipoanza kurudisha mapigo,hakutaka kuutumia mkono uliokuwa na hirizi. Alitumi mkono mwingine ila pindi Bluyner alipojaribu kujihami kuzuia ngumi zake, ndipo aliutumia huo mkono ambao ulionyesha kuwa na nguvu nyingi kwani ilimpelekea kumtegua mkono Bluyner. Mayowe ya maumivu aliyapasa Bluyner huku akiwa ameushika mkono wake ulioteguka,papo hapo riasi mbili tatu zilipigwa angani. Amri ikatolewa wafungwa wote wapande magari warudi Gerezani,kupitia nafasi hiyo Zabroni alitoweka akipitia kwenye msitu mdogo uliokuwepo jirani na maeneo hayo. Askari walipomuona akikimbia walimpiga risasi kama njugu lakini bahati mbaya hazikufanikiwa kumkuta,na hivyo Zabroni akawa ametoroka jela kupitia mazingira hayo ya kutatanisha yakisababishwa na hao Askari waliopewa jukumu la kuwalinda na kuwasimamia kwani uzembe walioufanya ni kuruhusu wafungwa wapigane.
Siku zote wahenga wanasema kwamba ng'ombe wa masikini hazai, akizaa basi huzaa dume. Ndivyo msemo huo ulipojizihirisha kwa Afande Veronica, kwani wakati Zabroni anatoroka jela,kwingineko Veronica nae alikuwa akimalizia hatua ya mwisho ya uhamisho wakuhamia kikazi ndani ya jiji la Dar es salaam asijue kwamba tayari yule mtu aliyemtia hatiani kwa kumdanganya na penzi la uongo hayupo tena jela,yupo huru ingawa haijafahamika wapi ataibukia lakini pia haijulikana style gani atakayo kuja mtaani.
Upande mwingine,taarifa ya kutoroka kwa mfungwa Zabroni, hatimaye ilimfikia mkuu wa gereza. Mkuu huyo alichanganyikiwa baada kupata hiyo taarifa,aliwaita wasaidizi wake kisha akawatangazia dau nono kwa yoyote atakae mkamata ama kufahamu mahali alipo huyo mtu mtukutuku Zabroni. Na moja ya Askari waliopewa dili hilo alikuwemo Afande Jimmy,ilihari huku mtaani nako Zabroni aliamuwa kujikita katika kazi ya kuzoa takataka akiwa na dhumuni la kutafuta nauli ili arudi kijijini kwao akalipe kisasi kwa Veronica pia na Bruno kisha akafungwe kihalari.
Zabroni ilibidi ajichakaze sehemu mbali mbali za mwili wake wakati huku akiwa katika mavazi yaliyoraruka raruka kila sehemu kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua,baada kuwa katika hali hiyo alianza kazi yake ya kuzoa takataka,moyoni akiamini kwamba iwe isiwe lazima atakuwa anatafutwa. Kwahiyo kazi hiyo aliamini pia itamfanya awe katika mazingira salama pasipo kusumbuliwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku moja Zabroni akiwa amechoka mchana jua kali maeneo ya Kinondoni, kando ya barabara alijalaza huku akitazama magari jinsi yanavyopisha kwa kasi na kusimama kusubiri taa ya kijani iwake. Mara ghafla mbele yake ikasimama gari ndogo aina ya RAV4,gari hiyo iliegesha pembeni kisha akatelemka Binti mrembo sana. Binti huyo alizipiga hatua mpaka mahali alipo simama mwanamke mmoja hivi wa makamo ambapo wawili hao walisalimiana huku wa kicheka, walionekana ni watu ambao hawajaonama muda mrefu sana. Walifurahi sana wakati huo huo Zabroni pale alipokuwa kajilaza alinyanyuka baada kuona kama binti huyo amemfananisha. Hivyo alistuka sana aliamua kusimama ili ajilizishe kama yule anayemfahamu au la!
___________

Zabroni alizidi kumsogelea yule binti ambaye kwa upande wake alikuwa amemfananisha lakini kabla hajamkaribia, binti yule aliambaa kuzipiga hatua kurudi kwenye gari lake. Hivyo Zabroni akawa hajamfahamu vizuri ila alistuka kusikia yule mama aliyekuwa akisalimia na yule binti akisema "Naona mambo sio mabaya Veronica,umerudi mjini sasa utazidi kunenepa", alisema hivyo mama huyo huku akicheka, yule binti aliyetajwa kwa jina Veronica aliposikia maneno hayo aligeuka ili amjibu. Alipo geuka alijibu akianza kwa kicheko "Ndio maana yake mama Lina", kumbe wakati Veronica anamjibu mama huyo mama ambaye alimfahamu kwa kujina la binti yake atwae Lina,Zabroni akapata kumuona usoni baada hapo awali kumpa mgongo. "Alaah! Kumbe upo huku kwa sasa! Sawa sawa popote ulipo nitakupinda tu",alijisema Zabroni baada kugundua kuwa yule binti aliyekuwa akimfananisha ndio mwenyewe Veronica. Tayari ile ahadi aliyoahidiwa Veronica pindi atakapo mkamata Zabroni ilitimia uhamisho wa ulikuwa umeshakamilrika,na siku hiyo alikuwa yupo katika matembezi yake kabla hajaanza kazi. Kupitia dili lile la kumkamatisha mtukutu Zabroni alipata pesa nyingi mno, alinunua gari lake pia alinunua nyumba maeneo ya Masaki jijini Dar es salaam. Maisha ya kamanda Veronica yakawa mazuri sana kwani akaunti yake benki nayo ilisheheni pesa ya kutosha,alikula na kuvaa atakavyo mwenyewe.
Veronica alipanda kwenye gari kisha akaondoka zake,huku nyuma Zabroni akibaki kumsindikiza kwa macho na mwishowe akatikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani ilihari tabasamu bashasha nalo likitawala kinywani mwake mithiri ya Simba aliyemuona Swala. Kitendo hicho cha Zabroni kumkodolea macho Veronica mpaka anaondoka mahali hapo kilimshangaza mama Lina,mama yule aliyekuwa akiongea na Veronica. Kwa mashaka akAmuuliza Zabroni "Kulikoni mbona unamtazama sana yule dada,unamfahamu?..",Zabroni aliposikia sauti hiyi,aligeuka akaacha kutazama kule barabarani akamtazama mama Lina aliyemsemesha. Alicheka kidogo kisha akajibu huku aking'am ng'am usoni mwake "Ndio namfahamu,yule si Veronica? .."
"Ndio yeye,kwa sasa ni polisi. Amehamishwa sijui kutoka sehemu gani huko ila kwa sasa yupo hapahapa mjini" ,aliongeza mama Lina. Zabroni aliposikia maneno hayo aliachia tabasamu bashasha kisha akajibu "Alaah! Jambo nzuri sana,unajua yule binti nimesoma naye kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Lakini mwenzangu akaendelea,mimi nikaishia njiani yote ikiwa changamoto ya maisha. Na sasa nazoa takataka." ,akacheka kidogo akakaa kimya.
"Ni kweli,ila siku zote soma upate kuelimika na sio kupata kazi. Kupata kazi ni tokeo sio tegemezi,wapo watu wamesoma sana lakini hawajapata kazi. Tusiende mbali, mimi nina mwanangu anaitwa Lina. Mwanangu kasoma mpaka chuo kikuu kamaliza lakini hana kazi"
"Umeona sasa? Ndio maana mimi nimeamua kujiajiri ila asikate tamaa. Acha nipambane na kazi yangu ya kuzoa takataka." kwisha kusema hayo Zabroni akaangua kicheko kwa mara nyingine tena kisha akaondoka zake.
Upande wa pili ndani ya Sophie Hotel alionekana Karani akiwa ameketi meza moja na Mr Rasi ama waweza kumuita Bruno,walikuwa wameketi huku mbele yao pakiwa na meza iliyosheheni vinywaji vya aina mbali mbali. Karani alikunywa bunda moja ya bia,akahoa kidogo kisha akasema "Kijana,kwanza nashukuru sana kwa kutii ombi langu la kukubali kuketi mahali hapa mimi na wewe"
"Aah asante sana mzee, heshima yako",alijibu Mr Rasi. Karani akaendelea kusema. "Nadhani bado hujafahamu fika nia na madhumuni ya kukuita mahali hapa,lakini ukweli ni kwamba nimevutiwa na uwezo wako wa kupigana. Hivyo basi kama hutojali naomba uwe moja ya wapiganaji wangu ili upige pesa,na kila pambano ukishinda utapata kiasi cha pesa milioni mia mbili", Karan alisema kisha akanywa maji yaliyokuwa kwenye grasi kuchamba koo. Mr Rasi kijana Bruno anayesakwa na serikali kila mahali kama shilingi,aliona katu hilo dili hawezi kuliacha kizembe. Upesi alikubali. "Sawa nipo tayari ila kabla sijasaini nataka kujua vipi serikali inaifahamu namna gani hii biashara", aliongea Mr Rasi. Karan akaangua kicheko cha madaha kisha akajibu "Kijana shaka ondoa kabisa, hii biashara inapesa ndefu sana. Kwa maana hiyo basi tunashirikiana vema na baadhi ya viongozi wa nyanda za juu, hawa nao ni warafi wa fedha tu. Chama chetu kila mwisho wa mwaka tunakutana na kuchangishana kisha fedha tunawapa hawa warafi ambapo nao kimya kimya wanatufanya tunazidi kuvuna pesa mjini ", Karan akamaliza kwa kicheko.
" Kwahiyo hofu ondoa kabisa ", akaongeza kusema Karan.
" Sawa hakuna shida, leta mkataba nisaini ", aliongea Mr Rasi. Haraka sana ililetwa kalamu na makaratasi yaliyojiorodhesha kanuni na taratibu ya mkataba husika,Mr Rasi akamwaga wino wakati huo akiwa hajui kama adui yake kwa sasa yupo huru.
Baada hilo zoezi kukamilika Mr Rasi aliambiwa aondoke nyumbani akajiandae kwa niaba ya kuhamia kwenye makazi mapya huku akiahidiwa kununuliwa gari pindi atakapo shinda mpambano wa kwanza waliomuandalia. Nje ya hiyo Hotel alionekana Tina akiwa amemngojea Mr Rasi,Tina na Mr Rasi tayari walikuwa katika mahusiano baridi kwani tangu siku ile Mr Rasi amsaidie kumpokonya yule kibaka aliyemuibia mkoba,Tina akawa ametokea kumpenda. Na hata siku ya pili Tina alipomuona Mr Rasi akipigana na wale vijana saba moyo wake ukatotokea kumpenda zaidi. Si yeye tu bali hata shangazi yake naye alimkubali Mr Rasi kwani siku hiyo naye alikuwepo,hivyo kupitia hayo matukio mawili tofauti Tina na shangazi yake wakaweka ukaribu zaidi huku shangazi mtu akimshawishi Tina kuweka ukaribu zaidi na kijana huyo ambaye alionekana shupavu na mkakamavu. Si mwingine ni Bruno ama Mr Rasi.
Kipindi wawili hao Mr Rasi na Tina walipokuwa wameweka ukaribu wao, yeye Mr Rasi hakuwa na sehemu maalumu ya kulala. Shida hiyo Tina aliifikisha kwa shangazi yake,shangazi yake alisikitika sana akamtaka Mr Rasi aishi nyumbani kwake. Mr Rasi hakulipinga hilo suala ingawa umakini bado aliuzatiti ili asigundulike. Hivyo siku hiyo baada kutia saini ilikuwa siku ya furaha sana kwake ingawa ilikuwa siku ya huzuni kwa watoto wa shangazi yake Tina pia akuwemo na shangazi mtu lakini vile vile kwa Tina kwa maana ilimbidi Mr Rasi ahame hapo nyumbani akaishi kwenye nyumba mpya aliyopewa. Walimzoea.
Siku zilisogea,ila bado uhusiano kati ya Bruno na Tina ukizidi kudumu. Kiasi kwamba Tina alimsahau kabisa Zabroni, hasa akikumbuka mambo aliyokuwa akiyafanya,moyo wala macho yake hayatamani abadani kumuona. Akaona kujiweka kwa Bruno Mr Rasi, ndio sehemu salama pakuweza kutuliza moyo wake asijue kwamba Mr Rasi na Zabroni ni maadui kama maji na moto.
Hatimaye siku ya pambano la Mr Rasi iliwadia, matajiri walishindana kutaja dau huku kando kando watazamaji wakishangilia. Siku zote Karan aliaminika kutokuwa na wapambanaji wazuri kwahiyo kupita imani hiyo,yule tajari mwenzake alikuwa akitaja dau nono akijua kabisa Karani hana watu wa kupigana na watu wake.
"Milion arobaini na tano" alitaja dau Karani,mwenzake akajibu
"Milioni stini na tano"
"Milion sabini na tano"
Million themanini"
"Milioni tisini"
"Milioni tisini na tano"
"Million miamoja"
"Mr acha vijana wathibitishe kile tulicho kinadi hapa kwenye kadamnasi ya watu",alifunga mjadala Karani kisha akakuja namba nne kwenye kiti alichokalia huku akiiweka sawa miwani aliyovaa. Mpinzani wa Mr Rasi ndio alikuwa wa kwanza kuingia ulingoni,shangwe zililipuka za kumshangilia huyo jamaa aliyeonekana kuwa na mwili wa mazoezi. Kwa madaha jamaa huyo alizungusha shingo yake aliipeleka kulia na kushoto kitendo kilicho pelekea watu kuzidi kupiga mayowe ilihari upande wa pili alionekana Mr Rasi naye akiingia ulingoni. Mr Rasi alitambua fika kuwa anafatiliwa sana,kwahiyo ili asiumbuke mahali hapo alizilaza rasta zake mbele na nyuma pia pembeni. Kufanya hivyo ni vigumu sana kumtambua. Kama ilivyo ada,nderemo na vifijo vilisikika wakimshangilia Mr Rasi. Mpambanaji mpya kabisa mbele ya watazamaji. Yule tajiri aliyekuwa akitaja dau nono mara mbili ya Karani,alistuka kumuona Rasi. Akavua miwani yake ili apate kumuona, alitaharuki ikiwa wakati huo huo alionekana Zabroni akajongea sehemu hiyo kutazama pambano huku akiwa katika mavazi yake ya kuzolea takataka. Naye pia alijiweka katika hiyo hali ili kukwepa mkono wa dola,kwani tangu atoroke jela uliundwa mkakati wa kumsaka mahala popote pale alipo. Hivyo kujiweka namna hiyo kulimfanya asigundulike,angeliweza kujiweka kivyovyote vile lakini aliamua kuwa mzoa takataka ili apate nauli ya kurudi kijijini akalipe kisasi kwa Afande Veronica pamoja na Bruno ambaye ni Mr Rasi. Lakini baadaye akaja kugundua kuwa tayari Veronica yupo ndani ya jiji,ila hakuweza kuacha kusaka pesa kwa niaba ya nauli kupitia hiyo kazi kwa sababu alijua kuwa huko kijijini bado kuna adui yake mmoja ambaye ni Mr Rasi na hata asijue kwamba hata Mr Rasi naye yupo jijini kama ilivyo Veronica, zaidi mahali hapo alipokuwa akijongea ndipo yupo huyo Bruno ama Mr Rasi.


Wakati kijana Zabroni anasogea eneo hilo kutazama ndondi za Mr Rasi,upande wa pili nako eneo hilo hilo ilikuja gari ndogo aina ya Hilux. Gari hiyo ilipaki kando kidogo ya uma wa watu waliokuwa wakishuhudia mpambano,kisha akatoka ndani binti mrembo ambaye si mwingine ni Tina. Tina alikuja mahali hapo kutazama jinsi mpenzi wake anavyopigana,watu baadhi walipomuona Tina walimkodolea macho. Kwani Tina alikuwa amependeza sana sana siku hiyo,kiasi kwamba aliweza kumvutia kila mtu. Kipindi Tina anafika hapo Mr Rasi alikuwa anachezea ngumi za kila sehemu ya mwili wake kana kwamba jamaa aliyekuwa akipigana nae alionekana kumzidi ubavu,lakini baada Mr Rasi kusikia sauti ya Tina ikisema "Rasi,sijapenda mimi" ,Hapo mr Rasi alijihisi kupata nguvu mara mbili ya awali. Alipigana ipasavyo mpaka akaibuka mshindi,ikawa furaha isiyo kifani kwa Karani lakini pia kwa mrembo Tina baada kuona yeye kuwa moja ya chachu ya ushindi.
Makubaliano sehemu ya kukutana yalifanyika baina ya matajiri hao,Karani na na mwenzake. Ilihari kwingineko upande ule aliosimama Zabroni alijikuta akivuta kumbukumbu siku za nyuma kipindi alipokuwa akipigana na Bruno,aliona mapigo aliyoyaona hapo ulingoni kutoka kwa Mr Rasi na yale ya Bruno yalifanana fika. Jambo hilo kidogo lilimtatiza Zabroni,lakini yote kwa yote hakutaka kutilia maanani na hivyo aliamuwa kuondoka zake kwani tayari mpambano ulikuwa umeshamalizika. Zabroni alizipiga hatua kutoka mahali hapo akazunguka upande ule ziliposimama gari za matajiri pia na gari aliyokuja nayo Tina,kabla hajazikaribia hizo gari alimuona binti aliyefanana na Tina akifunguliwa mlango na Mr Rasi. Zabroni alistuka,kwa sauti kuu akasema "Tinaaaaa",Tina aliposikia sauti hiyo aligeuka kutazama kule ilipotokea,hakujua mtu aliyemuita kwa maana watu walikuwa wengi sehemu hiyo. Zabroni baada kuona Tina hajamuona alinyoosha mikono,hapo Tina akawa amemuona. Haraka sana Zabroni alizipiga hatua kumsogelea. Alipo mfikia alimsalimia lakini Tina hakumjibu salamu yake,alishangaa sana Zabroni. Kwa taharuki akasema "Ni mimi mpenzi wako uliyeniacha kijijini", akacheka kidogo kisha akaendelea kusema "Tina inaama umenisahau? Au kwa sababu nimechafuka hivi ndio maana umeshindwa kunitambua? Amini Tina kwa sasa nipo mjini,niliamua kuachana na yale mambo niliyokuwa nikiyafanya. Ndio maana sikuhizi nimejikita kwenye kazi hii niliamua kukimbia kijijini baada kuona naogopwa sana",alisema Zabroni huku akiwa na tabasamu bashasha,wakati huo Tina alikuwa kimya akimsikiliza huku machozi yakimtoka. Aliyafuta kisha akamjibu "Sawa,yote tisa. Kumi. Mimi sio mpenzi wako tena. Nimepata mwingine anayejua nini maana ya mapenzi,na sio wewe mwanaume katili usiyekuwa na hata chembe ya huruma. Wako wapi wazazi wangu? Wewe ndio muhusika wa vifo vyao. Je, unadhani kwa jereha hili unaweza kuniponya? Hebu achana na mimi bwana." aliongea Tina huku machozi yakimtoka. Muda huo huo Mr Rasi alitoka ndani ya gari akazunguka ule upande aliosimama Tina akiwa anaongea na Zabroni. Alipofika alitaharuki kisha akamuuliza Tina "Tina,kulikoni kwani kuna nini?..",Tina hakujibu aliishia kumtazama Zabroni kwa hasira kali. Ukweli ni kwamba hata Mr Rasi hakuweza kumtambua Zabroni kwani wakati Rasi anamuuliza Tina swali hilo,Zabroni yeye aliinamisha uso wake. Ni kitendo ambacho kilimuwe ngumu Mr Rasi kumjua yule mtu anayezungumza na Tina.
"Hapana mpenzi hakuna kitu ila..",kabla Tina hajamalizia jibu lake, mara ghafla Mr Rasi alimkatisha kwa kusema "Ila nini? Unajua tunasubiliwa sisi? Wenzangu wote wapo tayari,sasa naona wewe umesimama nje muda mrefu tu hata unachokifanya hekieleweki", alifoka Mr Rasi kwa hasira. Tina alijua kuwa mpenzi wake kakasirika,hivyo alimsogelea kisha akamkumbatia mbele ya Zabroni halafu akasema "Tazama we mwenda wazimu, Tina sio mali yako tena. Huyu ndio mpenzi wangu kwa sasa,kwahiyo itapendeza kama utaniita shemeji popote pale utakapo niona. Lakini tofauti na hivyo utahatarisha maisha yako mwanahidhaya mkubwa wewe ", aliongeza kusema hivyo Tina kisha akaingia ndani ya gari,gari likawashwa wakaondoka zao huku nyuma wakimuacha Zabroni asiamini kile kilicho tokea. Moyoni akawa anajiuliza "Hivi ni kweli au ni fikra zangu tu?.." wakati Zabroni akiwa katika hali hiyo ya kutoamini kile alichokiona,upande mwingine nako ndani ya gari Mr Rasi akiwa na Tina walikuwa wakipiga zogo huku Tina akimsifu mpenzi wake kwa kuibuka kidedea. Lakini baada ya sifa hizo,Mr Rasi alimuuliza Tina juu ya mtu yule aliyekuwa akiongea naye "Tina kwani yule nani uliyekuwa ukiongea naye?" ,Tina mara baada kuulizwa swali hilo alikaa kimya ila baadaye kidogo alijibu "Nadhani unakumbuka sikuile nilipokwambia kuhusu matendo machafu aliyokuwa akiyafanya mpenzi wangu wa kwanza"
"Nani yule aliyekuwa anachoma nyumba hovyo? ..",alirudia kuhoji Mr Rasi huku akionekana kustuka. Tina akajibu "Huyo huyo,anaitwa Zabroni. Ndio nilikuwa naongea naye,hivyo ilikudhihilisha kwamba simtaki tena nikaamua kukutambulisha kwake kwamba wewe ndio mpenzi wangu. Ukweli Rasi,namchukia sana yule mwanaume kwani nafahamu yeye ndiye aliyewaua wazazi wangu. Sitaki na sitotaka kumuona tena mbele yangu" Tina alilia, wakati huo huo Mr Rasi alikanyaga breki kwa nguvu kiasi kwamba matairi ya gari yalitoa harufu. Papo hapo aligeuza gari kurudi kule alipotoka huku moyoni akijisemea "Huyu ndio niliyekuwa namsaka kwa muda mrefu,ngoja nikamalizane naye mapema kabla hajatoweka ndani ya hili jiji",alijisemea hivyo Mr Rasi ilihari muda huo Tina alikuwa ameshanyamanza amebaki sasa kushangaa namna Mr Rasi anavyo endesha gari kwa fujo kumfuata Zabroni. Kwani naye alitoka rumande ili amuue Zabroni kama njia ya kulipiza kisasi,ilihali Zabroni naye vile vile alitoroka jela ili amuue Mr Rasi ikiwa kama njia ya kulipiza kisasi.
Kabla Mr Rasi hajafika ile sehemu waliyomuacha Zabroni, Zabroni machale yalimcheza akaamua kuondoka mahali hapo haraka sana akiamini kwamba tayari Tina ndio mtu pekee mwenye uwezo wa kuvujisha siri ambayo ingeliweza kumtia hatiani akashindwa kulipa kisasi. Hivyo wakati Mr Rasi anafika na gari yake hakumkuta Zabroni, aliumia sana kwa maana alijua hiyo ndiyo nafasi ya kumuangamiza adui yake.
Zabroni sasa alianza kuhofia usalama wake,na hapo aliamua kutoka nje ya jiji la Dar es salam. Akaenda pembezoni mwa jiji ambapo huko alianzisha makazi yake mapya, aliachana na ile style ya kuwa mzoa takataka. Huko kando ya jiji alikaa takribani miaka mitatu kiasi kwamba hata wale Askari waliopewa majukumu ya kumsaka mfungwa huyo walianza kukata tamaa. Lakini mara baada kupita miaka hiyo mitatu,hatimaye alirudi tena mjini. Alijikita katika kazi ya kuosha magari huku umakini ukitawala ipasavyo katika mwili wake. Safari hiyo alibadilisha jina akajiita Ramso.
Siku moja hapo car wash ilikuja gari ndogo aina ya Noah,ndani ya gari hiyo alishuka binti mrembo. Binti huyo aliitwa Lina. Lina aliposhuka kwenye gari alichomoa simu kwenye mkoba wake,akawa amedondisha fedha shilling elfu tharathini zikiwa zimekunjwa. Bila kujua kama kadondosha fedha hizo alimsogelea Zabroni,kwani yeye tu aliyeonekana hana kazi muda huo. Alimsalimia kisha akamwambia amuoshee gari yake,Zabroni ambaye ni Ramso alimtajia bei. Lina hakuteteleka zaidi kusema "Haina tabu,basi naomba unioshee haraka nakuja mara moja. Nikitoka huku nikute umemaliza sawa kaka?..",alisema Lina msichana mrembo kuliko hata jina lenyewe. "Sawa ",alijibu Zabroni kisha mara moja akaanza kazi huku Lina naye akiambaa ng 'ambo ya barabara ambapo mbele kidogo palikuwa na jengo la supermarket. "Watu na maisha yao",alisema Zabroni wakati huo ameshaanza kuiosha gari la huyo mwanadada atwae Lina. Alipokaribia kumaliza, mara ghafla akaziona zile fedha alizodondosha Lina. Hima aliziokota akazitia mfukoni kisha akaendelea kuosha gari hadi akamaliza ambapo alikaa pembeni kusubiri ujira wake. Baada ya nusu saa Lina alirejea huku macho yake yakionekana kutazama chini wakati wote kana kwamba kuna kitu anakitafuta,alipomkaribia Zabroni alimlipa ujira wake kisha akapanda Kwenye gari. Kabla hajaondoka, Zabroni alimfuata kisha akatoa mfukoni zile fedha akamkabidhi "Dada hizi pesa zako? ..",Lina baada kuziona alishusha pumzi kwa kask kisha akajibu "Ndio..Doh! Nimezitafuta sana...kiukweli ni watu wachache sana wenye moyo kama wako. Kaka hebu nambie unaitwa nani?.."
Naitwa Rasmo",alijibu Zabroni huku Lina akimtazama usoni bila kupepesa macho.
Alimshukuru sana,alichukuwa shilling elfu kumi tu zilizobaki akamwachia mtukutuku Zabroni. Na tangu siku hiyo mazoea yakaanza baina ya Zabroni na Lina. Mazoea hayo mwishowe yakazaa mahusiano,ambapo baada mahusiano kukolea,Lina alimtaka ampeleke mpenzi wake akamtambulishe kwa wazazi wake. Wakati huo baba yake Lina ni Afande Jimmy, moja ya maafande aliyepewa jukumu la kumtafuta Zabroni ambaye tayari ni mpenzi wa mwanaye.
Mpaka nyumbani kwao na Lina Zabroni alifika,alimkuta mama yake sebuleni huku baba Lina akiwa chumbani. "Mama nafikiri niliwahi kuwaambia kwamba nimepata mchumba",alisema Lina kwa sauti ya kusitasita. "Ndio mwanangu nakumbuka,na bahati nzuri leo baba yako hajaenda kazini. Yupo ndani kapumzika,basi ngoja nimuite",alijibu mama Lina kisha akasimama akazipiga hatua kuingia chumbani huku sura ya huyo mtu aliyekuja na mwanaye ikimjia kwa mbaali kichwani mwake.
Punde si punde baba yake Lina Afande Jimmy alitii wito,alipokaa kwenye sofa tu macho yake yakagongana na uso wa Zabroni ghafla alishtuka, akakumbuka kuwa huyo ni mfungwa anayesakwa kwa udi na uvumba. Vile vile dau nono litatolewa kwa kamanda ambaye atafanikisha kumtia mbaloni.


Alistuka Afande Jimmy, ilihari muda huo Zabroni naye akionekana kutaharuki baada kugundua kuwa tayari yupo mkononi mwa Askari magereza aliyekuwa akimlinda jela. Pumzi kwa nguvu alishusha,huku akifikiria ni vipi atang'atuka hapo kibindoni. Wakati huo Jimmy alinyanyuka kutoka kwenye sofa akarudi chumbani upesi kisha akamuita mkewe "Mama Lina hebu njoo mara moja ",bila kuchelewa mama Lina alinyanyuka akamfuata chumbani mumewe huku subuleni presha ikizidi kumpanda Zabroni kiasi kwamba mpaka Lina alitambua kwamba Zabroni hayupo sawa huo muda ingawa hakutaka kumwambia.
Chumbani kule, Jimmy alimwabia mkewe ukweli kuhusu kijana Zabroni kitendo ambacho kilimfanya mama Lina naye kuvuta kumbukumbu,alikumbuka siku kadhaa zilizo pita "Kwa kumbukumbu zangu kiukweli huyu mwanaume sio mgeni machoni mwangu. Namkumbuka vizuri sana ila siku hiyo nilipomuona alionekana anafanya kazi ya kuzoa takataka. Lakini pia kwenye maongezi niliyokuwa naongea naye alinambia kwamba alisoma na Veronica, yule Vero mtoto wa mzee Busere ambaye kwa sasa ni Askari. Kwahiyo unapo niambia kwamba huyu katoroka jela,dah. Unanichanganya kidogo kiukweli ",alisema mama Lina. Jimmy alitazama paa la nyumba akionekana kutafakari kitu fulani akilini mwake,akashusha uso wake chini wakati huo akishusha pumzi ndefu. Baada ya hapo alisema "Unajua kwamba endapo kama nitamkamata huyu mtuhumiwa tutaogolea mapesa? Lakini pia hataakama ni mkwe wetu,huyu Lina bado anatakiwa aendelee na masomo sasa iweje atuletee masuala ya uchumba? ..hapana siwezi kukosa pesa,vile vile siwezi kuepuka kupandishwa cheo wakati mtuhumiwa tayari yupo mikononi mwangu..", aling'aka kamanda Jimmy kisha haraka sana alisogelea droo ndogo ya kitanda, akatoa pingu na bastora. Hima alirudi sebuleni ambapo alimkuta Zabroni na Lina wakiongea mambo kadhaa wa kadha huku Lina akionekana kumtoa wasi wasi Zabroni. "Kijana hapo hapo ulipo hebu simama juu na unyooshe mikono yako..", kamanda Jimmy alitoa amri hiyo huku akimnyooshea bastora Zabroni. Lina alistuka akajikuta haelewi kinachoendelea,kwani yeye hakufahamu kwamba mpenzi wake ni mfungwa aliyetoroka gerezani. "Baba nini sasa unataka kufanya? Kwanini unamtisha kijana wa wawatu? Ama mimi sistahiri kuwa na mwanaume?..",alihoji Lina huku akilia,lakini kilio chake katu hakikuweza kumfanya mzee wake ashindwe kutimiza agizo lake alilotumwa. Alimvisha pingu mkononi Zabroni, moyoni akiwa amedhamilia kumrudisha Zabroni jela. Hapo sasa Lina alimsogelea baba yake kisha akamshika mkono ili asifanye uamuzi huo, kitendo hicho kilimkera sana Afande Jimmy ambapo alimpiga kofi binti yake na kisha kumtupia maneno makali. Lina akaangukia kwenye sofa ilihari muda huo huo Jimmy alimuongoza Zabroni mbele yeye nyuma tayari kwa niaba ya kumpeleka moja kwa moja sehemu husika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini kabla hajampandisha kwenye gari lake,ghafla alisikia sauti ya ya Lina ikimuita. Afande Jimmy aligeuka akajikuta akistuka baada kumuona Lina akiwa ameshika kisu kwa dhumuni la kutaka kujiuwa. Machozi yakimtiririka akasema kwa uchungu "Baba,endapo utaitosa furaha yangu. Basi na mimi najiuwa hapa hapa mbele yako. " Kwisha kusema hayo alianza kujihesabia namba. Wakati huo mama Lina naye upande wa pili alikuwa akilia huku akimsihi mumewe asimrudishe Zabroni Jela, amuache huru kwani kufanya hivyo itapelekea kumkosa mtoto wao pekee, ambaye ni kama mboni yao.
Hapo Jimmy hakuwa na namna tena,alichomoa funguo ya pingu. Akamfungua Zabroni ingawa moyoni akionekana kufura hasira. "Huu ni upuuzi kabisa,kweli bora uzae chura kuliko mtoto wa kike mpumbavu kama huyu alaah ",alisema Afande Jimmy huku akizipiga hatua kurudi ndani ilihari muda huo Lina alidondosha kisu chini kisha akamsogelea Zabroni na kumkumbatia.
Basi mapenzi ya watu hao wawili yaliendelea kushamili,kiasi kwamba ilimpelekea Zabroni kumsahau kabisa Tina. Siri kuu aliitunza Afande Jimmy kwani tayari mtuhumiwa yupo kwenye mji wake. Lakini mwishowe aliona kuishi na Zabroni nyumbani kwake ni jambo la hatari sana kwa kibarua chake kwa maana tayari Zabroni ni mtu anayetafutwa na serikali mahali popote pale,hivyo endapo kama atabainika kuwa yupo nyumbani kwake basi huwenda Jimmy akatuhimiwa kumtorosha mfungwa huyo kitendo ambacho kitaweza kumfukuzisha kazi lakini pia hata kuhukumiwa kwa kosa hilo la jinai.
Hivyo Jimmy alimtafutia Zabroni nyumba nyingine mbali na eneo hilo analo ishi yeye. Huko alimpangishia chumba pia alimkabidhi gari ya kutembelea huku akimsisitiza umakini wa kuishi maisha hayo ya wasiwasi kuhofia kurudishwa jela.
Hakika lilikuwa ni jambo la furaha sana kwa Lina baada kuona baba yake ameendana na matakwa yake,hicho ndicho alichukuwa anakitamani kije kutokea. Kweli hatimaye siku hiyo kikaja tokea asijue ya kwamba kijana huyo licha ya kuwa naye kwenye mahusiano lakini pia anamkakati mzito sana wa kulipa kisasi. Hivyo kukabidhiwa kwake usafiri binafsi kulimfanya aanze kutembembea maeneo mbali mbali ndani ya jiji huku akitamani walau siku moja akumbane na Veronica,ila bahati mbaya haikuweza kutokea siku hiyo. Upande wa pili,Mr Rasi alijikuta akikosa amani wakati wote baada kugundua kuwa adui yake yupo naye ndani ya jiji. Aliwaza ni wapi atambamba ili amalizane naye kibingwa? Ikiwa wakati huo Zabroni naye akiwaza ni wapi atakumbana na Veronica amalizane naye asitambue ya kwamba Mr Rasi ama Bruno naye yupo jijini anamtamani kama mlevi aonapo pombe.
Siku zilisonga, miezi ikasogea. Mr Rasi akiendeleza kichapo kwenye mapigano yake huku Lina naye akiendelea kumtunza mpenzi wake hasa kujitahidi kutunza siri baada kujua kuwa mpenzi wake ni mfungwa aliyetoroka jela. Siku moja jioni sana,ilionekana gari aina ya Rav4 ikiingia nyumbani kwa kina Lina. Gari hiyo baada kupaki eneo maalumu alishuka msichana mrembo,msichana huyo hakuwa mwingine bali ni Veronica. Naam. Veronica na Lina ni marafiki wa kufa na kupona tangu walipokuwa shule ya msingi mpaka chuo. Siku hiyo Veronica alikuja nyumbani kwa kina Lina kwa niaba ya kumsabahi rafiki yake baada kupita miaka kadhaa bila kuonana.
"Karibu sana,Veronica ",Mama Lina alimkaribisha Veronica kwa bashasha ya hali ya juuu.
"Ahsante sana mama nimekaribia" alijibu Veronica huku akiketi kwenye Sofa. Salamu zilifatia kisha mama Lina akamtania kidogo Veronica kwa kusema "Naona tangu siku ile tukutane barabarani Magomeni,hatujaonana tena..khaa Veronica kama vile nyumbani kwangu hupajui? " alisema huku akitabasamu. Veronica akajibu "Ni kweli mama lakini nafikiri yote ni shauli ya kazi,istoshe nimehamia makazi mapya siku za hivi karibuni kwahiyo iliniwe vigumu kuanza kuzurula. Ila hakijaharibika kitu ndio nimekuja sasa...aammh kwanza Lina yuko wapi?.."
"Lina katoka tangu asubuhi,ngoja nimpigie aje haraka maana siku nyingi hamjaonana" ,Hima mama Lina alichukua simu yake akampgia binti yake. Lina akapokea ikasikika sauti ya mama yake ikisema "Lina ukowapi? Njoo nyumbani Vero kaja kukuona"
"Haaah! Vero? Mwambie nakuja anisubiri asiondoke",alijibu Lina kisha akaitupa simu kitandani akaendelea kuziweka sawa nywere zake kwani muda huo alikuwa ametoka kuoga baada kumaliza mchezo baina yake na mtukutuku Zabroni. Punde si punde Zabroni naye alionekana akitokea bafuni,lakini hakusikia kile Lina alichomjibu mama yake. Ila wakati anajifuta maji kwa taulo,Lina alimsogelea kisha akamwambia "Mpenzi wangu Ramso,Leo nimejikuta napata furaha zaidi. Rafiki yangu kipenzi kaja nyumbani kunitembelea kwahiyo naomba ujiandae twende wote ili nikakutambulishe kwake" ,alisema Lina kwa furaha asijue ya kwamba Zabroni ambaye yeye alimfahamu kwa jina Ramso anamtafuta kwa udi na uvumba Veronica ambaye ni huyo rafiki yake kipenzi aliyekuja kumtembelea siku hiyo.
"Usijali tutaenda, pamoja", Zabroni alijibu pasipo kujua ni nani huyo anayekwenda kumuona.

Wawili hao walijiandaa haraka haraka kisha wakaanza safari;wakati huo jioni ishatoweka,giza totoro tayari lilikuwa limeshatanda ndani ya jiji la Dar es aSalaam. Walipokuwa ndani ya gari,Zabroni na mpenzi wake wakuitwa Lina walikuwa wakiongea mambo mbali mbali hasa hasa kuhusu mahusiano yao.Lina alisema "Kiukweli Ramso sijatokea kumpenda mwanaume kama ninavyokupenda wewe,ndio maana baba alipotaka kukurudisha jela nikatishia kujiuwa "
"Ahsante sana kwa maneno yako matamu, je kwa mfano angenirudisha huko ungejiuwa kweli ama ulikuwa unamtisha tu?.."
"Kha Ramso,hakyaMungu ningejiuwa sitanii. Ujue mimi sipendi kukosa furaha katika maisha yangu. Lakini pia istoshe wazazi wangu wananipenda sana na ndio maana baba aliponiona nimeshika kisu haraka sana akakufungua pingu " alisema Lina huku akiwa amemgeukia Zabroni ambaye naye alionekana kuwa makini barabarani.
"Mmh naona mpenzi wangu tayari umekua dereva mzuri, lione kwanza ulivyokuwa unaogopa? Eti oooh nitaharibu gari,unadhani kujua kuendesha kwako gari na kuharibu bora nini? Bora uharibu mpenzi ilimradi tu ujue kuendesha..",aliongeza kusema Lina akizidi kujidhirisha ya kwamba kafa kuoza kwa mtukutu Zabroni. Zabroni alipoyasikia hayo maneno alifurahi sana moyoni akajikuta akijisemea mambo mengi kuhusu Lina. Wakati huo sasa walisimama baada taa nyekundu kuwaka, zogo mbali mbali ziliendelea wakingojea taa ya kijani nayo iwaruhusu. Punde simu ya Lina ikaita, mama yake alikuwa amempigia. Haraka sana alipokea kisha akasema "Hello mama tupo njiani tunakuja lakini tutachelewa kidogo kwa sababu kuna foreni mama yangu"
"Anhaa sawa basi mwenzio anataka kuondoka",alijibu mama yake Lina. Lina aling 'aka kisha akamtaka mama yake ampatie simu Veronica ili apate kuongea naye. Veronica alipokea akasema "Lina,mimi naondoka bwana nimekaa sana rafiki yangu. Naomba uniruhusu nitakuja kukuona siku nyingine sawa?.." Lina akajibu " Sijapenda best yangu unajua siku nyingi mimi na wewe hatujaonana,halafu istoshe nakuja na shemeji yako utaki umuone?..",hapo Veronica alicheka kidogo kisha akajibu "Nataka sana ila nimepigiwa simu kuwa nahitajika mara moja nyumbani,siku nikija kukuona tuatongea mpaka unichoke. Ammh leo naomba nimsalimie japo kidogo",alisema Veronica pasipo kutambua kwamba huyo mtu anayetaka kumsalimia ndio yule aliyemtia hatiani kwa kutumia kivuli cha mapenzi. Si mwingine ni Zabroni. Zarloni alichukua simu akaanza kwa salamu kisha akamuuliza jina lake"Naitwa Veronica ",alishtuka Zabroni kusikia jina hilo,jambo lingine lililomstua ni baada kusikia sauti inafanana fika na sauti ya Veronica yule aliyemkamatisha. Alipotaka kumdadisi zaidi ili apate japo ahakika kama ndio huyo Veronica anaye mtafuta,taa ya kijani ikawaka kuashiria gari zimeruhusiwa. Hivyo Zabroni alimrudishia simu Lina kisha akawasha gari safari ikaendelea wakati huo nyuma yake ilisikika gari ikipiga honi kumtaka Zabroni aendeshe gari kwa kasi ili kuokoa muda,lakin Zabroni hakufanya kama alivyotaka dereva huyo wa gari ya nyuma. Kitendo ambacho kilimfanya yule dereva kukasirika,alipopata nafasi alimzunguka akaendana naye sambamba huku akionekana kumtolea maneno machafu Zabroni. Zabroni alipomuona jamaa anafoka, haraka sana alitelemsha kioo chake cha pembeni ili apate kumjibu. Ni Mr Rasi. Alimkumbuka vema Zabroni wakati huo huo Mr akishindwa kumtambua Zabroni kwa sababu ya giza totoro ila Zabroni alimkumbuka Rasi kutokana na Rasta zake. Ndani ya gari, Lina kuna kitu alikidondosha chini ya miguu yake. Ikabidi awashe taa ili akichukue. Mwanga huo wa taa ulipomulika tu,upande wa gari ile ya Mr Rasi Tina alipiga chabo kutazama ni nani huyo anayejibizana na mpenzi wake,akamuona Zabroni. Akataharuki akalitaja jina la mtukutu "Zabroni... "
"Zabroni?..",alijiuliza Mr Rasi akishangazwa na jina hilo ambalo sio jipya maskioni mwake,wakati huo huo Zabron aliposikia sauti hiyo alihisi ni sauti ya Tina. Upesi aliingiza gea mbili mfuruluzo,gari ikaongeza kasi huku nyuma Mr Rasi naye alimuuliza Tina kuhusu Zabroni "Huyu ndio yule jamaa uliyekuwa ukimzungumzia?.."
"Ndio huyo,sijui anaendeshaje maisha yake. Haeleweki huyu mtu..",alijibu Veronica. Kijasho chembamba kikaanza kumpanda Mr Rasi huku moyoni akijisemea "Leo huyo mtu ama zake ama zangu,atanitambua",kwisha kusema hayo aliendesha gari yake kwa kasi ya ajabu huku akionekana kuwa makini kuzikwepa baadhi ya magari makubwa kwa madogo hasa hasa daladala ambazo kwa upande wake zilonekana kumkera kwani zilikuwa zikisimama hovyo hovyo. Lakini wakati Mr Rasi anamkimbiza Zabroni,mara ghafla simu yake ikaita. Bosi wake alikuwa amempigia alipokea haraka sana. Sauti ikasikika ikisema "Rasi ukowapi mbona unachelewa wakati saa nne mpambano unaanza? Muda pesa bwana", ililikuwa ni sauti ya Karani bosi wake Mr Rasi. Siku hiyo usiku palikuwa na pambano la V.I.P. Kwahiyo Mr Rasi lazima afike bila kuchelewa.
"Sawa nakuja bosi nipo njiani muda huu",alijibu Mr Rasi kisha akakata simu huku akikanyaga breki. Alishusha pumzi kwa nguvu kisha akageuza gari kuelekea ukumbini tayari kwa niaba ya mpambano ulingoni. Kiukweli moyoni mwake Mr Rasi alijilaumu sana,aliwaza ni lini atakutana uso kwa uso na Zabroni ili alipe kisasi cha wazazi wake lakini pia cha kaka yake ambaye ni Madebe. "Ipo siku yako tu nitakuadabisha", baada ya kuwaza kwa muda mfupi alijisemea maneno hayo Mr Rasi huku akiwa amefura hasira moyoni mwake.
Hatimaye alifika ukumbini,umati wa watu ulikuwa wengi sana. Usiku huo Derick alikuwa ameandaa pambano baada kupita siku nyingi bila kuandaa ligi la tajiri mwenzake ,kwa sababu aliamini kwamba Karani hana mpiganaji anayeweza kufua dafu kwa wapiganaji wake. Ila baada kusikia tetesi kuwa Karani kapata mpambanaji mwingine? Akaona ni heri aje amsabahi kumdhihirishia kwamba kwake bado sana,inabidi azunguke Nchi mbali mbali kumtafuta bingwa anayeweza kuwatetelesha wapiganaji wake.Hakika Derick alijiamini sana. Na hata muda na wasaa wa mpambano ulipo wadia, kabla hawajaanza kutajiana dau. Derick alisikika akimkejeri Karani. Alisema "Oi Karani naona pesa zimkuwasha sana haya funguka kiasi ulicho nacho. Lakini pia ukumbuke kuwa hapa ni daraja la juu na sio uswahilini"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa Derick,nadhani niliwahi kukwambia kwamba. Sio kila umuonapo kobe ameinama basi ukajua anatunga sheria. La hasha kobe mwingine anajiuliza atumie siraha gani kukuangamiza. Mimi ni kama Kobe, amini usiamini leo kwisha habari yako", alijibu Karani kwa kujiamini kabisa huku akiachia na kicheko cha madaha. Derrick naye alicheka sana kisha akasema "Sawa mimi naweka Milioni 500.."
"Naweka Bilon moja nukta tano",alijibu Karani. Hapo ikawa ukaanza ushindani wa kuzidiana dau. Mwishowe wakaafikiana baada Derick kusema atatoa Bilion nane nukta nane. Shangwe zilipuka wakimsifu Derick. Vijana wakaingia ulingoni, mpambanaji na Derick hakuchukua dakika sita ulingoni alipindishwa pua na Mr Rasi akawa amepoteza faham ulingoni. Rasi akaibuka kidedea. Derick alistuka akajiuliza "Mtu huyu wa aina gani?..", wakati huo Karani alisikika akisema "Derick tukutane Sophie hotel, istoshe kajipange upya sasa"
Kipindi hayo yanajili,upande wapili nako Zabroni na Lina tayari wamefika nyumbani. Walikuta Veronica ameshaondoka. Baada salamu na zogo la hapa na pale,mama Lina alimsimulia mwanaye jinsi rafiki yake alivyobadilika kwa sasa baada ya kupata kazi. Na yote kwa yote mama Lina alimpa picha mwanaye ya rafiki yake ambayo alimuachia ili akifika amuonyeshe. Lina alifurahi sana kisha akasema "Jamani Veronica, kabadilika sana daah! " alisema Lina huku akimkabidhi Zabroni ili naye apate kumuona huyo Veronica. Zabroni aliipokea picha hiyo,alipoitazama akamuona ni yule yule anayemtaka siku zote. "Huyu ndio rafiki yako?..", kwa tabasamu alihoji Zabroni. Lina huku alijibu "Haswaa wa kufa na kuzikana",baada Zabroni kujibiwa na mpenzi wake,alikaaa kimya huku moyoni mwake akijisemea "Naam! hapa sasa mchezo unakaribia kuisha. Nadhiri yangu ipo pale pale lazima.. Lazima.. Lazima nibandue nyeti yake. Mimi ni Zabroni ", akamaliza kwa kicheko ambacho alikichekea moyoni.


Zabroni alipania kumfanya Veronica hicho kitendo sababu tayari aliamini hilo suala linakwenda kutimia sababu anaukaribu na mtu huyo ambaye alimtia kitanzini baada kumteka kimapenzi.
Zogo kadha wa kadha ziliendelea hapo,na mara baada kuhitimisha maongezi yao waliaga na kisha kuondoka zao.
Walipokuwa njia wakirudi nyumbani kwao,Lina alimwambia mpenzi wake waende club mara moja japo kupozesha koo kwa kupata kinywaji baridi lakini pia nyama choma. Zabroni alikubali. Walielekea kwenye club moja iliyofahamika kwa jina Alminat Club,hapo palikuwa na kila aina ya vinywaji vile vile walimbwende wazuri ambao shughuli zao ilikuwa ni kusambaza vinywaji huku baadhi yao ambao wanafahamika kwa majina changudoa,wao walikuwa nje kidogo ya kumbi hiyo ya starehe,wao shughuli zao ilikuwa ni kuuza miili yao.
Walipofika mahala hapo wakwanza kushuka alikuwa Zabroni ambapo aliposhuka alizipiga hatua kuelekea kwenye mlango wa gari upande ule aliokaa Lina,alimfungulia mlango kisha akaubana na funguo akamshika kiuno wakaelekea ndani ya kumbi hiyo kupata walau chochote.
Walikunywa na kula nyama choma,walipohakikisha wametosheka ipasavyo waliondoka zao. Lakini wakati wanaondoka nyuma yao alionekana tajiri Derick akiwa na wapambe wake. Derick alionekana kuvurugwa mno baada kushindwa pambano aliloandaa na Mr Karan,hivyo alikunywa pombe sana ila alipomuona Lina alisitisha zoezi hilo la kunywa pombe kwa pupa,akamuita mpambe wake mmoja kisha akamuambia afanye juu chini amleta Lina mbele yake ili akakeshe naye usiku mzima. "Unanisikia vizuri? Nakutuma. Nenda kamlete yule mrembo aliyeondoka humu ndani hivi punde, nataka nikalale naye usiku kucha, akitaka pesa mwambie atapata kiasi chochote anacho kitaka,akikataa tumia uzoefu wako. Haya haraka sana nenda. Aam..no no noooo.. nendeni watu watatu mkafanye hiyo kazi ",alisema Derick kwa sauti ya kilevi, na alipokwisha kusema hivyo akamimina pombe kwenye grasi kisha akanywa mfurulizo. Wapambe wake baada kusikiliza matakwa ya bosi wao haraka sana walikwenda kutimiza azimio. Walipolifikia gari la Zabroni walimkuta Lina akiwa amesimama nje akimngojea mpenzi wake ambaye muda huo alikuwa amekwenda kumnunulia vocha kwenye duka ambalo lilikuwa hatua kadhaa kutoka mahali ilipo kumbi ile ya starehe.
"Habari yako mrembo ",alisema mmoja ya wapambe wa Derrick huku akiachia tabasamu bashasha.
"Nyie akina nani?..", kwa taharuki Lina alihoji huku akiwatilia shaka hao watu..
"Sisi ni wasaka tonge ili mwisho wa siku tuwapate warembo wazuri kama wewe, amini kuna bosi wetu amekupenda. Na anataka ukalale naye usiku kucha atakupa kiasi chochote cha fedha utakacho hitaji",alijibu kwa kujiamini mpambe wa Derick. Lina alikunja uso kwa hasira kisha akasema "Acheni upuuzi wenu,machangudoa hamjawaona mpaka mnifuate mimi? "
"Kwahiyo hutaki?.." aliulizwa Lina.
"Ndio sitaki!..",alijibu hivyo Lina wakati huo akitazama huku na kule kwa mbali akimuona Zabloni anakuja.
Baada Lina kuweka pingamizi,kiongozi wa hao wapambe aliamuru wambebe kwa nguvu ilimradi wamfikikishe katika mikono ya bosi wao. Upesi upesi wakanza kufanya kazi hiyo. Kitendo hicho kiliweza kuzua furumai kubwa eneo hilo lakini ghafla lilitulia baada mtukutuku Zabroni kufika.
"Mnataka nini?.." ,aliongea kwa sauti ya juu Zabroni. Wapambe wa Derrick waliposikia sauti hiyo waligeuka kumtazama mtu huyo aliyepasa sauti yake kwa ukali. Wakamuona Zabroni, ajabu wakatazamana kisha wakaangua kicheko.
"Wewe ni kama nani unajiamini na kuongea huo ujinga wako?..", mmoja wao alimuuliza Zabroni.
"Mimi ni Ramso, nasema sihitaji tufike pabaya. Achana na mpenzi wangu?.."
"Ahahahaha! Eti mpenzi wako. Braza muonekano wako kamwe hauendani na chombo unachomiliki..."
"Unaamana gani?..", akahoji Zabroni.
"Utajua nini namanisha! Apeche,hebu kula naye sahani moja huyo", kiongozi mkuu wa msafara mfupi uliokuwa na dhumuni la kumtaka Lina alitoa amri mpambe Apeche apigane na Zabroni,lakini Apache hakuweza kufurukuta zaidi alipotaka kurusha ngumi,Zabroni aliudaka mkono wake kisha naye akamrushia ngumi kupitia ule mkono wenye hirizi. Ilikuwa ngumi nzito, lakini bahati nzuri ngumi hiyo haikumfikia ila upepo uliosababishwa na uzito wa ngumi ile ulimfanya Apeche kukimbia kumuita bosi wake ndani ili walau aongeze wapambe wengine.
"Acha ujinga,unaweza kuniambia huyo jamaa anajua sana ngumi kiasi kwamba awashinde watu watatu?..", kwa hamaki alihoji Derick.
"Ndio bosi,huyu mtu sio wa kawaida kabisa t ",alijibu Apeche huku akitetemeka mwili mzima.
"Haya twende nikashudie", Derick alitoka ndani akazipiga hatua kuelekea nje ambapo pallikuwa na mpambano mkali kati ya wapambe wake na Zabroni. Lakini alipofika nje alikuta gari ya Zabroni inaondoka zake huku chini watu wake wakigagaa wakiwa wameshika mbavu zao wakihisi maumivu makali. Derick akaona Zabroni bila shaka anaweza kumpoza machungu,haraka sana alisogelea gari yake akamuambia dereva aifuate nyuma gari ya Zabroni. Wakati huo ndani ya gari Lina alikuwa akimwangalia Zabroni mara mbili mbili akimshangaa sana kamwe hakujua kama mpenzi wake ni moto wa kuotea mbali kwenye masuala ya ngumi. "Doh Ramso mpenzi kumbe unajua sana,unapiga kama..",kabla Lina hajamalizia kusema alichotaka kukusema,mara ghafla Zabroni akamuambia "Naomba funga mkanda mamaa,tunafuatiliwa nyuma" , aliongea kwa msisitizo Zabroni huku akiitazama gari iliyopo nyuma kupitia kioo cha pembeni (Side Mirror). Lina alituka haraka sana alipandisha kioo kisha akakaza mkanda ipasavyo. Zabroni aliendesha gari kwa kasi kuikimbia gari lile la Mr Derrick ila baadae akaona liwalo na liwe hakuona haja ya kukimbia akahofia kusababisha ajari bila sababu ya msingi,aliweka gari kando kisha akashuka. Wakati huo huo Derick naye aliweka gari kando kisha akashuka.
"Habari yako kaka mkubwa!.. Aaamh hakuna haja ya uhasama. Mimi ni mtu mwema sana na nimependa mapigo yako kwahiyo kama hutojali Naomba tupige pesa",alisema Derick huku akitabasamu. Zabroni alikumbuka siku za nyuma kidogo jinsi Mr Rasi alivyo mchukulia mpenzi wake,akawaza "Ama Tina alipenda upigaji wa Rasi? Na dhani hawa ndio wale wale acha nikubali ili nimuonyeshe Tina kuwa alichokipenda kwa Rasi hata mimi ninacho pia", kwisha kuwaza hayo akaachia tabasamu akionekana kufurahi dili tata lililopo mbele yake pasipo kujua kuwa Mr Rasi ndio Bruno kijana ambaye anamsaka kwa udi na uvumba ili alipe kisasi cha kifo cha kaka yake Madebe lakini vile vile cha wazazi wake.
"Nashukuru kukufahamu",alijibu Zabroni.
"OK kama hutojali shika kadi hii,ina namba zangu kesho nipigie ili tufanye kazi" , aliongeza kusema Derick. Upesi Zabroni alipokea kadi hiyo kisha akarudi ndani ya gari wakaondoka zao huku nyuma wakimuacha Derick akijinasibu kwa kusema "Karan umekwishaaaaa" .
*****
Kesho yake Zabroni aliwasiliana na Derick pasipo Lina kujua mkakati wake,makubaliano yalifanyika na mikataba ikasainiwa. Hivyo kilichokuwa kimebaki ni Zabroni kuanza kazi,na kizuri zaidi aliambiwa kamwe hatofatiliwa na serikali kwani wao pia ni serikali tosha. Jambo hilo lilimpa matumaini kibao Zabroni istoshe aliambiwa pindi atakaposhinda mpambano atapata pesa za kutosha ambayo itamfanya aendeshe vema maisha yake. Kumbe kipindi Zabroni anaaminishwa jambo hilo,upande wa pili tayari siri ilibuma baada kubainika kazi inayofanyika haipo kisheria yani kihalali. Ipo kiharamu zaidi,hivyo serikali iliamuwa kuwafukuza wale wahusika ambao wapo serikalini waliokuwa wakipokea rushwa kutoka kwa matajiri hao waliokuwa wakifanya kazi hiyo pasipo kibari maalumu na sasa shunghuli nzima ikabaki kuwakamata wahusika wakuu Karani na mwenzake wa kuitwa Derick pia na wengineo wachache.
Siku zilisogea,Zabroni sasa akawa ananogojea siku ya pambano iweze kufika ili apate ujiko mbele ya mpenzi wake wa zamani ambaye ni Tina. Hatimaye siku moja saa ya jioni simu yake ya mkononi iliita alipotazama jina akaona Derick bosi wake amempigia kwa wakati huo . Zabroni alipokea. Derick akasema "Rasmo jiandae sasa wiki ijayo utakuwa na pambano kali,kama unamjua ama umeshawahi kumsikia jamaa mmoja hivi anaye itwa Mr Rasi. Huyo ndio utapigana naye kwahiyo inabidi ujifue vya kutosha sitaki uniangushe sababu pambano hilo ndio litatufanya kuuaga umaskini", akamaliza kwa kicheko Derick.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa bosi kwa hilo ondoa shaka.",alijibu Zabroni kisha akainua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu sababu alihisi Mungu kayjibu maombi yake ya muda mrefu.
"Hahahaha, pasipo na shaka. Mungu amejibu maombi yangu", alijisemea kwa furaha wakati huo akitamani siku hiyo usike iwahi kufika.
Siku tatu nyuma kabla siku yenyewe ya mpambano haijawadia,ndio siku ambayo Zabroni alianza kupanga mkakati wa kumaliza azima yake iliyomtorosha jela kwa sababu alisikia Lina akiongea na Veronica akimwambia kuwa siku si nyingi atakuja kumtembelea. Siku hiyo ilipofika,Lina alimpasha habari hiyo njema mtukutu Zabroni. Habari hiyo ilipomfikia Zabroni hakika alifurahi sana. Kwa tabasamu bashasha akasema "Jambo jema sana mpenzi lakini pia itabidi tumpe taarifa kwamba mwezi ujao tunatarajia kufunga ndoa"
"Ahahahah, sawa", Lina alikubaliana na wazo la Zabroni na hata asijue ya kwamba Zabroni hana wazo la kufunga naye ndoa ila yupo katika jiji la Dar es salaam kimpango tu wa kutimiza nadhiri yake aliyopania.
Majira ya saa saba mchana,ndio safari ya Veronica ilipoanza kuelekea mahali anapoishi rafiki yake na mpenzi wake. Alipewa maelekezo mpaka akafanikiwa kufika ingawa aliishia nje kwa sababu nyumba ilikuwa kubwa halafu istoshe ilikuwa kimya sana. Lakini wakati yupo nje,Zabroni alifunua pazia kutazama nje, macho yake mawili yakapata kuiona gari Rava4 ya Veronica ikiwa imesimama nje. Akaachia tabasamu pana kisha akafunika dirisha kwa pazia ikiwa muda huo huo Lina alitoka ndani upesi akamfuata Veronica nje. Alipomfikisha sebuleni ghafla simu yeke ikaita, ni mama yake ndio aliyempigia. Lina alipokea ikasikika sauti ya mama yake ikisema "Lina fanya haraka uje baba yako kakamatwa na jeshi la polisi,tafadhali njoo mwenyewe usije na Ramso. Njoo moja kwa moja hapa kituo Stakishari ", kwisha kusema hayo simu ilikatika. Lina akastushwa na taarifa hiyo, haraka sana akajiandaa akamuaga Zabroni kiaina pia akamuaga na Veronica akimwambia kuwa aendelee kumsubiri anakuja muda si mrefu huku akimtaka amngoje huku wakipiga zogo na shemeji yake pasipo kujua kwamba kakabidhi fisi bucha.
Veronica alitulia sebuleni akimngojea shemeji yake aje ili waongee mambo mawili matatu,punde si punde naye akatokea. Ni Zabloni. Veronica alistuka kumuona mtukutu huyo,akiwa na hofu dhufo lihari akasema "Ni Wewe ama macho yangu?..", mtukutu Zabroni akiwa amekunja sura yake kwa hasira na ghadhabu akajibu
"Ndio ni mimi Zabroni ukajua nani?..."


Ulijiona mjanja sana! Ukasau kutambua kwanini mungu alianza kumuumba mwanaume na sio mwanamke?.. Veronica mshahara wa dhambi siku zote huwa ni mauti", alisema Zabroni kisha akachomoa kisu kikali, alizamilia kumuuwa Veronica. Veronica akastaajabu sana kumuona mtukutu huyo kwa mara nyingine tena, alijua tayari yupo matatani na hivyo haraka sana akaomba msamaha lakini Zabroni kwa muda huo hakuwa tayari kutoa msamaha, moyoni aliamini kuwa malipo huwa ni hapa hapa Duniani na mbiguni ni hukumu tu. Basi upesi akamchoma kisu upande wa titi la kulia,Veronica alipasa sauti ya kilo huku akizidi akiomba msamaha. Lakini Zabroni hakutaka kuelewa alirudia mara ya pili kisha mara ya tatu akakiingiza kisu hicho hicho sehemu nyeti ya Veronica, hapo Veronica alirusha miguu huku na kule akakata roho. Hakika ulikuwa unyama uliokidhiri alio ufanya Zabroni ambapo hakuona haja ya kuendelea kukaa katika nyumba hiyo, alitimua mbio. Alipofika nje hakuikuta gari, Tina aliondoka nayo. Hapo sasa Zabroni alijihisi kuchanganyikiwa haraka sana alimpigi simu Derick ili amtume mpambe wake aje kumchukuwa,kweli punde si punde gari ilifika. Zabroni alipanda safari ikaanza, safari ya kwenda kwenye mpambano huku nyuma tayari akiwa ameshamaliza azma yake. Istoshe hiyo siku ndio ilikuwa siku ya mpambano.
Hatimaye walifika ukumbini,ndani ya dakika kadhaa alipanda ulingoni. Bei zalitajwa kati ya Derick na Karani. Wakati huo Zabroni akijua mtu anayetarajia kukutana naye kwenye mpambano huo,huku mr Rasi ama Bruno yeye akiwa hatambui ni nani anayekutana naye. Lakini punde si punde Rasi alipopanda ulingoni alimtambua. Ni Zabroni. Yule yule aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba pasipo kumpata ikiwa muda huo huo matajiri walifikia muafaka,ndondi zilianza huku Mr Rasi akiwa na nguvu mpya na hali mpya baada kumuona mbaya wake. Na kabla hajarusha ngumi,alisema "Naitwa Bruno,nimetoroka mahabusu kwa ajili yako. Unamkumbuka Madebe?..".
"Maneno mengi humaliza vitendo, Ulivamia vita isiyokuhusu. Lakini kwa kuwa tumekutana kwa mara nyingine tena basi acha nikuadanishe. Ili azma yangu itimie. Unakumbuka kama nilikusamehe kipindi kile ? Sasa hatimaye tumekutana upya",alijibu kwa kujiamini kabisa Zabroni kisha ngumi zikaanza huku shangwe nazo za hapa na pale zikisikika, Bruno alionekana kutawala ulingo kwa sababu alikuwa na ile nguvu ya kupotea na kuibukia sehemu nyingine. Ila Zabroni alitumia nguvu ya hirizi aliyokuwa nayo ambapo aliweza kurusha ngumi nzito kiasi kwamba mpambano ule ukaonekana ni wa watu walikuubuhu. Wataalamu wa kupigana.
Wakati ugomvi huo unaendelea,upande wa pili Lina kuna kitu alikisahau,hivyo ilimbidi arudi mara moja nyumbani. Alipofika aliona damu nyingi ikiwa imesambaa kwenye sakafu,alistuka lakini alizidi kusonga mbele na hatimaye akamkuta Veronica akiwa ameuwawa kikatili. "RAMSOOO? ", alijiuliza Lina huku akiwa na taharuki kubwa moyoni mwake.

Wakati Lina yupo kwenye kwenye hofu dhufo lihari akishindwa kuamini kile akionacho, kwingineko napo pambano lilizidi kupamba moto Tina akiwa jukwaani akitamani sana Mr Rasi ammalize Zabroni ili iwe kama njia ya kulipiza kisasi cha kuwauwa aliwaua wazazi wake mzee Fungafunga na mkewe,na ndio maana siku hiyo Tina akawa anatamani Bruno amuadabishe Zabroni akiamini kuwa walau moyo wake utaridhika. Pindi Tina anatamani kitu hicho kiweze kutokea, upande wa Zabroni naye alikuwa akifanya jitihada za kusaka ujiko mbele ya Tina ili ajue kwamba bado yeye ni mwamba ulioshindikanika. Hakika ulikuwa mpambano mzuri sana,lakini ghafla polisi walifika kwenye tukio,walipiga risasi juu watu wakasambaaa. Mlio huo wa risasi ulimstua Bruno ukawa umemtoka mchezoni,nafasi hiyo Zabroni aliitumia kurusha ngumi kwa kutumia mkono wake wenye hirizi, ngumi hiyo ilipomfikia Mr Rasi alianguka chini kisha mapovu yakaanza kumtoka huku akirusha miguu huku na kule. Ilikuwa ngumi nzito yenye uchawi ndani yake. Amri ilisikika kutoka kwa jeshi la polisi lililofika mahali hapo,walimkamata Zabroni pia na Karani ikiwa Derick yeye alifanikiwa kukimbia.
Moja kwa moja watu hao wakafikishwa mbaloni ambapo walimkuta Afande Jimmy tayari yupo mikononi mwa mkono wa dora baada kubainika kuwa anaishi na mfungwa aliyetoroka jela kinyemela. Zabroni alipomuona baba yake mkwe yupo chini ya ulinzi makali alitambua fika kuwa yeye ndio chanzo cha hilo tatizo, hivyo aliweka bayana kuwa yupo tayari kwa chochote watakacho mfanyia ilimradi kamanda Jimmy wamuache huru ilihari moyoni akijisemea kuwa azmaa yake nimehitishi hakuna cha kupoteza. punde Lina akatokea hapo kituoni kwa sauti kali akasema "Ramso kumbe wewe muuwaji,kwanini umemuua Veronica? Kwanini lakini. Amekukosea nini " ,alihoji Lina kwa sauti ya kilio,muda huo huo nyuma yake Lina alitokea Tina. Naye akasema huku akilia kwa uchungu "Zabroni, mwanaume gani wewe? Mbona mkatili sana. Umeniulia wazazi wangu,leo hii umemuuwa na mpenzi wangu kwanini Zabroni kwanini lakini...". Zabroni hakujibu, alinyamanza kimya,habari ya kifo cha Bruno kikimuacha mdomo wazi, akajisemea "Inamaana Bruno naye kafa? Laah! sikutegemea ingawa ni moja ya kisasi cha rafiki yangu Bukulu. Mungu anisamehe",alijisemea hivyo Zabroni wakati huo huo Lina akachomoa bastola kutoka kwa polisi mmoja aliyekuwepo karibu yake kisha akajiwekea kichwani na kisha kusema "Ahsante Ramso kwa mshahara wako,siwezi kuvumilia hii fedhaha.. Kwanini umekuwa na roho mbaya namna hii? Siwezi siwezi kabisa kuishi najiua, ", Lina alipokwisha kusema hivyo akajivyatulia risasi. Zabroni hakuamini machoni mwake, akataharuki sana kwa sauti ya juu akasema "Hapanaaaa Lina usifanye hivyo"
"Hapana Linaaaa",hapo ghafla akazinduka baada kupoteza fahamu kwa muda mrefu. Jopo la madaktari liliingia wodin kumtazama mgonjwa wao aliyekuwa amepoteza kumbukumbu kwa muda wa siku tatu. Walimkuta akiwa ameketi kitandani huku akihema haraka haraka, mapigo ya moyo wake yalienda mbio kama saa mbovu ilihari kijasho chembamba nacho kikiuosha mwili wake. Pumzi ndefu akashusha, macho yake akayainua kutazama huku na kule na mwishowe kujikuta akiwa katika hali ya sintofahamu baada kugundua yupo Hospital.
"Hali yako?", sauti ya Dokta ilisikika akimuuliza Zabroni. Zabroni huku akisafa akajibu "Njema tu, aah unaweza kuniambia nimefikaje fikaje mahali hapa?.."
"Ndio, uliletwa ukiwa hujitambui. Ulizimia", Zabroni akataharuki kusikia habari hiyo, ndani ya kichwa chake akajiuliza "Inamaana kumbe yote yale nilikuwa nimezimia?..", hakika alijikuta amepoa mithiri ya maji ya mtungini wakati huo akikumbuka mara ya mwisho kabla hajapoteza fahamu alikuwa na nani na pia alifanya nini. Akakumbuka kuwa alikuwa na mzee Maboso raia kutoka Nchini Nigeria, na walikuwa katika ufukwe wa ziwa Victoria saa za jioni wakijiandaa kuingia kuvua samaki, lakini kabla hawajaingia mzee Maboso akawa amemwambia Zabroni kuwa ziwani kuna mambo mengi sana, kwa maana hiyo si rahisi kuingia pasipo kupakwa dawa ambayo itamrinda na mauza uza ya baharini.
"Sawa mzee wangu mimi nakusikiliza wewe tu, kwa sababu siku zote ukitaka kuruka sharti uagane na nyonga", alijibu Zabroni. Mzee Maboso, mzee ambaye kwenye safari ile ya kulipa kisasi cha kifo cha wazazi wake alimpatia dawa ya kupotea kimazingara, aliangua kicheko kisha akasema "Ni kweli kabisa, lakini yakupasa kujiamini ili ikuwee vyepesi kuzoea hii shughuli"
"Sawa", Zabroni akawa tayari kupakwa dawa ile ambayo mahususi kuzuia janga litakalo tokea ziwani. Mzee Maboso akampaka Zabroni dawa katika paji la uso wake na mikononi pia, na baada zoezi hilo kukamilika ghafla Zabroni akahisi kizungu zungu, baadaye hakujua kilicho mpaka pale alipojikuta yupo wodini huku akiwa ameota mambo ya ajabu sana.

BAADA SIKU TATU
Aliruhusiwa kurudi nyumbani, siku hiyo alilala usingizi mzito. Na pindi alipokuwa amesinzia mambo yale yale yakajirudia kwa mara nyingine tena katika ndoto kwa matukio tofauti tofauti. Ndoto ya ajabu kabisa kuwahi tokea kwa kijana huyo. Ndoto ambayo alianza kuiota usiku wa jana yake yake saa tatu alipopitiwa na lepe la usingizi,usingizi ambao alilala fo fo fo kutokana uchovu mwingi aliokuwa nao baada kutoka Hospital,alihema kwa nguvu baada kutoka usingizini,siku hiyo alichelewa pia kuamka. Akiwa kitandani anaitafakari ndoto hiyo,alisikia sauti ya mtu akibisha hodi. Zabroni aliamka akaenda kumsikiliza. Ni Tina mpenzi wake,alikuja kumjulia hali baada kusikia kwamba amerejea kutoka Hospital.
"Khe Zabroni wangu, pole kwa maswahibu?..", alisema Tina ambaye alimuota akiwa amehamisha mapenzi yake kwa Bruno ama Mr Rasi.
"Daah we acha tu Tina,kwanza baba na mama yako wazima?..",alijibu Zabroni huku akiacha na swali ambalo liliambatana na miayo.
"Ndio kwani vipi kuna tatizo?.."
"Hapana, hakuna tatizo",alijibu Zabroni.
"Mmmh! Unanificha wewe hebu niambie ukweli wako basi "
"Tina usihofu hakuna tatizo"
"Sawa, nimepita tu kukujulia hali. Naelekea kisimani kuchota maji.."
"Sawa baadae basi",alikatisha maongezi Zabroni kisha akarudi ndani kuitafakali ndoto hiyo na ukweli wa kuhusu mzee Maboso.
"Ndoto hii? Inamana gani?. Na huyu mzee Maboso alifanyia kitu gani hasa Loh! Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni. Naam! Leo nimepata kujionea maajabu makubwa katika ulimwengu usio wa kawaida" Yote hayo Zabroni alikuwa akijisemea ndani ya kichwa chake. Na baadahe jioni alitembea kijiji kizima, alipita hasa zile nyumba ambazo kwenye ndoto aliota kuwa amechoma moto. Alikuta zipo salama salimini. Vile vile alipita nyumbani kwa mama yule mjamzito ambaye kwenye ndoto aliota kwamba kamtumbua mimba yake. Hapo alikuta umati wa wamama wakiwa nje, kwa mbali Zabroni alisikia kuwa huyo mama amejifungua mtoto wa kike. Zabroni alishusha pumzi kisha akaendelea na safari moja kwa moja alielekea mpaka kijiweni, huko sasa alikutana na kundi la vijana wakipiga zogo huku birika lenye chai ya tangawizi likiwa mbele yao. Katika vijana hao alikuwemo na Bluyner,kijana ambaye Zabroni alimuota kwamba Bluyner ni nyampara gerezani. Nyampala ambaye alimpa taabu sana kwa kumkosesha amani gerezani.
"Zabroni,pole sana kwa matatizo bwana", alisema Bluyner. Zabroni alibaki kushangaa tu huku akilini bado akiitafakari ile ndoto. Alikaa kijiweni dakika kadhaa kisha akarudi nyumbani kwao kutuliza akili, alipokuwa njiani kabla hajafika nyumbani kwao alikutana na mzee Maboso,mzee ambaye alilowea Tanzania ila mzawa wa Nchini Nigeria. Kwenye ndoto Zabroni alimuota mzee huyo kuwa alimpatia dawa ambayo ilimfanya awe mtu wa kupotea katika mazingira yoyote,lakini pia awe mtu mwenye nguvu za ajabu. Zabroni alimsalimia mzee Maboso, Maboso akaitikia salamu hiyo kisha akasema "Pole sana kijana wangu ila kuna jambo nitakueleza".
"Jambo gani hilo?", Zabroni akauuliza kwa mashaka.
"Ahahah usijali ondoa papara ila leo soka limechezwa kwa uzuri kabisa. Timu yetu ya kijiji imeshinda lakini tuwashukuru wale vijana wageni walee..Bruno na kaka yake Madebe. Loh! Vijana wale wanajua sana soka sio mchezo. Nafikiri Miembeni wamewatambua vizuri",aliongeza kusema hivyo Mzee Maboso huku akicheka. "Bruno?..Madebe?.." Zabroni alijiuliza majina hayo, kwenye ndoto aliota namna gani walivyompa shida vijana hao ambao walikuja kijijini kwao kutafuta maisha kwa kulima vibarua, ambapo mwishowe wakajiingiza kwenye vita isiyowahusu.
"Unataka kuniambia hawa wageni ndio wametusaidia?..",aliuliza Zabroni kwa wasi wasi. Mzee Maboso alijibu "Haswaa, na huyu Bruno kapiga mpira mwingi sana. Mpaka kuna mwanadada mmoja hivi amempatia pesa"
"Nani huyo?..", alihoji Zabroni.
"Kwa jina nimesikia anaitwa Veronica, ni binti fulani hivi mgeni alikuja kushuhudia mchezo wa leo"
"Veronica?"
"Ndio! Kwani unamfahamu?.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana", alikataa Zabroni ila alijua fika ni Veronica mwadada ambaye kwenye ndoto aliota namna alivyomtia hatiani baada kumuamini katika mapenzi..
"Na sio huyo tu, Zabroni umekosa vingi. Ukweli mchezo wa lao ulijaza mabinti wengi. Nafikiri ungelikuwepo ungepata ujiko. Yupo binti mmoja hivi zamani kidogo aliondoka baada wazazi wake kuhamia mjini. Lina. Sijui unakumbuka? Naye alikuwepo pia ..", aliongeza kusema mzee Maboso huku akimaliza kwa kicheko. Ni jambo ambalo lilizidi kumshangaa mno Zabro na baada ya hapo waliagana,Zabroni aliendelea na safari yake ilihali mzee Maboso naye aliendelea na safari yake. Hapo walau furaha ikawa imetawala kwa kijana Zabroni ama wakuitwa mtukutuku, baada kufika nyumbani na kuwakuta wazazi wake wakiwa tayari wamerudi kutoka shamba,huku pembeni akimuona baba yake akiwa na mzee Fungafunga wakisikiliza taarifa ya habari kwenye radio mbao. Wakati kwenye ndoto aliota kwamba mzee huyo Fungafunga alikuwa na uhasama na baba yake.Hivyo Yote hayo ikabaki kuwa ndoto tu kwa kijana Zabroni,lakini aliyakumbuka maneno ya mzee Maboso "Pole sana kijana wangu ila kuna jambo nitakueleza",kwisha kuyakumbuka maneno hayo akaishia kutabasamu tu ikiwa upande wa pili Mzee Maboso akacheka sana Kishan akajisemea "Lengo langu litatimia tu"

***MWISHO**"



(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.