Simulizi: Je haya Ni Mapenzi Sehemu Ya Tatu (03)

Sakina hakuwa na tatizo kwa
jina ambalo Sabrina alimpa mtoto wao ila Juma bado hilo jina hakulitaka
kutokana na mambo ambayo yalimtokea nyuma.
Aliwahi kuwa na urafiki na mtu mmoja aliyekuwa akiita hivyo kisha yule mtu
wakagombana nae na kuweka chuki za milele kwani yule mtu naye alikuwa
akimuhitaji Sakina na kufanya ugomvi wao uwe mkubwa kupita wa kwanza.
Hivyo Juma hakutaka mwanae aitwe jina la adui yake, Sakina akamuuliza mumewe
"Sasa huyu mtoto tumuite nani?"
"Tumuite tu mtoto hadi pale nitakapompatia jina ninalolitaka"
"Mpaka lini sasa?"
"Leo leo nitampa jina kama umechoka kumuita mtoto"
Sakina hakutaka kugombana na mumewe hivyobasi akafanya kama alivyotaka.
Sakina akatembelewa na jirani yao mmoja kwa lengo la kumuona mtoto ila nae
alimkuta mtoto amelala, huyu jirani alimshangaza Sakina kwa maswali ambayo
alimuuliza kwani yalikuwa ni maswali ya mshangao
"Hivi ulijifunguaje Sakina?"
"Nilijifungua kawaida tu"
"Kawaida kabisaa!!"
"Ndio kawaida kwani wewe ulijua ni nini"
"Basi"
Akainuka na kuondoka bila hata ya kuaga na kumfanya Sakina apate maswali mengi
sana kwenye kichwa chake kwani hakuelewa yule jirani alimaanisha nini.
Joyce alipokuwa anajiandaa kwenda kwa Sakina akapigiwa simu na wifi yake kisha
akaambiwa
"Kuna jirani yenu hapo si mtu mzuri, kwahiyo kuwa makini na watoto
wifi"
"Jirani gani huyo?"
"Simjui ila ndio hivyo"
Kisha akakata simu na kumfanya Joy ajiulize maswali na kujisemea
"Simu za huyu huwa sio za kheri kwakweli bora hata asiwe ananipigia jamani
kwani ananitisha tu"
Kisha akamuita mwanae na kumwambia kuwa waende kwa Sakina kumuona kwani ndivyo
alivyopanga nae mwanzo kuwa wataenda kumuona ukizingatia Sabrina hakumuona tena
toka siku wametoka hospitali ingawa nyumba wanayoishi ndio hapo hapo.
Walimkuta Sakina akiwa na mtoto wake kama kawaida na mume wake naye alikuwepo.
Sakina aliwaeleza kuhusu yule jirani aliyekuja kumuona na maswali ambayo
alikuwa akimuuliza, ikabidi Joyce aulize vizuri kuhusu huyo jirani
"Ni nani huyo?"
"Si yule mama jembe"
Sabrina akashtuka sana na kufanya wamuulize vizuri kuwa kwanini ameshtuka vile.
"Wakati ulipokuwa mule ndani kabla ya kuniita mimi, nilimuona huyo mama
jembe kwenye mlango wa kule mlipokuwa"
Wote wakamshangaa na kumuuliza kama anauhakika, Sabrina naye aliwahakikishia
kabisa ila Sakina akasema kuwa atafanya kitu ili ajue ni wapi kuna huo mzizi wa
fitina.
Wakati wanazungumza, Juma nae akasogea na kuwatajia jina aliloamua mwanae
aitwe.
"Kuanzia sasa mwanangu ataitwa Jabali"
Sabrina akachukia sana kuona yule mtoto amebalishwa jina.
Sakina hakuwa na neno, ila kwavile mwanae alikuwa nae mkononi akajaribu kumuita
hilo jina aone kama litampendeza mtoto wao.
"Jabali"
Gafla hali ya hewa ilibadilika mule ndani kisha giza likatanda, na yule mtoto
alianza kulia kwa nguvu kama ameangushwa chini.
Gafla hali ya hewa ilibadilika mule ndani kisha giza
likatanda, na yule mtoto alianza kulia kwa nguvu
kama ameangushwa chini.
Sakina alishtuka sana na kutetemeka kwani hakuelewa tatizo ni jina au ni kitu
gani.
Giza lilitanda kwenye nyumba yao na kufanya wote waanze kuogopa, na ile sauti
ya mtoto kulia iliwafanya wazidi kupatwa na mashaka.
Sakina alijikuta akimbadilisha mwanae jina pale pale.
"Basi nyamaza mwanangu Jeff"
Ni kweli yule mtoto alinyamaza ila giza nalo lilizidi kutanda.
Mtu wa kwanza kufanikiwa kushika mlango alikuwa ni Sabrina na kuwafanya wote
watoke nje huku wanashangaa kuwa ni kitu gani kile, yani nyumba ipatwe na giza
la gafla kama vile kwakweli ilikuwa ni hali ya ajabu kwani haikuwahi kuwatokea.
Ikabidi wote waelekee ndani kwa Deo ambaye aliwashangaa na kuuliza
"Kwani mtoto ameshaanza kutoka nje?"
"Maajabu ya mule ndani leo imetubidi tu tutoke nae"
"Maajabu gani?"
"Yani mule ndani mmeingia giza la gafla"
"Nyumba yangu mimi inaingiaje giza la gafla?"
Deo akataka kwenda kushuhudia ila mkewe akamzuia lakini Deo hakutaka kusikiliza
kisha akatoka na kwenda kuangalia, Joy hakuwa na jinsi zaidi ya kumfata nyuma
mumewe.
Deo alipofika aliingia ndani ila hali ilikuwa kawaida tu wala hakuona hilo giza
walilolesema, Deo akatoka huku anacheka kwa kusikitika na kurudi ndani kwake
huku Joy akimfata nyuma.
Deo kufika ndani akawa anawauliza kwa kucheka
"Haya hilo giza liko wapi?"
"Lilikuwepo mule ndani"
"Kweli nimeamini mna mashetani nyie sio bure kabisa"
Akainuka na kwenda chumbani kwake.
Wakaishia kuulizana pale
"Inamaana sisi wote tuna mashetani? mmmh!"
Sakina alisema hawezi kukubaliana na ile hali hivyobasi alipanga kuwa lazima
arudi kwao kabisa na huko ataenda kujua mbivu na mbichi za kwanini imewatokea
vile.
Joy akamuuliza Sakina
"Kwahiyo wewe unaamini ni ushirikina?"
"Ni ushirikina ndio kwasababu hiki sio kitu cha kawaida"
"Mmh waswahili mnamambo jamani, haya nenda ukachunguze mama"
Juma alikuwa katulia tu huku akifikiria kitu cha kufanya.
Baada ya hali kuwa shwari ndipo Juma akamuomba mkewe warudi ndani kwao, naye
akakubali na kurudi ila kesho yake Juma na familia yake wakasafiri na kuondoka
mahali hapo.
Bado Joy hakuwa na furaha na maendeleo ya mtoto wake Sabrina, ndipo alipomuomba
mumewe kuwa wampeleke shule za bweni mtoto wao huyo ambapo Deo aliamua kukubali
kwani maendeleo ya mtoto wake kielimu yalirudi nyuma sana hivyobasi akaona ni
vyema kwenda kujaribisha shule za bweni ili kuona kama atabadilika au vipi.
Makubaliano yalipokamilika, Sabrina akatafutiwa shule na kupelekwa huko ambako
palikuwa mbali kidogo na nyumbani kwao kwahiyo haikuwa rahisi kwa yeye kurudi
tena nyumbani kama ilivyokuwa awali.
Sabrina alipooza sana alipokuwa shuleni na alikuwa ni mtoto mwenye mawazo kwa
muda mwingi na kufanya hata walimu wajiulize kuwa ana tatizo gani na kujaribu
kuwa nae karibu kwa muda mwingi ili kumuweka sawa na ili aweze kufanana na
watoto wengine.
Sakina alirudi nyumbani kwake baada ya mwaka mmoja na mtoto wake Jeff alikuwa
amekuwa kwasasa na aliweza kutembea hata kuzungumza baadhi ya maneno.
Sakina alikawia sana kurudi nyumbani kwake kutokana na mila alizozikuta kwao,
kwahiyo aliyerudi alikuwa ni mumewe na aliishi mwenyewe kwa kipindi chote hicho
ambacho mkewe alikuwa kwao.
Joy alimpokea vizuri sana Sakina kwani ilikuwa ni kipindi kirefu tangia
aondoke.
"Kheee, ndio ulienda kuzamia moja kwa moja!!"
"Kutokana na mambo nilivyoyakuta ilinibidi nifanye hivyo ila sasa nimerudi
na nguvu mpya na kasi mpya"
Joyce alicheka, mengi yaliyofanyika nyuma yalikuwa yameshasahaulika kabisa
kwani mambo mengi yalikuwa ni mapya ila Sakina alirudi na majibu karibia yote
ya mambo ambayo yalifanyika nyuma kati yao na kumfanya Joy apate hamu ya kujua
tena kuwa ni kitu gani na kwanini kilitokea kama ilivyokuwa Kwanza kabisa
alianza kumuuliza Joy
"Hivi mama Jembe bado yupo?"
"Hapana, alihama"
"Nilijua tu kuwa lazima ahame, mimi kwetu Tanga na niliaga kamwe siwezi
kusumbuliwa akili kiasi kile"
"Hebu niambie vizuri Sakina maana hata sikuelewi"
Basi Sakina akaanza kumueleza ilivyokuwa.
"Nilipoondaka hapa nilienda nyumbani kisha nikaenda kwa mtaalamu mmoja
huko kwetu na akanieleza kila kitu.
Kumbe mimi nilifungwa ile mimba ili nisijifungue ndiomana miezi ilipitiliza
bila hata ya kuwa na dalili yoyote ya kujifungua, kwakweli nilichoka ndiomana
nikaamua kwenda kule msituni na Sabrina.
Moyo wangu ulikuwa unaniambia kuwa Sabrina ndio mtu pekee wa kunisaidia hata
nikipatwa chochote huko porini sababu ya upendo niliokuwa nao kwake hata yeye
pia alinipenda.
Wakati tunarudi kutoka kwenye kale kapori tukakutana na chatu, kumbe hakuwa
chatu bali alikuwa ni huyo huyo mama Jembe hadi mimi nikamuangukia Sabrina na
hapo akajua kuwa amemaliza kazi. Nia yake ni kuvunja mahusiano yetu ndiomana
kuna kipindi hata wewe ulikuwa unanichukia bila sababu yoyote ile.
Ila Mungu mkubwa kwani tulipata msaada na kuwaishwa hospitali na mie
nikapelekwa leba ili nikajifungue sababu mtoto alikuwa mlangoni kabisa ila
hakutoka kumbe muda wote huo, huyu mwanamke mbaya alikuwa anazuia ili
nisijifungue.
Nilipoomba waniitie Sabrina ndio hapo alipochukia na kuja kumalizia kwako
hasira zake zote.
Nia yake ilikuwa ufe ila Mungu amekusaidia kwakweli sababu kile kitendo cha
wewe kuondoka pale hospitali ndio ilikuwa pona yako badala yake watu aliowatuma
wakammaliza mtu waliyemkuta amelazwa pale.
Na uliporudi nyumbani alitaka amalizie hasira zake kwa mumeo ila yule wifi yako
aligundua kitu ndiomana mumeo akapona.
Yule mama Jembe alikuwa mbaya sana, na mimi nimemfanyia yangu hadi
amehama"
Joy alikuwa kimya akisikiliza huku akisikitika sana kwani hakujua kama yule jirani
angemfanyia vile kama alivyosimuliwa na Sakina kwahiyo akaishia kushangaa tu.
Baada ya yote hayo, Sakina akamuomba Joy kusahau yaliyopita na kuanza ukurasa
mpya wa maisha bila kubughuziwa na mtu yeyote yule. Na maisha yakaendelea kama
kawaida, ingawa Sakina aligundua kuwa mumewe ana mwanamke mwingine.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: