OMBA PESA! OMBA TENA! KAMA HAKUPI OMBA TENA! KAMA HUWEZI KUOMBA KAA KIMYA ACHA KULALAMIKA WENZAKO WAKIPEWA!

The personal Blog of Gualbert Kashasha: JINSI YA KUMSAHAU MPENZI ...
Mwanaume anapenda kuombwa pesa, kama ambavyo nyie wanawake mnapenda kuona mwanaume anajiongeza na kukupa pesa bila kumuomba ndiyo namna ambavyo hata wanaume nao hupenda kuombwa pesa na mwanamke. Kuna wale wanaume ambao ni bahili wa asili, wale wanaopenda kulelewa ambao hata ukiomba na ukavua nguo ukatembea barabarani uchi bado hatakupa, hapana sizungumzii hao, nazungumzia wanaume wanojitambua.
Ni mwanamke, umeolewa au una mpendi wako, mume wako ana pesa na ni mtu wa kusaidia watu wengine, hapo nyumbani anatoa matumzi lakini hatoi pesa ya vitu vidogo vidogo vyako binafsi. Kwakua una kazi au hata wakati mwingine kazi huna lakini unaogopa kuomba. Wewe ndiyo wale akina dada ambao mnatumia ule mstari ambao unaniboa sana, sijui ni kama mnataka kuonekana kama mna tabia nzuri kuliko wengine, unasema “Mimi sijazoea kumuomba mwanaume pesa!”
Lakini hapohapo wenzako wakiomba na kupewa, wawe ni michepuko, wawe ni ndugu zake, marafiki au wengine unalalamika kuwa hakuhudumii lakini anagawa pesa! Unaboa, yaani mimi napesa zangu halafu unipe kazi nyingine ya kuotea kuwa wewe Pedi zimesiha, unipe kazi ya kwenda kwa mganga kupiga ramli ili nijue Mama yako anaumwa na unahitaji msaada, ndugu yangu nihangaike kutafuta pesa na wakato huo huo nihangaike na kutafuta matatizo yako.
Najua wakati mwingine unajisikia raha ukipewa bila kuomba lakini nasisi wanaume tunasikia raha kuombwa bila kutabiri. Jinsi unavyojisikia raha mumeo akikupa elfu kumi bila sababu ndiyo jinsi wanaume mkeo akikuambia shida yake na wewe kumtatulia, mwanaume unajihisi kama shujaa flani, kama kamfalume flani kuwa mke wako anakutegemea. Njinsi unavyolalamika kuwa mumeo hajiongezi na kukusaidia shida zako ndiyo wanaume wanavyolalamika kua huwaambii chochote unajifanyia mambo yako mwenyewe.
Naomba nimalizie kwa kusema, kama wewe ni wale wakujifanya, narudia wakujifanya eti wao ni wa classy flani hawawezi kumuomba mwanaume pesa, wanaona kama ni umalaya kuomba pesa wengine hata kwa mume wako basi kua classy wa matawi hivyo hivyo na kuacha kulalamika kua hakupi! Sio unajifanya huwezi kuomba lakini una matatizo chungu nzima mpaka kwenye ukucha ulokatika! Unapata matatizo badala ya kumuambia mume unaenda kukopa kwa ndugu wakati mume zake zinaishia kwa wengine!
Natamani niendelea lakini nachoka kuandika kwakua dada zangu nanyie wagumu kuelewa. Iko hivi mwanaume ukimzoesha huombi basi hatakua akitoa, kama kila kitu unafanya mwenyewe anakuona kama unamtenga, anakuona kama huna shukurani na wala humjali anaweza hata kudhani kuna mwanaume mwingine anakuhudumia au una kiburi. Hivyo omba, na kama hakupi omba tena na kama hakupi omba tena, tena kama ni mume wako omba na tena na kama ni mchepuko soma upepo kama heleweki kimbia!


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.