Diamond Platnumz akamatiki youtube, afikisha watazamaji milioni 900


 Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amefikisha watu milioni 903 waliotazama kazi zake mbalimbali katika mtandao wa Youtube hadi leo Jumatatu Machi 23, 2020 saa 7 mchana.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul alijiunga na mtandao huo Juni 12, 2011 na amepata watazamaji wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.

Diamond katika akaunti yake ya Youtube tayari ana wafusi 3.28 million akiwa msanii wakwanza Tanzania kuwa na wafuasi wengi katika mtandao huo.

Baadhi ya matukio anayoyaweka katika mtandao huo ni shoo anazozifanya ndani na nje ya nchi, matangazo ya bidhaa na huduma, matukio ya kijamii anayoshiriki na utayarishaji wa video za nyimbo zake.

Mbali na hilo pia amekuwa akiweka picha mnato anazopiga akiwa peke yake au na watu wake wa karibu, wakiwemo baadhi ya mashabiki zake wanaocheza nyimbo zake mbalimbali.

Mathalani wimbo  Yope aliyoshirikishwa na msanii Innos’ B wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umetazamwa mara milioni 73 ndani ya miezi sita, kuwa wimbo unaoongoza kwa kutazamwa zaidi.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.