Riwaya:: NDOA NDOANO Sehemu ya:: 19




Riwaya:: NDOA NDOANO

Sehemu ya:: 19


Endelea.........

Maposo alionyesha kumhitaji Mwamvita kwa hali yoyote ile, Alishinikiza watu wake kuvamia kijiji ambacho anaishi ili aweze kumkamata. Hakika watu walisikitika sana kiasi kwamba waliomba msamaha kwa mtu ambae haombeki kabisa, Maposo ni mtu katili sana ambae hulazimisha kutaka kile akitakacho. Katika msururu huo na yeye alikuwepo akimhitaji Mwamvita ajisalimishe la sivyo wanamchinja mtu huyo waliomshika hadharani. Mwamvita akiwa mbali sana aliweza kukamatwa na walinzi wke waliomuomba kuwa asijitoe kabisa kwenda pale kwa kuwa yeye ni mtu muhimu sana kwao. 'Mwamvita usipojitokeza basi fahamu watu hawa wanakufa wote nawachinja, jamani wanakijiji nafanya hivi kwa kuwa Mwamvita alikuwa mke wangu sasa kanikimbia na pia kasababisha ndani ya kijiji hiki mmemuua baba yangu tena kwa kumchinja kabisa na kuniletea kichwa nyumbani, haki ya nani nitarejesha maumivu hayo.
Alizidi kuongea mengi lakini bila ya yeye kufahamu kiwa Mumwa yupo karibu na yeye kwa kumlenga shabaha ya mshale akiwa mbali na yeye. Mwamvita kwa upande wake, aliwaomba wale vijana wake ambao ana waamini wahakikishe kuwa watoto wadodgo na akina Mama wanawekwa mahali salama kwanza. Nfipo wakafanya kama walivyoelekezwa. Wakati huo bado mateso yakiendelea alijitokeza Mzee Mashauri baba wa Mwamvita. Alijitokeza mbele ya Maposo na kumueleza jambo 'Haaaa haaa kumbe weee mzee uko huku na wewe pia mwanao ukamtorosha sasa leo nawaibisha mbele ya hawa watu' Ajabu Mzee Makalani alianza kupiga makofi ambayo yalimsitua kila mmoja, baada ya kuona wapo kimya basi akaanza kusema jambo ' Sasa muda umefika, wanakijiji huyu mtu mbele yenu anaitwa Maposo mtoto wa mbei yani yule mzee tuliyemchinja kwa upuuzi wake wa kuwabaka mabinti wadogo pindi anavyokuja hapa, pia huyu ni mtu mkatili sana hapa alipo ni wa kupigwa mawe na afe kabisa'. Maposo alikasirika kabisa akanza kusema ' vijana wangu mnalala nini wakato natukanwa na mtu ninayemtunza mm mwenyewe, alipojaribu mlinzi wake kumkamata Mzee Mashauri alitundikwa mshale wa shingoni na kupoteza maisha kabisa. Maposo alishtuka ilimbidi arudi nyuma kwanza. Akaenda mwingine kumkamata lakini mshale ulikuja kwa kasi hadi shinhoni mwake na kupoteza maisha.'  Maposo alihofia watu wake kuisha, akaamuru warudi nyuma na kumuacha Binti waliomshika, hakika wliwazomea na kuwapongeza mashujaa hasa Mumwa. Basi waliwakusanya maiti na kuwazika. Katika makaburi.
Ndani ya kijiji atokeako Maposo, wananchi na wao walichachamaa baada ya kudhulumiwa sana mali zao kipindi cha mavuno. Hii yote ilikuwa baada ya kupata taarifa ya kufa kwa Mbei na kukiona kichwa chake na wakajua kuwa hakuwa na nguvu yoyote zaidi ya walinzi ambao wametokana na wao. Basi mmoja wa vijana alikuja kutoka kwa Mwamvita na kuja kuwapa taarifa ' jamani wanakijiji Maposo kakimbia kule anarudi sasa hana nguvu yoyote kama mnataka kuishi vyema basi hakikisha kila kijana ambae unamfahamu kuwa ni mlinzi wa Maposo waambieni wazazi wao kuwaeleza vijana wao wafanye jambo ili kijiji kiwe mikononi mwetu jamani.' Taarifa hiyo haikuwa ngumu kuitikiwa kwani kila mmoja kachoka sana na mambo wanayofanyiwa hapo.
Maposo alikimbia na kurudi nyumbani kwake, aliamua kukusanya vijana wengine mitaani ambao wamefundishwa kumsaliti baada ya kuchaguliwa, hivyo maposo alikuwa anajichimbia kaburi mwenyewe. Alitoa mafunzo yake yote kwa vijana ili siku zijazo wakarufishe majeshi kule ambako walifanyiwa unyama.
Baada ya kuhakikisha kuwa wameiva. Akawaruhusu wakasalimie wzazi baada ya mafunzo kuidha ili watakaporudi, hilo lilikuwa kama kosa kwani vijana hao waliungana kwa pamoja na kuhitaji kumgeuka hata kabla hawajaanza kwenda huko....

Itaendeleaa........





(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.