Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA MWISHO 20





Riwaya:: NDOA NDOANO

SEHEMU YA MWISHO 20

Endelea...................

Baada ya kuhakikisha kuwa vijana wamekuwa tayari basi waliruhusiwa kwenda majumbani ili wakirudi waweze kufanya kazi ya kuwafuata wale watu wa Mwamvita pamoja na Mumwa. Vijana walirudi majumbani lakini kumbe wazazi wao walikuwa na lengo lao.
Hawakutaka kabisa vijana hao waweze kuwasaliti watu wasiokuwa na hatia, ni bora wao wakawasaidia na kumuangusha Maposo ambae alikuwa anaendesha mambo yake bila ya kuangalia haki ya mtu wala nini.
Mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la bwana MAPUA Aliweza kuwaomba vijana hao ambao walitoka katika mazoezi ya muda mrefu aweze kuongea nao na awaeleze mambo gani ambayo hawakuwa nayo vichwani mwao. Kweli vijana walijitahidi kuitana kila mmoja na wakakutana.
Waliendelea kumsubiri mzee Mapua mahali ambapo walielekezana kuwa wakutane kwa ajili ya mazungumzo. Hatimae Mzee Mapua anafika akiwa ananyemelea kwani haikutakiwa watu wa Maposo afahamu nini wanafanya. 'Haya vijana naomba mnielewe kwa hili jambo vijana, nadhani mnamfahamu Maposo'.
Kila mmoja aliitikia, idadi yao ilikuwa inakaribia watu kama thelathini, vijana ambao wametengenezwa vyema katika swala la upiganaji wa mapanga. ' Sasa kama mlikuwa hamfahamu Maposo na baba yake walishiriki kumuua mzee Moshi baba yake Mumwa, Maposo ndie anaywsababisha matatizo mengi hapa kijijini. Sasa nyinyi kama vijana tunatakiwa muwe makini sana tunatakiwa kumsaliti tumuue ili uongozi ubaki kwetu'.
Vijana walikubali kwa hayo maneno ambayo walikuwa wanaelekezwa na mzee Mapua. Ghafla waliona kwa mbali taa zikiongezeka, zikiwa zinakuja maeneo hayo. Lakini walichoshangaa kuwa baadhi ya wanakijiji wakija pale na kutoa msaada wa udhauri, ndipo mzee mapua akasema.
'Mkiona watu kama hawa wanaacha usingizi wao na kuja kutoa ushauri basi ni jambo muhimu sana.' Baada ya hapo walitawanyika na kuondoka. Kuelekea majumbani kwao.
Upande wa Mwamvita na yeye tayari hakutaka kumuacha kabisa Maposo aendelee kuishi. Usiku huohuo alijiandaa vyema ili asubuhi yeye na Mumwa waende kuutawanya utawala wa Maposo. Kabla hajafanya lolote, mumwa aliingia ndani humo na kumkumbatia mke wake.
Mwamvita alishajua kuwa kidume anahitaji nini ' Mume wangu, najua hujawahi nigusa tangu unioe nfio maana upobkaribu sasa uwanja ni wako kabla hatujaenda vitani kesho tuwe tayari tumelifanyia haki pendo letu na ndoa yetu.
Basi mke na mume waliweza kufurahi vilivyo na wakafurahi kuliko kifani, Asubuhi na mapema sana aliwaita watu wake na kuwaeleza kuwa wao wanaenda kupambana na Maposo, alafu wao waje kwa nyuma kumalizia vijana watakao kuwa wabisi kutaka kuelewa.
Kweli walisafiri wawili hao hadi kingo za kijiji cha Maposo muonevu. Mumwa alikuwa Mtaalamu sana kwa Utupaji wa mishale. Ukweli Mumwa alisogea na kumueleza Mwamvita ' Sasa mimi nachokoza vita kisha utanifuata nyuma'.
Aliutupa mshale wake hadi ulipomkita barabara mlinzi mmoja. Ndipo waliposhtuka wengine na mmoja wao akapiga yowe 'Tumevamiwaaaaaaa......' alikimbilia kwenye kengele ya kuita watu wale ambao walishafundishwa na maposo.
Muuaji hawakumuona zaidi walishtukia mishale ambayo iliwanyoosha barabara. Upande wa Mwamvita alisonga kijijini na kuwakusanya haraka wanakijiji na kuwaeleza kuwa mambo tayati na wanahitaji msaada wao. Mzee mapua aliwaeleza vijana sasa kuwa kazi imeanza rasmi. Vijana hao walikimbilia kwa maposo.
Mpaka kufika masaa kadhaa watu wote walishapoteana hatimae akabaki maposo peke yake, huku akishangaa kawekwa kati japo na ubaunsa wake. Maposo hakuamini kama vijana wamemsaliti na sasa akabaki peke yake. Wanakijiji waliamua kumpa adhabu maposo ya kumpiga mawe mzimamzima mpaka kifo chake. Kwa kweli walifanya hivyo na wakamteketeza.
Mumwa na mwamvita walifurahi sana ndipo wakarudi hadi kule kijiji ambacho yeye ni malkia. Aliamua kumpaatia mzee aliyekuwa karibu sana na baba yake kuwa ni mfalme na yeye mama yake na mumwa  wakarudi hadi kijijini kwao. Wanakijiji furaha yao walimpa uongozi mumwa pamoja na Mwamvita waweze kuongoza.
Baada ya muda kutulia Walienda makaburi ya watu wasiokuwa na hatia kama rafiki yake Makame. Kisha hadi hapo wakawa wamekamilisha lile tatizo la uonevu kama Mumwa alivyomueleza mkwe wake zamani kuwa atahakikisha anamuondoa Mbei na Maposo.
Mwamvita alipata mimba na alibahatika kujifungua mtoto wa kike ambae walimpenda sana na wakahakikisha asiishi maisha ambayo Mwamvita alipitia......

         AHSANTE KWA KUWA PAMOJA NA MIMI

                       MUDHIHILI H MNALI

                  ★★★M W I S H O ★★★





(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.