RIWAYA:: NDOA NDOANO SEHEMU YA:: 18
RIWAYA:: NDOA NDOANO
SEHEMU YA:: 18
Endelea.........
Mipango ya kuweza kuvamia katika ngome ya kijiji cha Maposo yaliendelea katika hatua mbali mbali. Mwamvita aliutumia uongozi wake katika kukiokoa kijiji chao ambacho hakikutamanika kutokaba na mambo ya watu wabaya. Siku moja Mwamvita aliweza kuwaita wanakijiji wote ambao walikuwa wanaishi pale, lengo la kuwaita watu hao ni kuweza kuwaeleza jinsi hgani wanahitajika kupambana na watu wabaya ambao watakuwa wanatokea vijiji vya jirani. Hapakuwa na mtu ambae aliweza kumdharau kabisa Mwamvita kwani alikuwa ni mwanamke hodari pia shupavu hali hiyo ilitokana na swala la kupitia matatizo mengi sana katika maisha yake iliyompelekea kuona chungu maisha yake yote ya ndoa. Wanakijiji walifika tayari na kuweza kumsikiliza vyema kiongozi huyo. 'Wanakijiji kuna swala moja ambalo nalihitaji tuweze kushirikiana kwa makini, muda si mrefu tutaweza kuvamiwa hapa na kundi linalotokea kijiji cha jirani hivyo hatutaki kupokonywa milki yetu bali tunahitaji kuwapokonya wale wabaya kisha turudishe ardhi kwa wananchi wanyonge.' Wengi wao walibaki kuduwaa kwa kumsikiliza mwanamke huyo akiongea maneno yake wengi waliweza kumdharau kuwa yeye ni mwanamke na atabaki kuwa mwamke, mambo ya vita awaachie wanaume.lakini ilikuwa tofauti sana kwa Mwamvita. Mumwa alimuendea mwamvita na kuhitaji kuongea nae baada ya kuhisi kuwa hali imetulia kidogo ' mke wangu tumepitia mengi sana sasa sijajua mapenzi yetu tunayafaidi lini maana nadhani hali imekuwa sawa mpaka leo wewe ni Malkia hapa bila ya kutegemea.
Mwamvita alimuangalia Mpenzi wake wakati huo wakiwa maeneo ya porini wakitazama baadhi ya wanyama wa mwituni pamoja na ndege ambao walikuwa wakiimba na kuruka. Mazingira yaliwapendeza wawili haoa kuwa pamoja kwa nyakati zile. ' Mumwa nakuahidi kama nilivyojitahidi kutoamini maneno ya watu kuwa wewe hujafa basi leo hii nakuahidi utapata kila utakacho najua muda mrefu sana, na isitoshe tuna hali nzuri ya kuishi kidogo, Sasa twende ndani basi'. Basi walikimbizana, ndipo Mumwa Akambeba Mwamvita na akaondoka nae kuelekea kwenye kibanda chake cha kujihifadhi yeye kama malkia. Ghafla alikuja kijana mmoja ambae alikuwa ni mmoja wa Walinzi katika himaya ya CHIJUNI ambae ina simamiwa na Mwamvita ' Wewe kijana vipi kuna swala gani unakimbia hivyo?' ' Malkia ,Malkia Tumevamiwa kule kuna watu wamekamatwa'. ' Wamekamatwaaaaa?' 'Ndiooooo' Walikimbia wote kwa pamoja lakini Mumwa alishtuka kidogo akawaacha wao watangulie kisha yeye akapita njia nyingine. Kweli kumbe kuna kundi la Maposo lilifika na kukamata watoto kadhaa ambao walikuwa wanalia sana, waliwatishia kuwaua endapo kama Mwamvita hajajitokeza. Mwamvita alitakiwa kukamatwa ili arudishwe kwa Maposo kama Maposo alivyohitaji, pia maposo alimhitaji Mtu ambae aliyemuua baba yake, na kumpelekea kichwa. Maposo alikuwa na hasira sana ndio maana yeye akawa anahitaji kumkamata kwanza mwamvita.
Itaendelea......
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments: