Batuli afichua siri ushosti wake na Wema
MREMBO Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefichua siri kuhusu urafiki wake na muigizaji Wema Sepetu kuwa ulirudi muda mrefu ila watu hawakufahamu. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Batuli amesema yeye na Wema wameanza kuzungumza muda sana ila hawakuweka wazi urafiki wao hadi video iliposambaa ndiyo watu wameanza kuzungumza yao.
“Mimi na Wema tulishakaa na kumaliza tofauti zetu, tumeanza kuongea kitambo sana, sema watu wameshtuka baada ya kuona video tukiwa pamoja huko Instagram. Pia watu wajue kwamba kuna kipindi lazima muache maisha yaendelee kuwekeana vinyongo moyoni sio vizuri,” alisema Batuli.
Wawili hao walikuwa kwenye bifu kwa muda mrefu huku chanzo kikitajwa kuwa ni kutofautiana itikadi za kisiasa ingawa wenyewe hawajaweka wazi.
Stori: Memorise Richard
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: