WATANZANIA 200 HUAMBUKIZWA UKIMWI KILA SIKU
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Leonard Makombo, amesema kuwa zaidi ya watanzania 200 huambukizwa virusi vya ukimwi VVU kila siku hivyo kufanya idadi ya maambukizi kuwa 72,000 kwa mwaka.
Amesema kuwa takwimu zinaonesha vijana wenye umri wa kati ya mika 14 na 24 ndiyo wanaongoza kwa maambukizo, wakichukua asilimia 40 ya maambukizo mapya.
Amesema ” Kwa kuzingatia kwamba takriban watu 200 wanaambukizwa VVU kila siku, 80 ni kutoka kundi hilo la vijana”
Katika maadhimisho hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye viwanja vya Furahisha jiji Mwanza, ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali, upimaji wa hiari wa VVU na utoaji wa huduma za ushauri nasaha
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: