Tabia Nne za Mpenzi asiyekuwa na penzi la kweli
WIKI iliyopita tuliona baadhi ya dalili ambazo zinaweza kukupa mwelekeo wa kujua kama mpenzi huyo ameumbwa kwa ajili yako, ama la, lakini wiki hii tunaangazia na kuzijua walau dalili Nne za Mpenzi ambaye hana mapenzi ya dhati nawe.
Ifahamike kuwa hakuna asiyehitaji mapenzi ya kweli ingawa kuna wapenzi wanaothamini penzi wmenzi wake anapokuwa na pesa au kazi Fulani na baada ya hapo hujitoa katika mahusiano hayo hali ambayo huleta kwikwi katika mtima wa moyo wa anayefahamu kupenda.
1. Muongo
Hakuna asiyefahamu athari za mtu muongo katika jamii, vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika mapenzi uongo ni sumu mbaya na nidalili moja wapo ya kuonyesha kuwa mpenzi wako hana penzi la dhati nawe na huyo aweza kukuletea athari za kufikiri hapo baadae endapo hautakuwa makini nae.
Hivi karibuni nilikuwa mjini Mbeya nikipata chakula katika moja ya mgahawa uliopo mkabala na Posta, katika mgahawa huo nilikutana na vijana wawili na msichana mmoja wakiwa wanakula chakula ambapo kati ya kijana mmoja alionekana kuwa ni mpenzi mpya wa yule binti ambaye alisikika akisema kiwa ‘’ukija kwangu atakalia sofa ambazo hujawahi kuziona maishani’’ hali iliyonishtua na kuelewa mara moja kati ya tabia alizonazo kijana yule ambaye anaonekana ni mcha Mungu.
Hivi utajisikiaje Mpenzi wako akigundua kuwa ulikuwa ukimdanganya na hatimaye yeye akajua ukweli wa suala ulilokuwa ukimpiga fiksi? Lakini ushauri wangu si kumacha bali jaribu kumshauri kwa hekima na akiendelea na tabia hiyo ujue kuwa hana mapenzi ya kweli kwako.
2. Kupenda pesa
Ukiona mpenzi wako wa kike ama kiume anapenda sana kupata pesa kutoka kwako tambua ni moja ya dalili ambazo zinajieleza kuwa hana mpango nawe bali analazimika kuwa nawe kutokana na pesa ama kipato chako. Mpenzi wa namna hiyo ili kujihakikishia dalili hii siku moja akikuomba pesa hata kama ameziona mwambie kuwa huna, hapo yupo tayari kuvunja hata mahusiano kwasababu kitu muhimu kwake hajapata na wala wewe si muhimu tena kwake.
Nieleweke kuwa sisemi pesa ni mbaya katika mapenzi, la hasha bali pesa na mapenzi ni sawa na trafiki na kondakta katika mambo Fulani yale………ya kuchafua mifuko kwenye nguo nyeupe……………na ni muhimu wapenzi mkapenda kupeana maarifa ya kufanya kazi halali ili kujipatia vipato kwa ajili ya kuepukana na hili.
3. Hajali kutokuwa jirani na wewe.
Mpenzi anaye kupenda muda mwingi hutamani kuwa nawe karibu na inapotokea hamjaonana hata masaa sita au matatu hujisikia shida ambapo kwa wengine hufikia kupiga simu na ukimuuliza anasemaje atakuuliza maswali yaliyoshonana kama ushanga mara upo wapi? Umekula? Na upo na nani? Na maswali mengi ya namna hiyo ili mradi moyo wake utulie.
Endapo Mpenzi wako mkiwa mbali naye kwa muda wa masaa mengi na yeye akaonyesha kuwa hakukosa chochote kutokuwa nawe karibu ama kuwasiliana nawe basi ujue kuwa mpenzi huyo ni kimeo yaani hana mapenzi ya dhati kwako.
4. Anapenda kukuudhi
Dalili ya Nne ya mpenzi asiyekuwa na mapenzi ya dhati nawe ni yule anayependa kukuudhi mara kwa mara kana kwamba anatafuta sababu ya kuachana nawe lakini anashindwa kutamka bayana kuwa haitaji tena kuwa nawe.
Maudhi hayana budi kutokea pale inapobidi kwa bahati mbaya sana na si kwa makusudi, lakini wapo wapenzi wanaowaudhi wenzao kwa makusudi huku wakiendelea kusisitiza maudhi hayo kama utani na kujua kwa makusudi kuwa anamuumiza mwenzi wake bila kuomba msamaha. Ingawa kuomba msamaha ni kipaji na hasa katika mfumo dume ambao unaonesha kuwa mwanaume anapoomba msamaha basi ujue katumia njia nyingi za kumaliza tatizo hilo zimeshindikana hivyo kaomba msamaha kwa kulazimika sana na kwa siri.
Mpenzi msomaji wa safu hii, baada ya kuona dalili hizo za mpenzi asiyemwaminifu kwako, je wajua kuwa tendo la ndoa lina faida kubwa katika afya yako? wiki ijayo jiandae kujua faida nane za kufanya ngono kiafya.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: