SHILOLE ATANGAZA VITA NA UNENE

 Mwanamama kutoka Bongo Flevani ambaye ni Mkurugenzi wa Mgahawa wa Shishi Food, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ametangaza vita rasmi na unene.

Baada ya kusemwa sana mitandaoni na mitaani kuwa amenenepeana kupita kiasi na kupoteza mvuto, sasa Shilole ameamua kuingia ‘gym’ ili kupunguza mwili.

Shilole amechukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wasanii wenzake pamoja na mashabiki wake kutopendezwa na unene wake kwani unamfanya kuonekana kituko kwenye jamii.

“Shishi Baby (Shilole) siku hizi amekuwa mnene sana kiasi ambacho huwezi kudhani kama ni msanii, bali ni mama muuza vitum bua,” ilisomeka sehemu ya maoni ya mashabiki wa Shilole mara baada ya kutupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, baada ya kuanza mazoezi magumu ya kukata mwili akiwa chini ya usimamizi za msanii Zola D, watu wengi wamempongeza Shilole kwa hatua hiyo.

Baadhi ya mashabiki wanasema wanasubiri kumuona Shilole akikondeana, lakini asijikondesha kupita kiasi kama ilivyokuwa kwa mwigizaji mwenzake, Wema Isaac Sepetu


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.