KIJANA AMUUA MPENZI WAKE KISHA NAYE KUJIUA

KIJANA aliyetambulika kwa jina moja la Paschal (24) anadaiwa kumuua Rosemary Gallus (34) kwa kumchoma kisu kisha na yeye kujichoma kisu kifuani na tumboni na kufa.



Chanzo cha kufanya hivyo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi uliopelekea ugomvi kati yao huku Paschal akimtuhumu Rosemary kutokuwa mwaminifu katika mapenzi yao.



Wawili hao wamekutwa wamefariki (nyumbani kwa mwanamke) Gongo la Mboto, Dar es Salaam, huku mtoto wao (1) akiwa pembeni ya maiti za wazazi wake na akiwa amejeruhiwa kidogo.



Wazazi wa Rosemary wamesema Paschal amezaa na mtoto wao lakini waliachana kutokana na ukorofi wa kijana huyo na siku ya tukio alikwenda kwa mwanamke kusuluhisha lakini yakatokea hayo yaliyotokea


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.