Isha Mashauzi: Jimbo Lipo Wazi, Natafuta Mchumba
Isha Mashauzi akiwa ndani ya studio za +255 Global Radio akifanya mahojiano na kipindi cha Jahazi La Pwani.
Muimbaji huyo alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Jahazi la Pwani kinachorushwa na 255 Global Radio.
“Jimbo liko wazi, nimewahi kuolewa mara mbili mume wangu wa kwanza nimezaa naye mtoto mmoja, na mume wangu wapili hatukubahatika kupata naye mtoto, waume zangu wote tulihitilafiana kila mmoja akaenda kutengeneza maisha yake.
“Sasa hivi niko mwenyewe natafuta mtu.” Alijibu Aisha baada ya kuulizwa swali kuwa kumekuwa na tetesi za yeye kuolewa na waume wa watu.
MUIMBAJI wa muziki wa Taarabu nchini Isha Mashauzi akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji wa kipindi cha Jahazi la Pwani, Odo Aisha.
Aidha, aliendelea kwa kusema.“Wanitafute, nahitaji nipate mtu atakayenienzi, atakayenipenda, sijali kuhusu muonekano wake, lakini tu awe na kipato cha kuweza kunisaidia na familia yangu. Nataka kweli sio kwamba natania, mimi ni mzuri wa kila kitu, wanitafute,” alisisitza Isha.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: