Harmonize ampongeza Burna Boy kushinda tuzo


Msanii kutoka konde Music Worldwide, Harmonize amempongeza Burna Boy kwa kushinda tuzo ya MTV EMA usiku wa kuamkia jana.

Harmonize ambaye alikua kwenye kipengele kimoja na staa huyo kutoka Nigeria ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza, kuwashukuru waandaaji wa tuzo hizo na kuwashukuru mashabiki kwa kumpigia kura licha ya kutotosheleza kushinda tuzo hiyo.

Harmonize ndiye alikuwa msanii Afrika Mashariki kutajwa kwenye kipengele cha Best African Act ambacho alikuwa anachuana na wakali wengine kama Burna Boy, Nasty C, Teni, PrinceKaybee pamoja na Toofan.

Ikumbukwe wakali wengine kutoka Afrika Mashariki, Alikiba, Sauti Sol na Diamond Platnumz wamewahi kuwa nominated na kushinda tuzo hiyo.

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.