Nimeazimia / nimekusudia siku nikifika DAR ningependa kufika maeneo haya yafuatayo

Salamu sana.

Jamani Mimi kijana wa kiume ambaye nimebahatika kuzaliwa katika mkoa wa TANGA na sasa kimaisha nipo mkoani MBEYA. Nimebahatika kutembea mikoa mingi ya TANZANIA ikiwemo MWANZA, SHINYANGA, DODOMA, SINGIDA, IRINGA, MOROGORO, PWANI, MOSHI, ARUSHA nk.


Lakini sijawahi kufika mkoa wa DAR. Dar Ni mkoa ambao bila shaka ndipo Mambo mengi yanayoiwakilisha Tanzania hupatikana.

Nimeazimia / nimekusudia siku nikifika DAR ningependa kufika maeneo haya yafuatayo.

1. Uwanja wa taifa wa Mpira wa miguu.
2. Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
3. Daraja la kigamboni
4. Kariakoo sokoni
5. Uwanja wa fisi
6. Mtaa wa MASAKI huko kwa matajiri eti.
7. Lugalo (kambi ya jeshi)
8. Makumbusho
9. Nitembee kwenye hizo fly over
10. Nitembee kwenye hizo njia za mwendokasi. (Nioshe nyota)
11. Nipite na huko kunapoitwa central POLICE nikamsalimie MAMBOSASA na kamanda SIRO.

12. Naskia nako Kuna hayo makumbi ya starehe sijui nini na Nini uko. Na kadhalika na kadhalika.

Jamani Mimi sioni haya kuitwa mshamba.

Ukweli Ni mzuri

Naomba nikija mnishike mkono na kunionesha jiji.

Mzee wa kasumba.

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.