Hili ni funzo kubwa katika Mapenzi, tujaribu kuchukua hatua ya busara na ya kiutuzima!
Chanzo kubwa cha mahusiano yangu kuvunjika na kipenzi changu ni tatizo letu wanaume wengi kwa sasa, nilipendana naye kipindi nipo chuo, sikuwa na stable economy kabisa.. akapata vishawishi na hapo tumeshakaa pamoja miaka kama mi tatu (Though silaumu kwa kuwa ameenda kwa mwingine kwa sababu hata sisi wanaume tungejaribu kuvaa viatu vyao tukawa wanawake tusingeweza vumilia wanaume wasio na pesa).
Nimekaa na kutafakari ila nimeona bado moyo wangu uko kwake, hata kama kawa na wanaume wangapi still i love her, ninachofanya ni ishu moja, nipo najipanga kiuchumi niwe na flow kubwa ya Pesa, kisha nimchukue au nimyanganye kwa mshikaji aloko naye sasa.
Wanaume wenzangu tukiwa hatuna Pesa sio kwamba hatupendwi.. tunapendwa sana tu ila tatizo ni mwanamke anakosa security ya future yake kwako, anaweza kuwa na wewe kwa sababu ya upendo ila uvumilivu wao unawafikaga mwisho, Tafadhali tusiwalaumu hawa viumbe wanapotuacha kisa hatuna pesa.. wamevumilia mpaka wakafika mwisho.
Nadhani kila mtu ni shahidi wa kupendwa hata wakati ule hana kitu, je hata kama huyo mwanamke alikuacha siku ukipata kitu huoni kwamba ni chaguo sahihi?
Mapenzi ya dhati ili yadumu pesa kidogo inabidi iwepo!
Pesa ni muhimu ila Upendo wa dhati muhimu zaidi
Binafsi nitamrudisha wa kwangu,,soon nitaleta mrejesho tuombeane tu SHIMO LITEME!
Khan
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: