SIMULIZI : Sitaisahau Tanga (sehemu ya 11)
Nikawa sijielewi kabisa nikajihisi akili yangu kama
ikiniruka hivi, nikazidi kuwaza na kuwazua bila ya kupata jibu la maana.
Mara gafla giza nene likatanda pale chumbani, nikazidi
kukosa amani moyoni mwangu, mara kuna kitu kikaja na kunikaba kooni nikaanza
kutapatapa na kuhangaika kama kwa dakika kadhaa ile hali ikatoweka na mwanga
ukarudi tena mule ndani. Mara yule binti akanipigia simu,
BINTI: Unajisikiaje mpenzi?
MIMI: Najisikiaje nini wakati umeniumiza wewe?
BINTI: Pole mpenzi.
MIMI: (Nikamjibu kwa ukali), pole yako haisaidii bhana.
BINTI: Kwahiyo unanikaripia eeh!
MIMI: Hapana sijakukaripia bhana.
Akakata simu, nikazidi kupatwa na hasira kila nikiwaangalia
wale ndugu zangu pale chini nakosa raha na pia nazidi kukosa amani.
Nikakaa nikajifikiria nikachukua simu na kumpigia yule binti
ila hakupokea baada ya muda akanipigia yeye,
BINTI: Eeh unasemaje?
MIMI: Tafadhari kuwa na huruma japo kidogo jamani, ona umetufungia
humu toka jana na hatujala chochote.
BINTI: Kwahiyo shida yako ni chakula tu?
MIMI: Hapana sio chakula tu ila nataka uwazindue hawa watu.
BINTI: (Akacheka sana), chakula utakipata ila kuwazindua hao
sio kazi yangu.
MIMI: Nihurumie tafadhari.
BINTI: Fumba macho.
MIMI: (Nikafumba kama alivyoniamuru)
BINTI: Haya fumbua macho yako.
Halafu akakata simu, Mungu wangu sikuamini kabisa
nilichokiona mbele yangu, kwani nilikuwa chumbani ila cha kushangaza chumbani
mule kulikuwa na shughuli mbalimbali zikiendelea, mara kuna watu wakiuza
chakula na wengine wakiuza vinywaji tena walikuwa makini na shughuli zao tu,
hofu kubwa ikanitanda moyoni, mara nikapokea sms,
"nenda ukajinunulie chakula sasa"
Nikahisi kupagawa kabisa na wala sikujielewa na sikuweza
kuwasogelea kabisa, nilijihisi kuchanganyikiwa kwakweli, mara simu yangu
ikaita,
BINTI: Unaogopa nini sasa?
MIMI: Aaah sijui hata naogopa nini?
BINTI: (Akacheka), wewe si umetaka chakula jamani,
nimekusaidia kukuletea wauzaji nakushangaa huendi kununua, kwanini sasa?
MIMI: Aaah mmmh kwani aah sikuelewi.
BINTI: Inamaana hutaki chakula tena? Niwaondoe?
MIMI: Mmmh eeeh nini sijui kitu.
BINTI: (Akacheka sana), ukome kuchukua mizigo usiyoweza
kubeba.
Akakata simu, ikawa ni kitendo cha kufumba na kufumbua wale
wauzaji sikuwaona tena.
Nikashikwa na bumbuwazi tu hata sikujielewa.
Nikiwa mule ndani sijielewi chochote nikasikia watu wawili
wakiongea pale nje, sauti ya mmoja wao niliitambua ni mke wa rafiki yangu.
Wakaanza kugonga mlango, nami nikaenda na kuwafungulia nao wakapitiliza moja
kwa moja ndani.
Yule mke wa rafiki yangu alikimbilia moja kwa moja pale
chini alipolala mumewe huku akimtingishatingisha aamke ila kama kawaida
hakuamka, yule mwingine ambaye alikuwa mdogo wa mke wa rafiki yangu alikuwa
pembeni akiangalia tu na wala hakusema chochote.
Mara simu yangu ikaita,
BINTI: Hao nao wamefata nini?
MIMI: Sijui wamefata nini.
BINTI: Mpe simu mmoja nizungumze naye.
Nikataka kumpa yule mke wa rafiki yangu ile simu lakini ile
anataka kuichukua mdogo wake akamkataza na kumwambia kuwa asiichukue ile simu.
Mimi nikabaki nawashangaa tu, mara yule mdogo mtu akaniamuru niikate ile simu
nami nikafanya hivyo. Akamgeukia dada yake na kumwambia kuwa atoe ubani kwenye
mkoba na akaombe moto nje, ikabidi nimuulize,
MIMI: Samahani mdogo wangu mbona unataka kuniletea mambo ya
mashetani humu ndani?
Nikaona kanigeukia na sura yote imebadilika, nikaanza
kupatwa na uoga.
Akaniambia jambo moja tu kuwa inapaswa nikubali kumtoa ndugu
yangu mmoja kama kafara ili niokoe maisha ya wale wengine au wote wapotee,
akaniambia kuwa nichague kati ya wale watatu ambao ni mama, kaka na dada.
Kwakweli nguvu ziliniishia nikajihisi kujisaidia haja kubwa
na ndogo kwa wakati mmoja kwani bado sikujua niamue lipi kumtoa ndugu yangu
mmoja kama kafara au wote wapotee, na je ndugu huyo nitamtoa nani kati ya mama,
kaka na dada bado sikupata jibu kwakweli.
ITAENDELEA
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: