SIMULIZI : Sitaisahau Tanga (sehemu ya 10)



Nikapatwa na hofu kubwa moyoni, sikuwa na furaha kwakweli. Nikahisi mama na dada wakizidi kusogelea mlango wangu, wakaanza kubisha hodi huku wakiniita jina langu sikutamani kuitika kwakweli nilijiona na mtu mwenye mkosi pale ndani, mama alizidi kubisa kuwa nifungue na nisipofanya hivyo atapiga kelele ili watu waje kubomoa mlango, aliposema hivyo nikahisi kupagawa kabisa kwani yule binti alinambia kuwa nikipiga kelele basi atauondoa kabisa uhai wa wale waliopoteza fahamu mule ndani, nilipofikiria hayo nikaenda mlangoni na kuwafungulia mlango. Baada ya kuwafungulia tu wakaingia moja kwa moja ndani nami nikaurudishia mlango,

MAMA: Mungu wangu, umemfanya nini kaka yako? (huku akimfata pale chini na kumtingishatingisha).
MIMI: (Huku nikitetemeka), hapana mama sijamfanya chochote.
DADA: Hivi una akili wewe? Yani wenzio wanatapatapa humu ndani na wewe umetulia kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea.
MIMI: Dada sielewi kitu.
Mama akiendelea kumwamsha kaka pale chini huku akijisemea,
"jamani mwanangu, sijui amekufa".
Mama ndio alikuwa hajielewi kabisa bora hata ya dada, mara yule binti akanipigia simu,
BINTI: Mwambie mama asilie.
MIMI: Usinichanganye ujue! Wewe ndio umesababisha yote haya.
BINTI: Mpe simu mama nimueleweshe tafadhari.
MIMI: Hapana, naogopa nae utamfanya kama hawa.
BINTI: Unampenda mama yako?
MIMI: Ndio nampenda.
BINTI: Ok mpe simu niongee naye.
Nikiwa bado sina maamuzi sahihi nikawa nimeganda na ile simu sikioni, dada akauliza
DADA: Kwani nani huyo?
MIMI: Eti anataka kuongea na mama.
DADA: Mpe basi mama aongee naye.
Nikampa mama simu, naye akaweka sikioni akiwa kakaa pale chini nikamwonga akiangukia pale pale, dada akapiga ukelele wa ajabu huku akimwita mama "mama mama mamaaaa".
Ilikuwa ni kitendo cha gafla dada nae akaichukua ile simu na kuiweka sikioni nahisi alitaka kujua ni nani huyo aliyeongea na mama, kufumba na kufumbua nae akawa chini akitapatapa.
Nilizidi kuchanganyikiwa kwakweli, na mimi nikachukua ile simu na kuiweka sikioni labda na mimi kinipate kilichowapata wenzangu ili nisiwe na ufahamu tena, ila nilipoiweka sikioni nikimsikia yule binti wa kitanga akicheka sana,
MIMI: Umewafanya nini ndugu zangu?
BINTI: Unataka kujua nilichowafanya?
MIMI: Ndio niambie umewafanya nini?
BINTI: Haya tazama hapo chini.
Halafua akakata simu, kuangalia pale chini hakuwepo mtu yeyote, wote walitoweka. Nikapagawa hakuna mfano nikahisi kurukwa na akili mule ndani, nikataka kwenda nje na kukimbia, simu ikaita tena,
BINTI: Usithubutu kwenda popote kama bado unawapenda ndugu zako.
MIMI: Unajua sikuelewi wewe? Yani sikuelewi kabisa, unamaana gani kunifanyia mambo haya?
BINTI: (Akacheka sana), maana yangu utaijua tu ila Kama unawapenda ndugu zako hawa, usiende popote pale.
Akakata simu, nikazidi kurukwa na akili mule ndani.
Usiku ukawa umeingia na masaa nayo yakizidi kuyoyoma. Ikawa saa sita usiku mara simu yangu ikaita kuangalia imeandikwa shemeji1, kumbe ni mke wa kaka ananipigia maana yeye ndiye nilimsave shemeji1.
MKE WA KAKA: Shemeji, kaka yako alisema anakuja huko, vipi mbona hajarudi hadi sasa?
MIMI: Aaah mmh shemeji kulikuwa na tatizo kidogo ila atarudi tu.
MKE WA KAKA: Atarudi muda gani jamani shemeji, ujue hii ni saa sita jamani.
MIMI: Atarudi tu.
MKE WA KAKA: Nakuja hukohuko, hata msinitanie kwa kufichiana maovu.
MIMI: Usije bhana atarudi.
MKE WA KAKA: Nakuja.
Akakata simu, baada ya muda kidogo nikasikia muungurumo wa boda boda nje. Mara mlango ukaanza kugongwa kuwa nimfungulie. Sikuwa na jinsi nikamfungulia,
MKE WA KAKA: Eeh mume wangu yupo wapi? Nilijua tu kuna mambo mnanificha nyie bora nimekuja kuyashuhudia mwenyewe.
MIMI: Hapana shemeji sio hivyo unavyofikiria.
MKE WA KAKA: Wee usinitanie kabisa, niambie ukweli. Yani unamwona kaka yako akitenda ufirauni halafu unajifanya kumtetea.
Mara simu yangu ikaita,
BINTI: Anataka nini nae huyo?
MIMI: Anamtaka mumewe.
BINTI: Mpe simu niongee naye.
MIMI: Hapana siwezi kukupa uongee naye.
Mara mke wa kaka akadakia,
MKE WA KAKA: Kwani nani huyo?
MIMI: Eti anataka kuongea na wewe.
MKE WA KAKA: Sasa si unipe niongee nae jamani.
MIMI: Hapana shemeji, siwezi kukuruhusu uongee naye.
Shemeji akanipora ile simu na kuiweka sikioni ili aongee nae, muda huo huo nae akaanguka chini na kutapatapa, ikawa sasa kama yale matukio nimeshayazoea.
Yule binti akanipigia tena simu,
BINTI: Unaupenda mchezo wangu?
MIMI: Aah usinichanganye bhana.
BINTI: (Akacheka sana), angalia tena chini.
Akakata simu, kuangalia akawa amewarudisha wale watu wote, nikazidi kutetemeka hata nisijue cha kufanya.
Ilikuwa hakuna kulala wala kula wala kufanya chochote.
Kulipokucha nikashtuliwa na simu ya mke wa rafiki yangu.
SHEMEJI: Vipi shemeji jana hamkufanikiwa?
MIMI: Kumbe alikwambia jamaa, hatukufanikiwa.
Mara akakata simu, nikasikia simu ya rafiki yangu ikiita kwa mara ya kwanza toka mfukoni mwake. Nikaichukua ile simu alikuwa ni yule yule shemeji.
SHEMEJI: Nasikia kuna matatizo huko.
MIMI: Aaah hapana, kwani nani kakwambia?
SHEMEJI: Nina mdogo wangu ana marhani ndio kasema.
MIMI: Aaah kakudanganya huyo.
SHEMEJI: Unajua kwanini nimekata ile simu yako na kupiga huku?
MIMI: Kwanini?
SHEMEJI: Ngoja tuje tutakwambia.
MIMI: Tafadhari msije jamani sitaki matatizo mengine.
Akakata simu, nikiwa bado ni mtu mwenye mawazo, mara yule binti akapiga simu yangu.
BINTI: Umenikera sana, nani kakutuma upokee simu nyingine?
MIMI: Jamani kwani na hilo siruhusiwi?
BINTI: Ngoja nikuonyeshe tena.
Akakata simu, nikawa nimeshikwa na bumbuwazi kuwa yule binti anataka kunionyesha mbwembwe gani hizo tena


Itaendelea tena kesho.....
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.