KUWA NA UHURU WA KUMCHAGUA UMTAKAE


Sifa moja ya kuwa na Uhuru wa kuishi ni kuishi maisha unayoyaweza,hapa utakuwa mtu mwenye tabasamu na furaha maishani mwako,,,kumbuka kuwa hata mume,mke au mpenzi utakae amua kuishi nae au kuwa nae,,mchukue mchague yule unaeamini ndiye mmiliki wa moyo wako na hisia zako na si yule anaemiliki mihemko ya tamaa zako,,
Kulazimisha maisha usiyoyaweza ni sawa na kujichimbia kaburi mwenyewe,,ndo maana hata utapokuwa na mume,mke au mpenz ambae umejilazimisha tu kuwa nae au kuishi nae kwasababu tu ya vitu fulani,,ikiwa si chaguo la moyo wako,basi tarajia kuwa mpishi wa maumivu na machozi kila iitwayo leo,,
Kuwa mkweli wa moyo na tabia,,hii pia itakufanya hata kama wewe ni fukara,,utaonekana tajira kwasababu moyo wako una utajiri wa UPENDO,,hata kama mke,mume au mpenzi ataonekana hafai kwa wengine lakini kwako atakuwa mume,mke au mpenzi bora kwasababu ndie aliyepo moyoni mwako.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.