Hadithi ya Kusisimua | Kwaheri Prosper wangu....


Nikiwa nasoma chuo kikuu jijini Dar mwaka wa tatu, kuna vitu vilinitatiza sana mimi kama mwanamke niliyekamilika, irene niljiuliza sana. Tangu kuzaliwa mpka umri wa chuo kikuu sikuwahi kuwa na mwanaume, nilikuwa mzuri tu na wanaume wengi walinitaka ila nilikataa nikiwa na nia ya kumpata nimpendaye nikiwa nishamaliza chuo na kuwa na kazi yangu. Nilisikia wasichana wengi pale chuoni wakilalamika kusalitiwa na wengine kushindwa hata mitihani kisa mapenzi! niliwashangaa sana na niliwaona washamba sana. Nilipenda siasa kiasi hivo nikafungua akaunti Facebook ili kufuatilia wanasiasa na habari mbalimbali za siasa kwani ndoto yangu ilikuwa niwe mwanasiasa maarufu duniani . Katika pitapita za matandaoni facebook niliona sura moja ya mwanaume, jina lake 'Prosper. Kimuonekano alikuwa maridadi sana na alionekana mtanashati niliamua kuangalia post zake, kiukweli kila picha yake ilikuwa nzuri huku akiwa kaandika maneno km si ya kuelimisha basi ya kutia moyo na kufurahisha.
Kadri nilivoona picha zake nilihisi raha Fulani moyoni hivo nikamtumia ombi la urafiki yaani friend request , zilipita siku 3 bila kupokelewa, na siku ya 4 alilipokea ombi langu tukawa marafiki. Kadri siku zilivozidi kwenda nilizidi pata hamasa ya kumuona na nilike picha yake kila alipo post. Nilihisi km kupenda niwe karibu nae vilee.
Kuna siku nilihisi kumpenda kabisa nikaamua kumtext ‘hi’ alijibu ‘hi too’, nilichat nae na kuuliza yuko wapi alijibu Iringa na kuniuliza niliko nikajibu Dar. Nilimuuliza wasoma au unafanya kazi maana unavopendeza akajibu ‘nasoma nahuu ni mwaka wa mwisho!’ Moyo wang ulilipuka kwa furaha, namimi nikamwambia niko mwaka wa mwisho alifurahi pia, tulizidi chat hapa na pale kila nilipopata nafasi na kila siku zilivo songa nilizidi kumpenda zaidi hisia zilizidi sana. Irene nilijitahidi sana kujizuia ila wapi, tofauti na wanaume wengine Prosper hakuwahi kuomba namba ya simu na wala kuzungumzia suala la mapenzi kitu kilichofanya nimuone mstaarabu sana. Niliweka profile, alinitext Irene umependeza sana na una uzuri wa asili’, moyo wangu ulikufa ganzi kwa kusoma tu ile message yake, kiukweli nilimpenda sana. Nilimueleza kuwa yeye ni Hb hakujali /hakutilia maanani sana, alisema tu nadanganya niliishiwa pozi Irene wa watu, ila alisisitiza kuwa mi ni mzuri na napendeza…. nilizidi kudata sana.
Miezi sasa ilipita huku nikwa sijielewi kabisa, niliwasikia baadhi ya mabinti wakisema kuwa kamwe usimuamini mtu wa face book au mitandao ya kijamii nilianza kukata tama ila nikajikuta najipa moyo kwani Prosper wangu kila siku alinitext huku akinitakia masomo mema kitu kilichonipa faraja kubwa, sasa hata kusoma nilipunguza nilipenda kuchat na Prosper kutokana na uchangamfu wake, moyoni niliumia kozi nilijua aliko lazima ana wasichana km si wapenzi basi anasoma nao na anaka na wanafaidi sana. Nilipata wivu sana.
Sasa likizo ilikuwa imefika, nikamueleza kuwa nitakuja iringa kwa ndugu zangu. Kiukweli nilimdanganya kwani sikuwa na ndg yeyote ila nilifikiri kuja kupanga guest ili tu nimuone. Niliomba kuonana nae nikija na akasema yupo tayari alionesha kufurahi sana na kusema kuwa atakuja kunisubiri stend hata kama naenda kwa watu. Nilitamani kumwambia ukweli ila udhaifu wa kike ulinishinda na hasa ukizingatia mila za kiafrika. Nakumbuka niliingia dukani na kununua nguo za kiume kwa kuangalia picha zake na kukadiria nguo ambazo zingemtosha, nilijaribu kuchagua rangi ambazo alipendelea, nikalipia mpaka wauzaji wa pale Kriakoo wakaona wivu, ‘dada hakika shemu wetu atapendeza sana’ nilitabasamu ‘asante sana’ na kuondoka. 
Nilipiga simu kwa wazazi na kuwaambia kwetu sitarudi kwani nilikuwa bize na ukizingatia likizo yenyewe ilikuwa fupi, hakuna aliyepinga, nilijua nadanganya ila kwaajili ya Prosper nilijiona niko sawa!. Sasa ilikuwa saa 12 nikiondoka Ubungo na Basi la Chaula huku nikimtumia Prosper mesege kuwa nimeondoka, hakuwa hewani, niliumia sana na kutamani hata tu mesege ya kunitakia safari njema, ila hakuwa haewani. Nilijpia moyo na safari iliendelea sasa tulikuwa morogoro! Niliingia facebook na kuona akiwa amejibu ‘my dear Irene usisahau zawadi pia saa 8 nitakuwa stend kukupokea, nakutakia safari njema na Malaika wakulinde rafiki yangu kipenzi” nilifurahi sana na gari iliendelea na safari sasa tulikuwa kitonga. Nilifurahi na kuchukua pochi yangu iliyokuwa na kioo na kujiangalia, nilijona kama nipo na Prosper Nlitabasamu pekee, sikuamini km kweli nitaonana nae na itakuwaje, lolote na liwe nilijiseme moyoni mwangu.. 
Tulifika Ilula na dereva akafungulia redio miziki iliendelea kama kawaida ila baada ya muda ilisikika Breaking news, yaani habari zilizotufikia hivi punde: “KIJANA MMOJA AMEGONGWA NA GARI KARIBU NA STENDI KUU IRINGA NA KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO. TAARIFA ZA AWALI ZINAONESHA NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU NA JITIHADA ZAIDI ZINAFANYWA NA JESHI LA POLISI ILI KUBAINI CHANZO CHA AJALI NA JINA LA MWANAFUNZI HUYO. MWILI UMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA” Mapigo ya moyo wangu yalipanda sana na jasho lilitoka makwapani, nilistuka sana mpaka abiria aliyekuwa karibu yangu alishaangaa sana. “Prosper jamani uko salama!” nilijikuta nikiropoka na watu wakageuka wote kuniangalia, jasho lilinitoka mpaka usoni, niljifuta na kuangalia nje nikaona kibao Ipogoro, nimefika niljisemea, sasa sijui prosper wangu! 
Niliingia Facebook na kuangalia meseji nilifurahi kuona Prosper kanitext “my Dear ndio naenda stend! Umefika wapi? Nakusubiri kwa hamu na zawadi yangu, karibu sana Iringa” Ila hakuwa online. Tayari tulikuwa stendi, nilijiweka sawa na kujifuta uso nijiangalia kwenye kioo na spidi kutabasamu nikisubri kupokelewa na Prosper. Nilichukua begi langu la mgongoni na kushuka huku nikiangalia huku na kule kama nitaiona sura ya Prosper! sikuona sura ya Prosper kabisa, nilijaribu facebook ila hakupatikana! Pembeni kidogo kulikuwa na watu wengi, wakiwa na huzuni, wengine wakisema wanaenda hospital, nilimuita dada mmoja nikamuuliza akasema kuna mwanachuo kagongwa na gari na kafariki, hivo anaenda hospitali kuangalia km ni rafiki yake Prosper ambaye alimuaga kuwa anaenda kumpokea rafiki yake wa DAR! Nilhisi kizunguzungu na miguu kuishiwa nguvu, niljikaza na kumwambia twende wote hospitali!!
Moyo wangu ulijaa wasiwasi mweingi mno na machozi yalinilengalenga nilifuta kwa kitambaa . Tulikatisha barabara na hatimaye tulitokea jengo lililoandikwa “IRINGA MORTUALY” miguu iligoma kuingia ila nikajilazimisha ‘dada twende’ alisema mwenyeji wangu. Nilijikaza na kuingia watu walikuwa wengi mno na wengine walikuwa wanalia, nilisikia kaka mmoja akipiga simu “ehh halo, rafiki yangu Prosper Assey katutoka kwa ajali ya gari wakati akiwa mjini kumpokoea mgeni wake” sasa nilikosa nguvu kabisa, tumbo lilikuwa likiuma na machozi yakitoka, Yule dada aliniangalia tu, waliturusu tuingie ili kujiridhisha kama ni mwenyewe niliingia na kisha droo ikavutwa daktari alifunua mwili kisha kwa macho yangu nilishuhudia Prosper wangu akiwa amefariki. Nililia sana kwa sauti kubwa mpka wakawa wananishangaa, nililia mno. Polisi walieleza uongozi wa chuo jinsi ilivotokea na chuo kusema kesho mwili utasafirishwa kijijini kwao Madege na hivo watakao sindikiza waandike majina. Nilitoka nje na kukaa kwenye mti huku nikilia sana! Nilichukua nguo zile nilizo kuwa nimemnunulia mpenzi wangu niliyempenda sana, niliumia zaidi kwani alikuwa amefariki ghafla bila kumwambia nampenda, ‘Prosper, Irene nakupenda sana, nakupenda mwenzio naumia mapenzi yananitesa Prosper kwanini hivi? Amka baba uone zawadi yako! Mimi nitampa nani jamanii?” nililia sana, waliendelea kandikisha na wanafunzi wenzake walijitokeza, wakike kwa wakiume, nilisogea nijiandikishe niende, lakini nilizuiliwa kwa kuwa hakuna aliyenifahamu kabisa. Niliumia sana, sikuwa na wakumweleza akanielewa kwa wakati ule, nilihisi mwenye mkosi nikikumbuka sura yake kwenye lile kabati kama vile anatabasamu ila alikuwa ameshaenda na udongo utammeza mpenzi wangu Prosper!
Sasa ilikuwa asubuhi na gari lilikuja kubeba mwili, nilimuona mama mmoja akilia sana “mwanangu mwanangu umefanya nini, amka mwanangu mamako nakutegemea” alilia kwa huzuni mno nilijikuta nalia zaidi, kwa haraka nilitambua alikuwa mama wa prosper!. ‘Yaani angekuwa mamamkwe wangu’! Niliwaza, mwili ulichukuliwa kwenda kijijini Madege kwa mazishi. 
“kwaheri Prosper nakupenda sana! upumzike salama mwanaume wangu, nilikuja kukwambia nakupenda Prosper ila umeenda, umetangulia hii yote kwaajili yangu, nisingekuwa mimi ungali hai Prosper nitakuja na tutakuwa wote pumzika mahali pema peponi ” nililia kwa huzuni mno walinishangaa kwa kuwa hakuna aliyekuwa akinijua gari liliondoka, nikabaki pekee pale mochwari…. 
kifo hauna huruma umemchukua mpenzi wangu Prosper kabla sijamwambia! Prosper moyoniv mwangu unaishi, zawadi zangu nimezitunza, thank hasa zawadi kuu ya usichana wangu! lala salama Prospe

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.