SIO KILA ANAYEKUONESHA KUKUPENDA SASA ANAFAA KUWA MUMEO AU MKEO.
Si kila anayeonesha kukupenda sasa anafaa kuwa mumeo au mkeo. Elewa kwamba kuna wanawake wengine ambao wao kupenda kwao hawamaanishi ni ili waolewe, wanapenda tu na kufurahia kampani lakini ukiwatajia ndoa, usije ukashangaa wakakataa kuolewa. Hawa wa sampuli hii ukiwalizimisha utakiona cha mtemakuni.
Namaanisha kwamba, wapo wanawake ambao lile neno ndoa tu kwao limewakalia kushoto lakini wanajua kupenda na kuwaridhisha wanaume. Ni sawa na kulazimisha kumuoa changudoa ambaye ni mtaalamu wa kudatisha, mtaalamu wa kubembeleza na mtaalamu wa kumpa furaha mwanaume yeyote kwa kuwa ameona pesa. Ukimuoa mwanamke wa aina hiyo ukidhani utapata mambo kama hayohayo, umeumia.
Hilo lipo pia kwa wanaume, kuna wale ambao wanaweza kuonesha upendo wa hali ya juu lakini hawako tayari kuingia kwenye ndoa. Ukilazimisha kuolewa na mwanaume huyo, umeula wa chuya kwani huwezi kuyapata mapenzi aliyokuwa akikupa kabla ya ndoa.
Kwa maana hiyo nihitimishe kwa kusema kuwa, lazimisha ndoa lakini kwa mtu ambaye una uhakika anahitaji kuingia kwenye ndoa na umemsoma vizuri na kubaini hawezi kuja kukuletea maumivu siku za baadae.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: