MWANAMKE ACHA KUHARIBU NDOA/MAHUSIANO YAKO KWA VITU VYA KIJINGA!


UTAMU KITANDANI APP

Umeolewa, au upo kwenye mahusiano yako siriasi. Hufanyi Biashara yoyote ambayo unaitangaza kwenye mitandao kusema kuwa wateja wako wanakufuata Inbox. Hivi kwanini unahangaika na Inbox za wanaume, kuchart na kujibu watu ambao huna mpango nao! Mwanaume anaanza kukusifia kwenye mitandao inbox, kisa ka like picha zako zote kwa pamoja unachanganyikiwa unafikiri sijui nini, una mtu wako, mke wa mtu kabisa!

Najua kuna watu ambao mnasema kuwa kuna mtu anaweza kukufiata kwenye mtandao wa kijamii akakupa madili! Lakini mtu wa dili unamuona, mtu anaanza kukusifia makalio unataka akupe dili. Lakini mtu anayekutaka, mwanaume aliyekutongoza hata akija kukupa dili kweli unafikiri mume wako au mpenzi wako akijua atachekelea.

Halafu kibaya hata meseji hamfuti, mnabaki nazo tu eti unajidanganya mume wangu hakagui simu yangu. upuuzi mwingine ni kuwa, hata kukaa kimya hamuwezi, umetongozwa tu huko na lijitu hulijui, limekuahidi upuuzi kibao kwakua akili zenu sijui zikoje ukasema umjaribu kumuomba pesa kujua kuwa yuko siriasi, ukamuomba kakutumia laki basi unajiona umefika.

Basi ndiyo unaenda kumuambia na shoga yako, kutangaza kuwa umeomba pesa umepewa. Hivi mimi ni mume wako, mpenzi wako, nakukuta umeomba mwanaume mwingine pes amabye hata humjui huko kwenye mitandao, halafu uniambia nilikua namjaribu, sijatembea naye, sijui na upuuzi mwingine gani unafikiri nitaendelea kuwa mume wako! labda kama maini yako yako shingoni.

Dada zangu, najua mtaanza mbona wanaume wanatongoza, iko hivi, nyie mnaweza kusamehe lakini wanaume ni wagumu kusamehe, sio mimi ndiyo ilivyo, ukiniuliza kwanini sina jibu, ni kama uniulize kwanini jumatano isingekua jumamosi! Sijui, ila ndiyo hivyo. Sasa kwanini uharibu mahusiano yako, ndoa yako tamu kwaajili ya mjinga flani ambaye inawezekana hata kuonana hamuwezi kuonana!

Mnaboa, na kama utasoma hii post, hutaingia kwenye simu yako, ukaanzia Facebook, ukafuta ma meseji na wapuuzi wote uliokua unachat nao mnadanganyana unaomba vihele,a ukaenda Instaggram, telegram mpaka Whatsapp basi unastahili kuachwa tu hamna namna, unastahili kuwa shamba darasa! Aisee nimechoka kuandika, acha!


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.