Kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanaume, unapaswa kujua mtazamo wake juu ya uhusiano huo.

UTAMU KITANDANI

Mabinti zangu
Kujeni hapa
Nasema hivi:-
Kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanaume, unapaswa kujua mtazamo wake juu ya uhusiano huo. Sio kila mwanaume anayekufata na kukwambia anakupenda anamaanisha, wengine hujaribu bahati zao kutokana na tamaa zao za kingono.
Dada zangu, kuingia kwenye uhusiano na mwanaume huku ukijiaminisha kuwa yeye ndiye atakuwa mume wako bila kupima mawazo yake kwa kina juu yako, hapo ni kuudanganya moyo.
Kitendo cha kujifungisha ndoa mwenyewe na kuamuwa kuishi kwa mwanaume ambaye bado hajawa tayari kwa ndoa, huko ni kujipotezea muda. Mtu hajakuoa,ushazaa naye au kakwambia anakupenda na anakueleza mambo yake ya kimaendeleo, hiyo isiwe sababu ya kwenda kuishi kwake bila ndoa.Inawezekana kwenye uhusiano huo umemfumania mara kadhaa na wanawake, umelalamika sana kuwa anakutendea visivyo, umemlalamikia kuwa anakutesa kwa tabia zake mbovu, still unamuita “mume wangu” na kuendelea kujipa moyo ipo siku atakuoa. Ifungue akili yako upya.
Ikiwa mwanaune hajakuoa na bado unavumilia mateso, jua mwenye matatizo ni wewe na si huyo mwanaume. Na huna haki ya kulalamika kuwa anakupotezea muda hapana, wewe ndio unajipotezea muda kwakuwa yeye bado anatafuta mchumba na bado hajapata mtu wa kuoa na ndio maana hadi leo hajakuoa wewe.
Angekuwa anakupenda na yupo tayari kuoa basi angekuoa wewe kutokana na uvumilivu wako. Kama unavumilia endelea kuvumilia hivyo hivyo huku ukiamini atakuoa, lakini kumbuka mwanaume akiwa anapata huduma zote za ndani ya ndoa ikiwa bado hajaoa, kwake suala la kuoa huja kwa kudra za Mungu.
Napenda kuwaamusha sana wadada maana ukiupoteza muda kwa kujidai unajua kuvumilia sana jitu na kujidai unajua kupenda hata usipopendwa basi jua kabisa wewe muda wako una expire.. Yaani muda wa kujichagulia mme ni kuanzia 21-28 ukifika 29 utaanza kukutana na waume wa watu 30 na kuendelea utaanza kuwaza bora uzae tu ulee maana vija wote hawatakutizama kumbe uliupoteza muda wako kwa li mtu lililokua danganyanyifu na laghai na ulilijua kabisa ila ukajidai tu wewe mgumu wa kupenda..
Anayekupenda yeye ndio anahangaika na wewe siyo kwa kukupa pesa no kwa kukuweka sawa kwa kutaka akuoe.
Upo nyonyo?!

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.