JINSI UNAVYOZIDI KUMFAHAMU MPENZI WAKO KIUNDANI MAMBO HAYA LAZIMA YATOKEE
Ukweli ni kwamba jinsi unavyozidi kumjua mtu kiundani, ndo kadri utakavyoona mienendo yake vizuri zaidi, Maana kuijua tabia au mienendo ya mtu unahitaji muda zaidi, ziko tabia hujificha zenyewe kutokana na mazoea lakini unapokuwa na ukaribu na mtu utabaini hata zile tabia za ndani sana ambazo mtu anazo, Hivyo ndo ilivyo kwa sababu TABIA YA MTU NI KAMA NGOZI kuna wakati unaweza kuitaja ngozi ni nyeusi na kumbe kuna maji ya kunde ndani yake, Hii ndo sababu Mahusiano na Ndoa zinakwama maana wengi hawazijui tabia halisi za wenza wao, Hakuna mtu atataka MAHUSIANO asidanganye, Ni asilimia ndogo sana mtu kusema ukweli pindi anapokuwa anahitaji nafasi kwenye Mapenzi, Na hilo limesababisha watoto wengi wanatelekezwa ama kukosa malezi ya mzazi mmoja, Sababu kubwa inayosababisha hayo ni urafiki kutodumu kama ilivyotarajiwa, Unaweza ukafikiria unampenda mtu mpaka uone matendo yake ya upendo kwako na usiweze kuona uhalisia ila ukaona picha ya matendo ya upendo, Nimejifunza MAPENZI MATAMU NA YENYE AMANI YA WATU WENYE KIPATO CHA CHINI... Wengi wanapokuwa hana hela au ana misongo au njaa kimbilio lao kuu PENZI ili apate faraja, Nisikufiche uhitaji mkubwa kwenye MAPENZI ni namna tunavyoweza kubebeana madhaifu na kufarijiana, kwa upendo wa Mungu hakuna ambaye atapenda kumliza mwenzie, wengi wanalizwa kwa njia walizopitia kupokea upendo wa kipepo yaani Unampenda mtu kwa kumng'ang'ania wakati hakupendi na wala huhisi vibaya, Upendo ni kitu cha tofauti sana hasa unapokuwa na Mtu ajuaye kupenda utajiona VIZURI! Upendo ni kuchagua kumhudumia mtu ambaye ameushika MOYO WAKO... Upendo ni kumbeba mtu bila kujali upendo wake mdogo kwako, Upendo ni utulivu na upole ili kuruhusu MOYO ufanye kazi yake, Upendo wa kweli haugawanyiki kwa namna yoyote ile, Upendo wa kweli ni mgumu kuuelewa na mara nyingi unakuingiza kwenye kero, Upendo wa kweli ni maumivu na kujitoa kwa mwenza wako, Upendo ni kuhisi hatari muda wote kwani MOYO hutafuta namna ya kujiokoa, Upendo wenye nguvu husababisha ujasili kwenye hatari yoyote NI KAMA KUJITOSA BAHARINI wala usijue utaokolewa ama utajiokoaje! Yote hayo yanaletwa na neno moja UPENDO WA DHATI... Kuupata upendo huo ni nadra ila upo unazagaa tu na wenye kujaaliwa KUPENDA KWA DHATI wanateseka pa kuuweka Upendo wao, Hesabu ya MAPENZI haina cha profesor kwani hata wenye PhD ya Hesabu wanalia juu ya MAPENZI... Wewe Bwana ukiona umependwa na unampenda shikilia hapo hapo maana ni ngumu sana KUPENDWA UNAPOPENDA.
#Elista_kasema_ila_sio_she ria
#Elista_kasema_ila_sio_she
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: