KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 20





ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: Wakati huo huo sajent Kibabu nae, akiwa amekaa seat ya mbele ya gari hilo, aliweza kumwona vyema kabisa Monalisa, akikimbia na kuangukia barabarani, hapo sajent Idd Kibabu akaachia tabasamu la fisi, “kiulaini kama kumsukuma mlevi” alisema Kibabu akitegemea kusikia miripuko ya risasi, zikimiminika kwa Monalisa, na kweli mala ikasikika pah! pah! pah! pah!, endelea........
.
Ni milipuko ya risasi, lakini aikuwa kama ilivyo tarajiwa, maana haikuelekea kwa Monalisa, na wala aikutoka kwa askari, waliopo nyuma ya gari, kwa macho yake Monalisa aliona, mchakazo mkubwa wa Risasi ambazo alijuwa fika zinatoka kwa Edgar, zikitoboa kwenye shingo za askari kama watatu hivi, waliopo nyuma yagari ungezema walikuwa wana pigwa na nyanya masalo, maana shingo za askari wale zili vuja damu, ambazo zilitawanyika na kuwa mwagikia wenzao, ovyo ovyo, Monalisa akiwa ameganda pale chini akisikilizia maumivu makali ya goti alilo libamiza chini, aliwaoana wale askari walio pigwa risasi, wakining’inia kwenye mabomba ya gari lile, huku bundu kizao, zikiwatoka mikononi na kuanguka chini kabisa yani barabara, wakionyesha kuwa wamesha poteza maisha.
“endesha gari tunashambuliwa wewe” alipaza sauti sajent Kibabu, sambamba na mtafaruku mkubwa waskari wake, waliokuwa nyuma ya gari, ambao walipiga kelele za kuomba msaada, wakutoka kwenye kifo, kila mtu akitumia lugha aliyo ijuwa yeye, ni baada ya kuona wenzao wamesha tandikwa risasi za shingo,
Dereva Kado alifanikiwa kuliondoa gari, na kutoka mahali pale, huku gari likishindwa kukimbia sana kutokana na kutobolewa tairi moja la nyuma, ata hivyo lilifanikiwa kusogea umbari kama wa mita mia tatu mbele,
hapo Monalisa akiwa bado yupo lake chini, akihisi kama vile miguu yake imeishiwa nguvu, kutokana na kugonga goti chini kwanguvu, akamwona Edgar akija mbio mbio, kumfwata, ata alipo mfikia aka mwona akichukuwa mikebe ya risasi ya bunduki zilizo dondokea barabarani, yani zawale awalio charazwa risasi, na wakati huo huo akaliona gari jingine la polisi, likija mbio mbio kutokea upande lilipotokea lile la kwanza, hapo Edgar akazubaha, akamfwata Monalisa, aliekuwa amenyooshea mkono, nikama alikuwa anataka msaada wakuinuliwa toka pale alipo kuwepo, “wengine wanakuja, tuondoke hjaraka” alisema Edgar, huku ana ukamata mkono, wa Monalisa na kumvuta kwake kwanguvu, kwa maana ya kumwinua, nakweli Monalisa akainuka, lakini akuwa anaweza kutembea vizuri, kutokana na maumivu yagoti, hivyo kwa msaada wa Edgar wakaondoka mahari pale na kuzama tena porini, wakibadiri uelekeo, sio ule walio kujanao mwanzo, sasa walielekea mashariki zaidi, upande ambao walizidi kuzama porini, na kuingia kwenye bonde moja kubwa ambalo liliunganika na mto flani mdogo,
Huku wale porisi wakitumia dakika kama tano hivi kujijenga tena, na kuungana na wenzao waliokuwa kwa mguu, na kuanza kushambulia kwa pamoja, lakini nikama walikuwa wanawshambulia hewa, maana tayari wakina Edgar walisha ingia kwenye korongo, na kuzidi kutembea mbele, huku Edgar akimpa msaada wakutembea Monalisa,
“hacheni kushambulia nyie wajinga, mna mshambulia nani sasa, hamuoni kama hakuna mtu mbele yenu” aliongea Koplo Mapombeka, na wale askari wahacha kushambulia, na wote waka kimbilia kwenye gari lililo shambuliwa, ambako Sajent Kibabu alikuwa amesimama kama sanamu anawatazama askari watatu walio kuwa wana ninng’inia kwenye ma bomba ya chuma ya gari lile, wakiwa wana vuja damu sehemu za shingo, “haaaaa! kauwa tena?” lilikuwa swali lililo ambatana na mshangao, toka kwa koplo mapombeka, ambae akushangaa peke yake, ata wale askari wengine ambao hawakuwepo kwenye gari nao walikuwa wameduwaa, wasiamini macho yao, “jamani huyu mtu mbona wa kawaida tu alafu anatusumbua namna hii?” aliuliza mmoja wa askari wale kwa mshangao,
Sajent Idd Kibabu kwa mala ya kwanza alionekana akiwa ameganda kama ville aliuacha mwili pale na kuondoka zake, maana alikuwa amesimama huku amekodoa macho kutazama miili ile mitatu ambayo sasa ililikuwa ina shushwa na kupakizwa kwenye gari jingine, ambalo nalo kuna askari walikuwa wanashusha silaha na bahadhi ya vyakula vikavu, yani mikate biscuit na juice, iliwaweze kuwapakiza wale askari marehemu, huku KADO nae alikuwa anaangaika kuandaa jerk na tairi, kwaajiili ya kubadilisha lile lililo tobolewa na risasi, “siwezi kuamini kama huyu mtoto, anaweza kufanya mambo kama haya” alisikika sajent Kibabu akiongea kwa sauti ya chini iliyo ashilia kuto kuamini, anaaacho kiona mbele yake, siyo yeye peke yake ata askari wenzake aliotoka nao songea, ambao kwa sasa walibakia nne na PC Kado ndie ange kuwa watano, maana kati ya wale askari watatu walio chalazwa risasi, wawili walikuwa ni askari wa sajent Idd Kibabu, yani aliotokanao songea,
Kibabu alitazama kwa machungu sana wakati miili ile ina pakizwa kwenye gari, pamoja na askari mmoja wa hapa makambako, alie tandikwa risasi begani, kule porini, tayari kupelekwa mjini, ili nae akapate amatibabu, “hivi huyu ni mwanafunzi au jambazi kweli?” aliuliza tena Kibabu huku akimgeukia PC Charles, alie kuwa amsimama karibu yake, bahati nzuri hakukuwa na askari wa makambako karibu yake, “atamimi naingiwa na mashaka juu ya huyu kijana” alijibu PC Charles, huku wakilisindikiza kwa macho gari, lililo ongozwa na koplo Mapombeka, likiondoka kwa speed kali, huku askari watatu wakiwa wame ning’inia nyuma.
Hapo sajent Kibabu akageuka, na kuwatazama askari walio tawanyika eneo lile, “Pc Khassim na kundi lako wafwatilieni awa washenzi, na sisi tuta endelea kutembeae na barabara, mawasiliano muhimu” alisema Kibabu kwa sauti iliyo jaa machungu makubwa, “akikisheni huyu mshanzi ana uwawa mala moja akipatikana, tena kifo cha machungu” alisistiza Kibabu, “ndiyo afande itatekelezwa” alijibu polisi CONSTEBLE Khassim, na kuliamulu lile kundi alilo kuwa nalo porini kwa mguu, kuchukuwa bahadhi ya vyakula na kuanza safari, kuelekea kule waliko kimbilia wakina Edgar, ilichukuwa dakika tano kuchukuwa vyakula na kunaza safari, wakiwaacha wakina Kibabu wana malizia kubaadiri tairi. *******
Nyumbani kwa mzee Anderson, kama ilivyokuwa mwanzo, nje walionekana watu wachache waliokuwa wanakunywa pombe, uku story zikiwa ni zile za kutekwa kwa Monalisa, bibi harusi mtarajiwa, ambea leo ilitarajiwa kuona akivishwa pete yauchumba, tofauti hapo nje kwa sasa lilionekana gari la jeshi, aina ya land rover 110, mali ya jeshi la ulinzi, ambalo ndani yake alionekana askari mmoja mdogo mdogo hivi, akiwa amekaa mbele ya usukani, akiegemea kiti cha dereva kichovu kweli kweli, akionyesha amechoka sana, haraka haraka ni kwamba, kanali Kisona alikuwa amesha wasili hapa kwa bwana Anderson, “samahani mwanajeshi karibu chakula na vinywaji” ilikuwa sauti ya mama mmoja mtu mzima iliyo mstua huyu kijana mdogo dereva wa Kanali Kisona, ambae toka asubuhi haja pata nafasi ya kuweka chochote tumboni mwake, “asante sana mama” aliitikia askari private Rajab, huku anafngua mlango wagari, akijuwa kuwa amesha pata shibe, maana njaa ilikaribia kumzimisha. Rajab aliongozwa na yule mama mtu mzima, ambae alienda kumwonyesha sehemu ya kwenda kukaa, ilikuwa pembeni kidogo ya watu wengine walio kuwa wana kunywa pombe, alafu yule mama akamletea kijana sahani ya pilau na soda, kisha na yeye kaa pembeni, “nzani mmekuja kutusaidia kuhusu Monalisa?” aliuliza yule mama, huku akimtazama Rajab ambae aliasha anza kulifinya pilau, akishushia soda.
Nikweli kamanda Kisona alikuwa ndani yasebure ndogo, ndani ya nuymba ya tajiri huyu, ambayo ina sebule mbili, “poleni sana jamani” alisema Kanal Kisona, akiwatazama kwa hawamu watu wote waliokuwepo mle ndani, yani mama na baba Monalisa, baba na mama Erasto na Erasto mwenyewe, “tuwezi kupoa baba, mpaka tujue Mona yupo wapi?” alisema mama Monalisa, kwa sauti ya kichovu,uliosababishwa na kilio mfululizo, “usijari mama, naimanai watoto watapatkana wakiwa salama,” alisema Kisona kwa sauti tulivu iliyo asiriwa na hali ya mama huyu, “watoto. watoto wangapi, au kuna mwingine amepotea?” aliuliza baba Monalisa kwa mshangao, huku wote mle ndani wakishangaa pia, “inamaana amjasikia kuwa tukio hili linamuusisha na kijana Edgar Mbogo, rafiki wa Monalisa” alisema Kisona, na hii ilikuwa ni makusudi ili kuangalia watu hawa wanaichukuliaje taharifa ya Edgar kumteka binti yao, hapo aliweza kuona sura za hawa binadamu zikiwa zina kunjika kwa hasira, “usije ukamtaja tena huyo mshenzi kuwa rafiki wa Monalisa” alisema mama Erasto kwa hasira kali sana, huku Erasto akijisonya sonya kwa hasira, “kwanini jamani, kwani mna ugomvi na familia ya mzee Mbogo?” aliuliza Kisona huku akijuwa fika jibu litako kuja ni hili, “yani baba ungejuwa huyo kijana alivyo anaza kumfwata fwata binti yetu toka utotoni, ata usingesema” alisema mama Monalisa, kwa sauti ya mikwaluzo iliyosababishwa na kilio cha muda mrefu, “lakini uwezi kusema michezo ya utoto ndio iliyo sababisha muamini kuwa Edgar amefanya hicho mlicho sikia” alisema Kisona kwa sauti tulivu, iliyo jaa bisara, “utoto mtu aliandika na barua kabisa, mtoto gani anajuwa kutongoza, yule ameamua kuni komoa mimi” ilikuwa ni kauri ya Erasto iliyo ambatana na hasira ya illevi levi, “kijana unazani anakukomoa kwa sababu gani?” aliuliza Kisona huku akimtazama Erasto, kwa sura tulivu kabisa, “sababu nime mzidi kete, yeye sialikuwa anamtaka Mona” alisema Erasto kwa sauti ile ile yenye uchungu na hasira iliyo zidiwa na ulevi, “hapo nimenza kuelewa, wewe ulikuwa rafi wa Edgar sio?” aliuliza Kisona na hapo hapo Erasto akadakia, “tena ata barua ya kumtongoza Mona alinipa mimi niipeleke” hapo Kisona akacheka kidogo, “ok! wewe mjanja sana, kwa hiyo uka mpa Monalisa kisha auka enda kumweleza mama yake?” kauli ya Kisona iliwafanya wote mle ndani watazamane kwa zamu, wakimwona huyu jamaa, nikama mnajimu, yani watabiri wazama za kale, akuna alie mjibu wala kusema neno, “hivi nikiwaambia kuwa, watu hawa wamekaa miaka mitatu pamoja, na Edgar akuwai kumfanyia lolote baya binti yenu, mnaweza kuamini?” aliuliza tena Kisona, hapo nikama baba Monalisa alikuwa ana zinduka toka usingizini, “kwa hiyo Edgar nae alikuwa anasoma Mbeya?” aliuliza kwa mshangao bwana Anderson, huku akimkazia macho Kisona, “ndio, tena jana wame maliza chuo pamoja, na ndio wakapata matatizo wakiwa njiani wana kuja songea” alisema Kisona, akionyesha kuwa anaelewa kinachoendelea, “sasa kwanini amteke binti yetu?” aliuliza mama Monalisa, “unazani Monalisa ametekwa kama mlivyo sikia?” aliuliza Kisona akimtazama, mama Monalisa, “sasa unazani polisi wanadanganya?, najuwa tu! Edgar amemteka Monalisa ili aniwai” kauli hiyo iliiyo mponyoka Erasto kutokana na mipombe yake ilimshangaza kila mmoja mle ndani, ata wazazi wake, kasolo Kisona peke yake alie ishia kucheka kidogo, “wazee labda hamjasikia taharifa ya pili, nikwamba Edgar anausishwa na ujambazi ulio tokea juzi usiku hapa songea, wakati yeye, na binti yenu walikuwa Mbeya” hapo mzee Anderson na mke wake walitazamana, wakitafasiri maluwe luwe yaliyopo kwenye hadithi ya Monalisa na Edgar, “unataka kuni ambia kumtu amedanganya kuhusu Edgar kumteka mwanangu?” aliuliza mama Monalisa, kwa sauti yamshangao, “tena siyo hivyo tu! amani na waambia kuwa, bila Edgar, mngekuwa amesha letewa taarifa ya kifo cha binti yenu” alisema Kisona kwa sauti yenye msisitizo, “huyu lazima atakuwa ametumwa kuja kumtetea Edgar” alisema Erasto, ambae akiri yake ilimtuma kuwa, mpaka sasa, iwe kwa hiyari au lazima, bikira ya bibi harusi hipo hatarini, Kisona aliishia kucheka tu!, “Misago ebu ongea na Erasto, akae kimya, maana sasa naanza kupata mwanga” alisema mzee Anderson akimweleza baba Erasto.
“naujuwa wasi wasi wa huyu kijana, unajuwa mapenzi ayazuiliki, ata kama imepita miaka mingi, kiasi gani, mala nyingi, waliopendana utotoni ndio walio zikana uzeeni, na waliopendana chekechea ndio walio owana chuoni, kwahio Erasto ondoa hofu, kama Mona ana kupenda awezi kukusaliti” alisema Kisona, kisha akaaga “wazazi na majirani nawaomba muwe watulivu ogopeni kutoa taharifa ovyo kwa mtu yoyote, na ta kigundua walipo binti zenu tunaomba msiwe wepesi kutoa taharifa hovyo” alisema bwana Kisona kisha akainuka na kutaka kuondoka, ila akakumbuka jambo aka mgeuka na kusema, “tafadhari msi mweleze mtu yoyote haya tuliyo yangea” alisema Kisona kisha akaondoka zake, akiwaacha wanafamilia hawa wakitazama kwa mshangao, nikama walikuwa wameganda kwa dakika nzima, kisha bwana Anderson akagutuka, “mke wangu naenda Makambako” alisema baba Mona huku anainuka haraka toka kwenye kochi na kuingia chumbani kwake, akifwatiwa na mke wake, “baba mona namimi naenda” alisema mama Monalisa, huku wakiingia chumbani, na kuwaacha wageni wao wanatazama, kwa mshangao wa nukta chache alafu nikama waliulizana kuwa tunangoja nini, nao wakakurupuka, na kukimbilia nyumbani kwao ambapo ni nyumba ya tatu kutoka kwa kina Monalisa,
Kisona alishangaa kuona wanafamilia hawa wakipita mbio mbio, nusu wamgonge wakati ana taka kuingia kwenye gari, akumwona dereva wake Rajab, akageuka huku na huku akamwona akiwa ana nawa mikono, akionyesha wazi kuwa tayari alikuwa amesha finya pilau, Kisona akameza funda lamate,******
Saa kumi za jioni, Kibabu alikuwa amesimamisha gari pembezoni mwa barabara hii ya vumbi, kilomita zaidi ya kumi natisa, toka pale waliposhambuliwa na Edgar, sasa aliweza kuona magari machakavu ya mizigo na matrekta, yakielekea mjini na mizigo ya viazi mviringo na matunda mbali mbali, yanayopatikana kwa wingi sana ukanda huu, yakielekea mjini, na wao waliyakagua kuakikisha kuwa Edgar na Monalisa hawa piti eneo lile wakitumia magari yale, “Mike, hivi huyu kijana ndio yule tulie okota kitambulisho chake kuwa ni mwanafunzi au ni mwingine?” aliuliza sajent Kibabu, akionyesha kuchoshwa na mwenendo wa oparetion hii ya kuwasaka vijana hawa, “ndio yeye afande, kwani vipi?” aliuliza Mike, ambae alimwona vyema Edgar pale hotelini, “huyu jamaa anaonyesha kuwa na mafunzo yakijeshi, tena ya kivita, “maana ukiachilia kwenye matumizi ya silaha, pia ana uwezo wa kutumia cover (maficho), kule barabarani ame mwokoa yule binti na kutukimbia kwa under fire cover, tena closs fire, “kukatiza kwenye mapigo) na alicho kifanya pale nyuma, ni mapigano ambayo utumiwa na spcial force, yanaitwa pin down fire, and movement” alisema Kibabu ambae alionekana kuwa na wasi wasi na Edgar, “inamaana ana mafunzo makubwa kuliko sisi?” aliuliza Mike, kwa mshangao, “ndio, tena tusipo angalia vifo vitaongezeka, ebu ona ndani ya masaa machache tume wapoteza askari watano na huyu wasita amepigwa begani” alisema Kibabu, huku akiwatazama askari wake waliokuwa wana endelea kukagua magari na materctor yaliyobeba mazao toka mashambani, huku wakijigawia bahadhi ya matunda, kwaajili ya kuweka tumbni mwao, baada ya kuwa wamesha maliza mikate na juic zao, na kplo Mapombeka alikuwa bado hajarudi toka mjini*******
SSP Kingaramakiwa tayari amesha jipanga kwa safari ya Makambako, alitoka nje ya ofisi yake, ghorofa ya pili, na kushuka chini, ambako alikuta magari mawili ainaya Toyota land cruzer boy wazi, ya pick up, yakiwa na sakari kilamoja watano, wenye bunduki na mabegi yao, wakimsubiri tayari kwa safari, lakini kabla hajaingia kwenye gari akaliona gari la kanal Kisona likiingia eneo lile la ofisi za polisi mkoa, “kumbe ninge chelewa kidogo, ninge kukosa bwana Kingarame?” alisema Kisona akiwa amesha shuka kwenye gari na kumfwata Kingarame pale alipsimama, yani nje ya gari alilo tarajia kupanda, “tana ata hapa unanichelewesha” alisema Kingarame kwa zarau, “kwani unaenda wapi kamanda?” lilikuwa swali, lakini nikama lilikuwa linakejeli ndani yake, maana Kisona alishaona dalili za safari kwa askari na magari yale, “sidhani kama inakuhusu, ipo chini ya polisi” alisema Kingarame, ambae aligeuka na kufungua mlango, lakini Kisona akamwai, “ila unajuwa kuwa hao unao wafwata ni wanafunzi” kauri hiyo ilimstua sana kingarame, akageuka na kumtazama Kisona, “mwanafunzi ndio nini, wakati amesha poteza askari wangu wawili?” aliuliza Kingarame, kwa sauti yachini, huku akimkazia macho Kisona, “uwezi kuhisi kuwa wamefanya hivyo kuokoa maisha yao, na siyo majambazi kama unavyo zania?” aliuliza Kisona huku akimtazama mzee huyu, ambae alionekana kuanza kujaa hasira, “hivi kanali kwahiyo unataka tukubari mauwaji kwasababu wana jikoa, kwahiyo jambazi akiuwa, ni sahihi kwa kuwa anajiokoa?” aliuliza Kingarame kwa sauti ya juu, “kamanda naomba tubadiri jina tusisema ujambazi tuseme mbio za kijiti” alisema Kisona huku akitabasamu, “unamaanisha nini, au umeishiwa la kuongea?” aliuliza kwa jazba Kingarame, “kwani wewe unaonaje, Lukas ame wapa wakina Monalisa, sijuwi kama mta wauwa, au wata fikisha ushaidi” hapo Kisona aliweza kumwona Kingarame akitoa macho kama vile amekabwa shingoni, kwajinsi alivyo onekana akingaika kutafuta neno lakuongea, lakini Kisona akamuwai, “nimekuja kukuomba ondoa askari wako karibu na vijana wale, kabla watanzania awaja sikia kinachoendelea nyuma ya panzia” alisema Kisona kisha akaakageuoka na kutaka kuondoka zake, lakini kabla hajafika mbali akasikia, “afande kuna taharifa nyingine kutoka makambako” Kisona akageuka na kutazama kule sauti ilikotokea, alimwona askari wakike yule msaidizi wa Kingarame ambae malanyingi uwa anamkuta ofisni kwa kamanada huyu, alie kuwa anakuja mbio mbio, “kuna nini tena?” aliuliza kingarame kwa shahuku, Kisona akiwa ametega sikiokusikiliza taharifa hiyo, “ande kuna taharifa ya askari wengine watatu, wameuwawa kwenye mshambulizi na yule jambazi” hapo Kisona aligeuka nakumtazama Kingarame macho yao yaka gongana, Kisona akatabasamu na kuanzakuetembea kuelekea kwenye gari lake.
“Roja wewe ukiniacha nyumbani, kaliweke gari pale ofisini, makambako tutaenda na mzee Mbgo yeye ataendesha gari” alisema Kisona, huku safari ikiendelea kuelekea nyumbani kwa Kisona,*******
kati kati ya msitu huu, uliopo katikati ya Njombe na makambako, ndani ya bonde moja kubwa sana ambalo limeungana na mdo unao anzisha maji ya nayo enda kwenye mto mkubwa wa mufindi, walionekana Edgar na Monalisa wakiwa wana jikongoja kuufwata mto uo ambao ulikuwa unazidi kuongezeka kila walipo zidi kutembea mbele, wakiwa wamechoka sana huku matumbo yao yakiunguruma kwa njaa, “Mona ebu tupumzike kidogo nikutazame goti” alisem Edgar ambae alikuwa na kazi ngumu sana ya kumsaidia Monalisa kutembea, “haya tupumzike, lakini wawezi kutukuta kweli?” aliuliza Monalisa, huku wakisogea kwenye mti mmoja mfupi hivi, kati ya michache iliyopo pembezoni mwa mto huu mdogo, ambapo Monalisa alikaa chini na kujilaza kabisa kwa uchovu, huku Edgar akiwa amesimama mbele yake, akimtazama Monalisa, pale alipo lala, alianza miguuni mpaka kwenye maja yaliyoonekana vizuri ndani ya suruali ya jinsi asa kutokana na kulala chali, ukweli Edgar aliwezakuona hips za Monalisa zilivyo chomoza vyema, akatama jinsi mtuno wa kitumbua ulivyo jichora, chini ya kitovu cha binti huyu, mwenye tumbo dogo ambalo lilikuwa wazi, baaada ya kupanda juu kidogo, likiacha wazi kitovu.
Monalisa alilala pale chini, huku akisikilizia njaa tumboni mwake, waliwaza kwa muda mchache kisha aka tazama mbele yake akamwona Edgar amesimama mbele ya, ana mtazama, hapo Monalisa akahisi kuwa Edgar anatazamanini, haraka sana, Monalisa aka jiziba sehemu ya tumbo na kitumbua chake, huku anapandisha macho yake usoni kumtazama Edgar, na macho yao yaka kutana wote wakatabasamu.“Mbona unanitazama hivyo?” aliuliza Monalisa, huku akikwepesha macho yake, yasitazamane na macho ya Edgar, “nashangaa” alisema Edgar, huku anaanza kuvua mkanda wa bunduki na kuiweka chini, yani pembeni kidogo ya pale alipo, kisha aka chuchumaa na kuushika mguu wa Monalisa, ule ulio umia, “unashangaa nini?” aliuliza Monalisa ambae sasa alikuwa anaweka vizuri tishet lake kuzuwia tumbo lake, “yani licha ya vurugu zote hizi na uchovu, lakini bado unaonekana mzuri sana” alisema Edgar, kwa sauti tulivu iliyo jawa na upendo kwa rafiki yake wazamani,ambae aliachia tabasamu pana sana la furaha, huku Edgar akiwa anafungua kamba za viatu miguuni mwa Monalisa, “kwani Edgar, mimi ni mzuri sana?” aliuliza Monalisa huku akimtazama Edgar alie kuwa meunamisha usowake kwenye mguu wa Monalisa, “katika maisha yangu sijawai kukuona ukiwa mbaya” alijibu Edgar, ambae sasa alisha mvua kiatu kwenye mguu ulio umia, na kuaza kupandisha sulluali hii ya jinsi, mpaka kwenye goti, “kwahiyo unanipenda?” aliuliza Monalisa huku akijichekesha, “sijawai kukuchukia” alijibu Edgar, ambae sasa alikuwa anatazama michubuka kwenye goti la Monalisa, huku ameulaza mguu laini wa binti huyu kenye mapaja yake, “mh! kwani umaanisha toka utotoni?” aliuliza Monalisa huku akimtazama Edgar alieuwa ana vua bgi lake la mgongoni na kulifungua, “sidhani kama kunakipindi kingine ambacho tuliwai kuonyeshana upendo mkubwa kuliko kipindi hicho” alijibu Edgar huku anatoa pamba spiriti na bandeji, kwenye mkoba, nizile walizo nunua kwa rehema jana usiku.
Monalisa alicheka kidogo, kicheko flani cha kivivu, “mimi naona sasa ndio unanionyesha upendo mkubwa sana, ule ulikuwa ni utoto tu!” alisema Monalisa huku akimtazama Edgar alie kuwa anaandaa dawa kwaajili ya matibabu, Edgar alicheka kidogo, kisha akamtazama Monalisa, macho yao yaka kutana, “kama uliwai kuzarau upendo wangu kwako, kipindi kile, basi ulikosea sana, ujawai kunitoka kichwani mwangu” alisema Edgar kwa sauti ambayo iliuchoma moyo wa Monalisa, “kwanini unasema hivyo, unamaanisha kuwa mimi ndie nilimwambia mama kuwa umeniandikia barua?” alisema Monalisa kwa sauti ya kukwepa lawama, lakini Egar hakujibu, zaidi alimimina spiriti kwenye pamba, “ata kama ukini kasirikia, ni ujinga wako mwenyewe” alisema Monalisa kwa sauti kali iliyo anza kutawaliwa na hasira, na kitu kama ili mkorofisha Edgar, ambae aliukamata kwanguvu mguu wa Monalisa, na kuanza kupakaza pamba yenye spriti kwenye kidonda cha Monalisa, ambae aliachaia yowe moja kali la uchungu, “mamaaaaaaaa! inaumaaaaaaa” lakini Edgar kama vile hakuwa na masikio aliendelea kupakaza ile spiriti kwenye kidonda cha Monalisa akiwa bado ame ukamata kwanguvu mguu wa binti huyu mrembo, baada ya kuona inatosha akaachia, “mshenzi wewe umefanya makusudi” alisema Monalisa huku akifuta machozi usoni mwake, “makusudi vipi, kama ungeteaka isiume, unge weka mikojo yako”
itaendelea hapa hapa kwa





(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.