KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 22
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA 21: “eti Eddy bado unanipenda kamazamani?” swali la Monalisa lili mstua Edgar, ambae aligeuka na kumtazama Monalisa,ambae anae alikuwa amemkodolea mach huku anatabasamu, “sijawai kukuchukia ata sikumoja,” alijibu Edgar, “basi nipe Jacket lako nasikia baridi” endelea......
Edgar alitabasamu kidogo, kisha aka lifungua jacket lake ambalo muda wote alikuwa amelifunga kiunoni, na kumpatia Monalisa, ambae alilivaa mala moja, na safari ikaendelea, wakiufwata moshi ambao ulikuwa una onekana ukifuka mbele yao, umbali wa kilomita moja na nusu. ******
Jioni hii Rehema alikuwa dukani kwake, akiendelea kuuza dawa, huku muda wote akijutia kitendechake cha kuwandoa wakina Edgar mjini na kuwapeleka kule Utwango, wakai akiwa katika mawazo mazito ya kujishushia lawama, mala akapita rafiki yake mmoja mkubwa sana Lusy, anae fanya kazi hospirali ya kitongoji cha Makambako, ambae mala nyingi sana uwa anampa wateja wa dawa, kwa kuwaelekeza waende wakanunu hapa, akiwatajia jina la duka nasehemu lilipo, “niambie Rehema mbona kama mnyonge hivyo?” aliuliza Lucy ambae aliona mwonekano wa rafiki yake huyu, “uchovu tu vipi mbona leo umechelewa kurudi?” aliuliza Rehema, maana mida ya kurudi kwa Lusy, uwa ni saa nane mchana, sasa ilikuwa ina ingia saa kumi nambili nanusu, “mwenzangu ni umbea tu! ulio nichelewesha” alisema Lucy aliekuwa kwenye dirisha la kuuzia dawa, Rehema akiwa ndani, “he! kunanini tena dada?” aliuliza kwa shahuku huku anatega sikio, “ndugu yangu polisin sijuwi wana lisaka jambazi gani huko porini, wlinawauwa hilo, mpaka huruma, yani sasa majeruhi wameaua kuwapeleka Njombe” taharifa hiyo ikamshtua sana Rehema, “he! sasa hao majambazi wamewakamata?” aliuliza kidadisi Rehema, “wawakamatie wapi, yani wanavyo angaika huko porini mpaka huruma” alisema nurse Lucy, ambae baada ya muda mchache akaaga na kuelekea kwake, akimwacha Rehema ana tafakari.
Nabaada ya kutafakari kwa muda mfupi akaona nivyema ile habari ikimfikia bwana Kisona, hivyo Rehema akaindea simu yake ya mezani, na kupiga nyumbani kwa rafiki yake Elizabeth Leonard, lakini yote kwa yote akaambiwa kuwa Kisona yupo safarini, anaelekea Makambako, lakini taharifa hiyo aikumzuwia Rehma kumwachia ujumbe Elizabeth, yani enda Kisona atapiga simu amweleze kinachoendelea, na endapo yeye atakutana nae basi ata mweleza kinacho endelea.*****
Giza lilisha tanda, mida ilisha kuwa saa moja na nusu, sajent Idd Kibabu na kundi lake la askari walikuwa wame gawanyika kwa makundi mawili makubwa, kundi moja likiongozwa na yeye kibabu, la pili liliongozwa na koplo Mapombeka, ambae alikuwa amesha rudi toka Njombe alikopeleka wagonjwa, na kuchukuwa maitajio mengine kama alivyoagizwa na sajent Kibabu, kundi la kwanza ambalo ni la kibabu, lili bakia pale pale ambapo walikuwa toka mwanzo wana kagua magari ya tokayo mashambani, ambayo sikuzote uwa yana pita asubuhi sana kuelekea mashambani na kurudi jioni, huku kopolo John Mapombeka na kundi lake, wakiwa wame sogea mbele zaidi, wakifanya doria, kuakikisha Edgar na Monalisa akatizi eneo hilo la barabara, “mka kesho asubuhi inabidi tuingie kwenda kutatfuta mabaki ya miili yao” alisema Koplo Mapombeka, wakiwa njiani wanazidi kusonga mbele, “kivipi?” aliuliza Mike, ambae alikuwa kundi moja na koplo huyu kutokea Makambako, “kama wata ingia ndani zaidi ya msitu huu, lazima watakutana na wanyama wakali, sababu msitu huu umepakana na mbuga kubwa ya wanyama ya serous, hivyo ata wakulima wanao lima viazi na matuna kwenye eneo hili, uwa wana ishi kwa tahadhari kubwa sana” alisema Mapombeka, na wakati huo walikuwa wanaingia kwenye eneo la mashamba, wakiona vijumba flani flani vidogo, na watu wakiwa wamekaa nje ya vijumba hivyo, wakizunguka biwi la moto wa kuni, kujikinga na baridi iliyokuwa inapuliza eneo lile, “nazani mahali hapa pata tufaha, kwa usiku waleo” alisema Mapombeka, na PC Mike akaunga mkono, ni kutokana na kuitaji sana sehemu ya kupumzika, sababu toka sakata hili limeanza, hakuwa amelala vizuri. ******
Saa Mbili kasoro, ndio muda ambao msafara wa bwana Kingarame uliingia Njombe ni baada ya kutembea kwa mwendo wa masaa matatu, “inabidi tuka report kituo cha polisi wilaya, kisha tuelekee huko Makambako” alisema Kingaarame, wakati huo Njombe ni wilaya moja wapo ya mkoa wa Iringa, na makambako ni kitongoji chake, na ilikuwa lazima areport hapo ikiwa makao makuu ya Polisi wilaya.
Msafara ulielekea moja kwamoja polisi wilaya, na kusimama mbele ya ofisi za polisi wilaya ya Njombe, ambapo SSP Manase Kingarame, alipokelewa na OC Kipanta, kwa salut, kisha akaingia ofisini kupewa maelezo na taharifa fupi, “afande kwamujibu wa koplo ambae ameleta majeruhi na mareehemu wanne mala ya mwisho, huyu jambazi ni mtu hatari sana, napengine anamafunzo ya kijeshi” alisema ocd Kipanta, lakini Kingarame nikama hakuwa amemwelewa vizuri, “ebu subiri kwanza, twende kwa hatua, hao marehemu wengine ni wepi?” aliuliza Kingarame huku akimkazia macho OCD Kipanta, “afande nazani umepishana na report ya jioni hii, ukweli ni kwamba kuna askari wengine wanne wameuwawa, na wawili wamejeruhiwa” alisema OCD Kipanta, “aiwezekana, inakuwaje mtoto mdogo .....” nusu Kingarame alopoke, lakini akajizuwia, “ukweli afande ata sisitume stushwa sana” alisema OCD Kipanta, na hapo kikapiata kimya kidogo, kisha Kingarame akauliza, “kwahi wapi karibu kutoka eneo la tukio, Makambako au hapa?” ili lilikuwa jibu lahisi kwa OCD, “hapani karibu kidogo, ata sehemu ya kulala, tumekuwekea hapa hapa Njombe, Serena Hotel,” hapo Kingarame alielewa somo, “ok! naitaji kutumia simu yako mala moja” alisema Manase Kingarame, na OCD aka mpisha ofisini, ili aongee na sehemu aliyo itaji kupiga.
Nibaada ya kupiga sehemu mbili tatu, akimwulizia Basso, mwishoe Kingarame aka mpata PC Basso, na kumpatia jukumu la kwenda nyumbani kwa Kisona, kumwangamiza kabisa, ili aacha kuwafwatilia, maana kwa jinsi walivyoongea mala mwisho pale polisi mkoa, ilionyesha wazi kuwa, Kisona anafahamu kilakitu zaidi alikuwa anatafuta ushaidi tu!, “Afande nazani tumeshachelewa, maana huyo kanali ameonekana jioni hii, akiwa anatoka nje ya mji, inasemekana anawezakuwa anaelekea Njombe” taharifa hii ilizidi kumchanganya bwana Kingarame, ambae alikatasimu kwa ghazab, “huyu mshenzi mbona amepania kuniingiza kwenye matatizo” alisema kingarame, kwa sauti ya chini huku ana jisonya kwa hasira.
Kingarame aliwaza na kuwazua kwa dakika kama mbili hivi akapata jibu, kisha akainuka na kutoka nje ya ofisi, akikutana na OCD Kipanta aliekuwa anaongea na wale askari waliotoka Songea, “hooo! afande umesha maliza” alisema OCD Kipanta “ndio bwana, ila lazima usiku huu, nikaonane na askari waliopo huko polrini” alisema Kingarame na kabla ya kuelekea huko, kwanza Kingarame akaomba kuonyeshwa hotel ambayo anatakiwa afikie, ilikuwa ni kazi ya dakika kumi, ambapo yeye alionyeshwa chumba chake pale Serena hotel Hotel pekee yenye hadhi ya juu kwa eneo hili la mji wa Njombe, (kwa kipindi hicho), akipewa chumba namba saba, kati ya vyumba kumi katika ghorofa ya tatu, ya hotel hii aya Serena, alafu askari wakaelezwa watafikia kwenye bweni la askari kaperah.
Dakika mbili baadae, tayari safari ya kwenda porini ilkaanza, huku OCD Kipanta akiongoza msafara, kwa gari lake aina ya land Rover 110, nayeyepia alikuwa na askari watatu, wenye SMG, sasa msafara ulikuwa wa magari manne mida hiyo ilikuwa saa tatu kasoro,********
Nidio mida ambayo mzee Mbogo alikuwa ana simamisha gari pembeni ya barabara, karibu kabisa na duka mmoja, lililopo kwenye safu ya maduka, ya hapa kati kati ya mji wa Njombe, “nimekubari mzee Mbogo, unauwezo mkubwa wa kukimbia na gari, ila story yako ya safari ya harusini, ilikuwa nzuri sana” alisema Kisona huku akifungua mkanda wa kwenye kiti, alicho kuwa amekalia, kisha aka geuka kidogo na kumtazama koplo Kataembo, aliekaa seat ya nyuma yake, usawa wa dereva, yani kulia mwa gari, “watu wanaweza kupata dakikatano za kuangalia maiataji” alisema kanal Kisona, kisiha aka fungua mlango wagari, “ndiyo afande” aliitikia Katembo ambae na yeye, aka waeleeza wale askari wengine, ambao licha ya kumsikia Kisona akimweleza Katembo, lakini hawakutakiwa kufanya lolote mpaka waambiwe, “haya jamani dakika tano” hapo askari wale waka shuka huku wakiwa na silaha zaoambazo walizi tundika mabegani, kilalia kifuani, “mzee Mbogo twende zetu au bado unawaza kuhusu Edgar?” alisema Kiosna baada ya kumwona mzee huyu akiwa bado ndani yagai nyuma ya usukani, “haaa! wapi, ninacho waza siyo usalama wake, ila ninacho waza ni idadi ya vifo vya polisi vitakavyo jitokeza mpaka iliswala litakapo isha” alisema mzee Mbogo huku nayeye anashuka toka kwenye gari, “ni kweli bwana Mbogo, kunakitu bado sija kuuliza, hivi inawezekana Edgar ndie anae wa angamiza hawa polisi?” aliuliza Kisona huku yeye na baba Edgar, wakielekea kwenye duka la karibu, “ndio, inawezekana endapo amepata silaha” alijibu Mbogo, na wakati huo waikuwa wamesha fika kwenye duka.
Baada ya bwana Kisona kumsalimia mkinga huyu wakiume alie kuwa anauza duka, kisha akamwuliza, “ni wapi tunaweza kupata sehemu ya kupiga simu?” hapo yule mkinga akawaelekeza, hapakuwa mbali toka dukani kwake, ni duka kama la tatu hivi, “kwa hiyo mzee unamaanisha Edga anauwezo wa kutumia silaha?” aliuliza bwana Kisona, wakati wanaelekea hapo kwenye kibanda cha kupigia simu, “tena uwezo wa hali ya juu, sababu nilimfundisha kuwinda” alijibu baba Edgar, na wakati huo walisha fika pale kwenye kibanda cha simu ambapo walimkuta mpigisha simu anajiandaa kufunga,
Kisona alipata mawasiliano na mke wake, lengo lake ni kumjulisha kuwa ameshafika Njombe, japo mke wake alishangaa sana kwa muda mfupi walio utumia, pia akamweleza ujumbe wa Rehema, hapo akamshauri kuwa ampigie simu dada huyo, ili amwleze zaidi, Kanali Kisona akakubari ushauri huo, akapiga simu kwa Rehema, ambae alimweleza kama alivyo elezwa na Lucy, “kwa hiyo inawezekana kuwa kutoka hapa Njombe ni karibu zaidi na hapo walipo?” aliuliza Kisona, “ndio japo nikama katikati ya Njombe na makambako” alijibu Rehema, baada ya kukata simu Kisona na mzee Mbogo wakashauliana, waweke kambi pale Njombe, kwa nza itawasaidia kuwakwepa wakina Kingarame, ambao wao waliamini kuwa mkuu huyo wa polisi ameenda Makambako, ata Kisona alipo alipo piga simu kwa brigedia Haule, na kumweleza uamuzi wake, nae akamuunga mkono na kumwaidi kuwajullisha wenyeji wao waliopo makambako, yani mkuu wa kambi la jeshi la ulinzi lililopo makambako, ili watakapoitaji msaada wasisite kuwasaidia, “kwahiyo itabidi mfikie hotelini, maana hapo Njombe hakuna kambi lolote la jeshi, malipo yatafanywa na Commanding officer wa Makambako” alisema Brigedia Fransis Haule. baada ya hapo mzee Mboo pia aliongea na mke wake, akimweleza kuwa wamesha fikaNjombe na wanaanza kazi ya kuwatatuta wakina Edgar, pia akamweleza kuwa endapo watapata mawasiliano ya kueleweka basi, atamjulisha, iliakitaka kupiga aweanapiga.
Ndivyo ilivyo kuwa, na hotel yenye hadhi pale Njombe, ilikuwa ni Serena hotel pekee, nao wakenda kuchukuwa vyumba mahali hapo, na mpangilio ulikuwa kama ufuatavyo, Kisona alichukuwa chumba namba Mbili cha ghorofa ya tatu, nikati ya vyumba kumi vilivyopo ghorofa ya tatu, huku mzee Mbogo nae akipewa chumba namba tatu, kwenye ghorofa hiyo hiyo ya tatu, na ya mwiisho, huku askari wengine wakipewa chumba kimoja kwa watu wawili, kwa usalama wa silaha zao, wasingeweza kulala mmoja mmoja, ambao walipewa vyumba katika jengo la chini kabisa, sijuwi ndio ghorofa ya kwanza, au safu ya kwanza, hivyo walichukuwa vyumba vitatu, namba sita, namba kumi na mbili na kumi na tano, baada yakuakikisha wamesha kagua vyumba vyao, na kuchukuwa namba za simu za hotel wakizituma kwa watu muhimu, kama familia na kwa bwana Haule, wakaenda sehemu ya chakula, na kupata chakula, huku wakipanga mikakati ya uanzaji wa kazi yao, hapo kesho, maana usiku huu waliofia kushambuliana na polisi waliopo huko porini, kwakisingizio cha kwamba, awakuwajuwa.*******
Giza lilikuwa totoloooo! baridi ilikuwa inapuliza kiuakika, mvumo wa upepo wa baridi ulisikika, ukivuma kwa fujo, huo ndio mfumo wa baridi ya MAKAMBAKO, kilicho waongoza wakina Edgar na Monalisa, ambao walikuwa wamesha vuka mto, ni kinjia chembamba kinachopandisha toka mtoni, na sasa wawili hawa waliweza kufwa njia hiyo, safari ikiwa kimya kimya, Edgar akiwa ameushka mkono wa Monalisa, kila mmoja kiugulia uchovu na njaa, huku wakiona mng’ao flani kama ishara ya kuwepo kwa moto mbele yao, ambao kwa sasa ilionyesha kuwa ulikuwa karibu,
mala wakaanza kuona dalili za kuwa wamekaribia kwenyemakazi flani ya watu, maana walinza kuona miti ya mianzi (bamboo), na migomba ya ndizi, huku mianzi hiyo ikiwa imewekewa pindande vya miti huo huo wa muanzi, mfano wa kikombe flani, (mbeta) kwalengo, la kukinga utomvu au maji maji ya mti huo, (ulanzi) yanayo tumika kama juice au wine yani pombe, ambayo wazungu wanaita, (bamboo wine, au bamboo juice) “pengine tumesha fika, nasikia kama kunasauti za watu” alisema Edgar uku akisimama na kuiweka bunduki yake mgongoni, ili kuchelea kuwatishia wenyeji wao, ambao waliitegemea uwapa msaada, hakuwa na wasi wasi na bastora yake ambayo ilikuwa kiunoni, “sijuwi watakuwa wamepika?” aliuliza Monalisa sauti yake ikionyesha kumezwa na uchovu, wakutembea ulio changanyika na njaa yakutwa nzima, hapo Edgar alicheka kicheko kidogo, kilicho mezwa na njaa, na kuishia tumboni, “kwanini wasipike, kwani wao hawali?” alisema Edgar kisha akaanza tena kutembea, huku Monalisa akiwai na kuudaka mkono wake, huku kila wapo zidi kusogea ndipo walio zidi kusikia sauti za watu wakiongea na kucheka, ikionyesha walikuwa wamechangamka sana, huku pua zao zikivuta harufu yay a nyama ya kuchoma au kubanika.
Wawili hawa walitembea hatua chache na kujikuta wametokea nyuma ya vibanda vinne ya vya nyasi, huku kati kati ya vibanda hivi, ukionekana moto mkubwa kiasi, sambamba na kelel za watu ikionyesha kuwa walikuwa wamelewa, taena itakuwa ni ulanzi, hapo wakina Edgar waka shuru kwa mungu wao, kuona wameshapata msaada japo wa chakula kwanza, na mengine yata fwata, “nyie wakinanani?” walistuliwa wakina Edgar na sauti toka nyuma yao, wote wakageuka, waka mwona mtu mmoja akiwa ameshika bunduki moja iliyotengenezwa kienyeji, mala nyingi utumika kwa uindaji haramu, tena mtu huyu alikuwa ameiweka tayari kuwa fyetulia, maana alisha waonyeshea, “sisi ni wageni huku tume potea njia” alisema Edgar haraka haraka, akijuwa kuwa lazima kuna jambo la kuchukuwa tahadhari, “tembea mbele haraka, mkileta unja nawafyetua” ilisikika ile sauti na mbaya zaidi ilikuwa ni wazi kabisa inamilikiwa na mtu alie kuwa amesha kunywa pombe, basi bila ubishi Edgar na Monalisa wakatembea, mbele waki fwata maelekezo ya yule jamaa, ambae aliwapeleka usawa wa kati kati ya vile vibanda vinne, ‘jamani tume pata wageni” alisema yule jamaa alie shikilia bunduki, akiwa nyuma ya wakina Edgar, “wageni gani tena usiku huu?” ilisikika sauti ya mtu mwingine upande huu wa ndani ya mduara wa vibanda,
Naam walipo tokeza kati kati ya vile vibanda waliweza kuona watu watano, tena wanaume walioomnekana kuwa ni majangiri, wanaoishi huku porini, kutokana mwonekano wao, “!waooooo! macho yangu au naota, mbona kama namwona malaika mbele yangu?” alisema mmoja kati ya hawa watano waliokuwa wamekaa wakiuzunguka moto, ambao ulikuwa na vichanja vilivyo tandazwa nyama juu yake, na madumu ya pombe yakiwa mbele yao, yule jamaa aliweka chini kopo la pombe na kuinuka, alioneka akiyumba yumba kwa ulevi, wakati anatembea kumfwata Monalisa, alie simama nyuma ya Edgar karibu kabisa na na uwafanya watu hawa wasiweze kuiona smg mgongoni kwa Edgar, “jamani sisi tume kuja kuomba msaada wakuonyeshwa njia ya kwenda mjini, wala atuna ugomvi na mtu” alisema Edgar, kwa sauti flani ya kuwa tahadharisha, “unataka kutufanya sisi wajinga, hapa atakiwi apajuwe mtu yoyote, unataka tuwaache alafu mhenda kutuchoma kwa polisi” alisema yule jamaa mlevi mmoja alie kuwa amsha wasogelea wakina Edga, na wenzie wakacheka kilevi levi, huku yule alie shika gobole, akienda kukaa kwenye gogo, pembeni ya moto na kujiunga nawenzake kuendelea kunywa pombe, “daa! jamani sijawai kumwona mschana mzuri kama huyu” alisema yule mlevi ambae alionekana kuwa ndie mkubwa wao, kwa sauti ya mshangao, “leo nita faidi usiku kucha” alisema tena yule jamaa, Edgar akuyapenda maneno ya yule jamaa, ambae aliinua mkono wake na kutakakushika ziwa la Monalisa, Edgar aka mdaka kiganja cha mkono, na kukibinya kwanguvu, kiasi kwamba yule jamaa akaonekana akikunja usio kwa maumivu, “mzee sidhani kama itakuwa vyema nifanye jambo baya, naomba usimguse huyu mwanamke, na utuache tuondoke kama umeshindwa kutusaidia” alisema Edgar, akiwa bado ameusikilia mkono wa yule jamaa, pasio kujuwa kuwa tayari yule mwenye bunduki alisha simama na kumwelekezea lile gobole, “Sogea pembeni we mjinga, si umetuletea mwenye demu” akika kauri hii ili mfanya Monalisa azidi kutetemeka, maana alijuwa kuwa leo inaweza kuwa ndio mala ya kwanza uingiziwa dudu, na mbaya zaidi itakuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, wakati huo Edgar ambae anawajuwa wawindaji haramu wanavyo kuwa hakiri mbovu, alijuwa ni kweli wamezamilia kufanya wanacho sema. akamtazama yule ale simama na gobole, akamwona bado ame mnyooshea bunduki, Edgar aka mwachia mkono yule jamaa alie taka kumshika ziwa Monalisa, “ebu! mchukueni huyu mpuuzi, mka mchinjilie mbali, pumbavu jambo baya jambo mbaya jambo mabaya, sasa anaenda kufanyiwa huyu demu wako” alisema yule jamaa, na hapo wakainuka wale jamaa wote, waliobakia pale kwenye gogo, na kuanza kumfuata Edgar, pasipo kujuwa kuwa Edgar alikuwa na store ya silaha mwilini mwake.... WADAU TUME KWAMA KIDOG
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments: