Je Unafahamu Faida za Maharage Mwilini? Fuatilia Hapa
Maharage ni chakula ambacho watu wengi hukichukulia kama chakula cha hadhi ya chini kisichokuwa na manufaa kiafya.
Huu ni upotoshaji, kwani maharage yana faida nyingi sana mwilini ambazo watu wasiokula maharage wanazikosa.
Hizi hapa faida 9 za kula maharage, fahamu zaidi.
1. Hupunguza lehemu (cholesterol)Moja kati ya vyakula vinavyopunguza lehemu mwilini ni maharage. Nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye maharage hujishikiza na lehemu ziwapo tumboni na kuzuia lehemu zaidi kufyonzwa mwilini.
2. Huzuia sarataniMaharage ni chakula chenye madini ya manganese pamoja na vitamini K ambavyo vyote kwa pamoja huzuia kuharibika kwa seli kunakosababisha saratani.
3. Huboresha afya ya ubongoKemikali ya thiamine pamoja na vitamini K zinazopatikana kwenye maharage husaidia katika kuboresha afya ya ubongo.
4. Hutawala kiwango cha sukari mwiliniMaharage yana nyuzi nyuzi ambazo hupunguza kiwango cha metaboli cha wanga (carbohydrates) mwilini. Kwa kufanya hivi huwezesha kutawala kuongezeka kwa kiwango cha sukari hasa baada ya kula chakula. Maharage pia yana protini ambayo husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini.
5. Huongeza nguvu za mwiliKuwepo kwa madini ya chuma pamoja na manganese kwenye maharage kunayafanya kuwa na nafasi kubwa katika kuongeza nguvu za mwili.
Madini haya ni muhimu sana katika kuuongezea na kuupa mwili nguvu.
6. Huimarisha mifupaMadini ya calcium pamoja na manganese ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya mifupa. Maharage ni chanzo kimojawapo kizuri cha madini haya.
7. Huboresha ngoziMaharage husaidia michakato ya metaboli ya asidi ya amino, gluconeogenesis, neurotransmitter synthesis, histamine synthesis, asidi ya mafuta (fatty acids), lipids and hemoglobin synthesis kwenda vizuri.
Ikumbukwe kuwa hivi vyote vina nafasi kubwa katika kuboresha afya ya ngozi.
8. Huboresha afya ya moyoAina nyingi za maharage zina vitamini B9 (folate au folic acid) ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya misuli ya moyo.
9. Huboresha afya ya machoMadini ya zinc yanayopatikana kwenye maharage ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya macho. Hivyo ulaji wa maharage mara kwa mara utaboresha afya ya macho yako.
10. Huboresha uwezo wa kumbukumbuKama nilivyotangulia kusema kuwa maharage huboresha afya ya ubongo, uwezo wa kumbukumbu huboreshwa pia kupitia ulaji wa maharage.
Vitamini B1 inayopatikana kwenye aina mbalimbali za maharage hukabili ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer’s na dementia).
11. Huondoa sumu mwiliniVyakula vingi vya viwandani huhifadhiwa kwa kutumia vihifadhi vyenye sulphites; Sulphites inapozidi mwilini ni sumu. Hivyo basi kemikali ya molybdenum inayopatikana kwenye maharage inasaidia kuondoa sumu ya sulphites mwilini.
12. Hukabili shinikizo la damuKama tulivyoeleza kwenye makala nyingine, potassium, magnesium pamaoja na protini husaidia sana kukabili shinikizo la juu la damu. Maharage hukabili shinikizo la damu kwa kuwa ni chanzo kizuri cha potassium, magnesium pamoja na protini.
13. Hupunguza uzitoVyakula kama maharage vina nyuzinyuzi zinazokuwezesha usihisi njaa mapema, hivyo kuepuka kula mara kwa mara na kusababisha kuongeza uzito wako.
Ikumbukwe pia maharage ni chakula ambacho kina kiwango kidogo cha mafuta (fat), hivyo hakisababishi uzito mkubwa wa mwili.
14. Husaidia kutibu tatizo la kutokupata chooKama nilivyoeleza kwenye hoja zilizopita, maharage ni chakula chenye nyuzinyuzi kwa wingi; ikumbukwe kuwa vyakula vyenye nyuzinyuzi ni tiba bora ya tatizo la kutokupata choo.
15. Husafisha tumboWakati baadhi ya watu wakiyachukulia maharage kama kitu kinachovuruga tumbo, maharage yana nafasi kubwa kwenye afya ya tumbo.
Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa kula maharage kwa kiasi cha kutosha kutasafisha tumbo lako na kukukinga na maradhi ya saratani ya utumbo (colon cancer).
16. Husaidia kukabili maradhi ya asthmaUtafiti uliofanyika ulibaini kuwa kuna uhusiano kati ya upungufu wa madini ya magnesium na kutokea kwa maradhi ya asthma. Kutokana na maharage kuwa na kiwango kizuri cha madini ya magnesium, basi yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kukabili maradhi haya.
17. Huboresha na kukomaza seli nyekundu za damuVirutubisho vilivyoko kwenye maharage husaidia katika maendeleo na ukomavu wa seli nyekundu za damu.
18. Huzuia kuzeeka mapemaKuzeeka mapema? Ndiyo, kutokana na maharage kuwa na kemikali zinazozuia kuchakaa kwa seli za mwili, yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuzuia kuzeeka mapema.
19. Huboresha afya ya kucha na nyweleBiotin, madini ya chuma pamoja na protini vinavyopatikana kwenye maharage vina nafasi kubwa katika kukupa kucha imara pamoja na nywele zenye afya njema.
Je bado huoni umuhimu wa maharage katika afya ya mwili wako. Anza kula maharage uboreshe afya ya mwili wako sasa. Ikizingatiwa kuwa maharage ni chakula kinachopatikana kwa bei rahisi tofauti na vyakula vingine kama vile nyama na samaki, hivyo huna kisingizio chochote.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: