KWA NINI WANAUME WANAKUWA WASALITI KWENYE NDOA?

Wanaume kutoka nje ya ndoa si kwa sababu wake zao ni wabaya au hawako smart, haana. wanawake wengine ni wazuri sana na wako smart kabisa , ni nini basi huwapelekea wanaume kutoka nje ya ndoa.
wanawake wanao mpango mkubwa na mzuri wa kudumisha ndoa zao,lakini kuna mambo ambayo hata wao huwa hawaelewi ni kwa nini hali kama hio hutokea .tuangalie hizi maana mbili za kwa nini wanaume hufanya hivyo.
-kati ya wanaume 3 kati yao mmoja anatoka nje ya ndoa , na hapa hakuna mwanamke anaejua kuwa mwanaume anatoka nje ya ndoa yao.
-asilimia 92 wanasema kuwa kutoka nje ya ndoa sio kwenda kufanya ngono, ila io sababu kubwa inayofanya kutoka nje ya ndoa.
KWA NINI WANAUME WANACHEAT.
images-11 KWA NINI WANAUME WANAKUWA WASALITI KWENYE NDOA?.
Wanaume wanatoka nje ya ndoa kwa sababu zifuatazo,
_upweke wanaopata ndani ya mahusiano yao na ndoa zao
_Uthibitisho unatoka kwa wanawake wengine
_hakuna utulivu wa kutosha nyumbani.
_wanaona kama hawajaliwi na wake zao.
Wanawake ambao wana wanaume wanaocheat, yaani wale wanaowapokea wanaume wa watu hujua sababu ya yule mume kufika kwake, kwa hio huchukulia hio faida ya kumfanya ajisikie kukamilika. atamfanya awe na furaha, ajione ni mwenye thamani na ni mtu anayekubalika na ni mshindi .kwa hio hupata vile ambavyo hapati kule nyumbani.
Kama umewahi kumuona mwanaume anayecheat , angalia familia yake , watoto wake , mke wake na ndugu zake jinsi wananavyokosa mapenzi yake na msaada kutoka kwake. huhamishia mapenzi kwa yule anaeona kuwa ndie mtu pekee wa kumpa furaha na amani.
DALILI ZA MWANAUME ANAYECHEAT.
1.mke mwenye mume wa aina hio atamgundua , maana huwa hana hisia kwake, na huwa anamwepuka mke wake ili asije kuwa na hisia nae.
2.Anakuwa na maneno mengi yasiokuwa na sababu , ugomvi ugomvi tuu.
3.Anakuwa hana hamu tena na mke wake kama ilivyokuwa pale kwanza.
4. Anakuwa ni mwenye gubu kila siku mara umefanya kile na kile.
5.Hakai nyumbani , na huchelewa kurudi na hata asirudi kabisa.
UTATA ULIOPO KATIKA UKWELI KUHUSU KUCHEAT.
Watu wengi wanasema kuwa mwanamke ndio anaesababisha mwanamume kuwa mdanganyifu ndani ya ndoa. kwa sababu mwanamke ndio mjenzi wa ndoa , akilala yeye kila kitu kinaharibika, . lakini ia kuna wengine wanasema sio mwanamke anaesababisha haysa mambo yatokee. hili sio suala la mchezo. maana hapo ni kulaum upande mmoja.
Wanawake wengi hufikiri kuwa nikimwonyesha mume mapenzi na kumjali sana atakuwa hafanye kazi zingine za hapa ndani au hata kumsaidia watoto, hio sio kweli hayo ni kinyume chake.
Unapomheshimu mume na kumpenda na kumjali na kumheshimu , mume atakupenda na kukuthamini zaidi na atakaa nyumbani upendavyo , na atakusaidia kazi hata zile ambazo hukutegemea kuwa atazifanya. maana anakujali na kukupenda kama wewe unavyompenda.
UNAWEZA KUNIAMBIA NI WANAUME WANGAPI HUWAACHA WAKE ZAO NA KUWACHUKUA WANAWAKE WAREMBO?
BINAFSI NAONA HAKUNA.
Mwanamume mmoja alisema kuwa nina wanawake wengi tena ni warembo ninaotoka nao, lakini sio warembo kama mke wake, hakuna aliemzidi mke wake.
Mwingine akasema wanawake ninaotoka nao hata sio wazuri na hawana maumbo mazuri kama umbo la mke wake.
sasa hapo uelewe kuwa wanaume hawaendi nje ya ndoa kwa ajili ya kumchukia mke wake au kwa ajili ya kuwa na wake wabaya , na wala hawatoki nje ili kutimiza haja zao, wanaenda kutafuta amani na kutaka kuthaminiwa na kujiona washindi, ndivyo wanavyopenda katika maisha yao ya mahusiano na ndoa.
Wanaume wanadanganya kwa sababu hisia zao huotea ndani ya ndoa na mahusiano yao, mume huhisi kutokukubalika na anakuwa ni mtu mwenye mawazo na hupata upweke mkubwa ndani ya ndoa.ndio maana huenda kwa wale wanaoziba yale mapengo yaliopotea. wanaume wana hisia za kuonekana na kuishi.
Lakini pia kuna wanaume wanaotoka kwenye ndoa , haijalishi hata kama unamjasli na kumpenda na kumthamini kwa namna gani , hawa wana mapungufu fulani ndani ya akili zao na huwa hawajuti kwa kufanya kitendo hicho , hujiona wako sahihi. na hii husababisha matatizo ndani ya ndoa,
Kuna mwanamume mwingine ukimkamata huwa anakubali kuwa amecheat, na huwa wepersi wa kuomba msamaha pale tu wanapoona wamekamatwa, hujirekebisha na kurudi kwenye mstari.
Kumbuka kuwa kudanganya ndani ya ndoa na mahusiano inaumiza sana, na hayo maaumivu huchukua muda mrefu kupona. ni bora basi wanaume kujitahidi kuwa waaminifu ndani ya ndoa na mahusiano yao. kuna wanawake nao hucheat lakini ni mmoja kati ya 100.
Nakukaribisha kutoa maoni yako. siwezi kukupa ushauri wowote wa kufanya naamini mume wako hacheat,na kama anatoka ndani ya ndoa nakuombea kwamungu upate njia nzuri ya kumrekebisha.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.