USHAURI: Jinsi ya kuweza kuhifadhi pesa kutoka katika mshahara

Wakuu naomba ushauri wenu.


Nawezaje kuokoa walau pesa kadhaa kutoka ktk mshahara wangu? Ninapokea laki sita na nusu tu na nipo single sijapanga ninaishi home.

Home hawanitegemei hata kwa shilingi mia yangu ila najikuta matumizi yangu ni mabovu at the end nashindwa hata kuokoa walau hata laki mbili kwa kila mwezi!

Ushauri wenu tafadhali!

NB: Sinywi pombe wala sina hawala wa kunichuna but nashangaa tu haka kahela kanavyopukutika wakuu

Mdau mwingine akiomba ushauri

PipiJojo said;

Habari zenu.
Mimi ni mwajiriwa (private sector), mbali na mshahara wangu, kwasiku siwezi kukosa hata elfu10. Tatizo ni kwamba suala la kujiwekea Akiba linanipa shida... Nikikaa na hela lazima nitumie tuu yani hata kwa vitu ambavyo sio muhimu at that time. Nimejaribu kuweka kwenye simu bado ni mwendo wa kujiunga tuu Na Bundle.

Sielewi ni tamaa au sijapata njia sahihi za kujiwekea akiba pengine.
Naombeni ushauri ndgu pengine ni njia zipi nitumie angalau niweze kujiwekea hata elfu moja kwa siku.

============
USHAURI KUTOKA KWA WADAU:
============
Mdau 1:


Fungua savings account ambayo hutaweza kutoa pesa kuzidi certain limit in a year or month. Kisha hakikisha kila mwezi unatoa kiasi cha fedha (kiwe fixed e.g laki au elfu 50) kutoka kwenye mshahara (account inayosave mshahara eg deposit account ) na kupeleka kwenye hiyo savings account. Uliza kama bank yako wanaweza kufanya hivyo automatically bila ya wewe kufanya hivyo personally.

Goodluck
Mdau 2:

Mdau 3:

Mdau 4:

Njia nyingine nzuri ni kuingia vikoba au vikundi vya savings. Vinafundisha sana discipline ya kutumia hela coz kila mwezi lazima uweke pesa kiasi flank mnakua kikundi cha watu 10-20.Na kupitia savings zenu mnaweza kopeshana kwa riba .mimi niko na vikundi 3 kimoja kila mwezi 50 thou kingine 200 thou na kingine 10 thou yani mshahara ukiingia tu najua 260,000 sio yangu.... and it's worth it coz mwishoni mkiamua kugawana unafanya kitu cha maana Sana
Mdau 5:
Weka akiba lakini pia tujifunze kuwa na tabia ya kuwekeza kile tunachokihifadhi ili kizae zaidi....ununuzi wa hisa ni moja ya njia nzuri na nyepesi ya kuwekeza cha msingi kuchagua kampuni sahihi ya kununua hisa...nilinunua hisa za swissport miezi sita iliyopita na Ieo thamani yake imepanda kwa karibu 90%....njia hii inawafaa sana watu ambao hawana muda wa kutosha wa kusimamia biashara zao wenyewe au ni waoga kufungua biashara zao wenyewe....ukitaka maelezo zaidi kuhusu hisa unaweza kuni-pm but zinalipa sana....kwa kipato chako cha laki sita unaweza ukawa unanunua hisa za laki moja,mbili hata tatu kila mwezi na baada ya muda utakuwa mbali sana.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.