Mara nyingine Maisha ya Ndoa ni Vita! Huyu jamaa sijui nimfanyeje


Nawasalimu sana Wakuu.
Straight to the point.!!
Nimeoa takribani miaka 9 imepita sasa.
Nikiri sijawahi kuwa na mgogoro mkuubwa kivile kwenye ndoa yangu. Zaidi ya zile confusion za hapa na pale.

Mke wangu anafanya kazi kwenye moja ya taasisi ya Afya, ya serikali.
Sehemu ambayo alianza kazi, miezi miwili tu! Baada ya kumuoa.

Namwamini sana wife wangu kwa kweli, ila kuna utata umeibuka over recently na ndio maana naandika hapa, kuongezewa hekima na Busara kutoka kwa wazoefu wa hii taasisi takatifu inayoitwa Ndoa.

Kuna jamaa anafanya kazi na mke wangu ila department tofauti na ninafahamu kuwa wanafahamiana tokea mwanzo as long as wamesoma pamoja, sema huyu jamaa alimtangulia wife kidogo.
Na ni mtu tunayejuana ila hatuna mazoea kivile.

Shida inaanzia hapa huyu jamaa alimwomba wife, amsaidie pesa kidogo 1.5M kwa minajili yakumrudishia ndani ya siku chache na baada yakujieleza vizuri juu ya hilo hitaji lake wife hakuweza kumpatia yote so alimpa 900k, bila kunishirikisha akiamini jamaa hawezi kuacha kumrudishia.

Zikapita siku kadhaa, jamaa kimya, ikapita mwezi kimya!
Ikabidi wife amuulize, jamaa akaanza kupiga chenga. Nakutoa sababu zisizo na maana tena.
Hiyo pesa wife aliitoa kwenye akaunti yake, binafsi sikushtuka mapema.

Duuh, jamaa anaanza kumchombeza wife, kwa kumpiga sound za hapa na pale, mara anamwambia akitoka job aipitie hiyo pesa sijui lodge gani huko. Alijua kabisa wife hakunishirikisha kwenye ile pesa so hawezi kuniambia...

Juzi kati hapa wife alivyoona mizinguo inazidi ikabidi anipe picha kamili na misamaha mingi, simply kwasababu alimheshimu yule jamaa ambaye alikuwa anamwita Kaka.

Sijaamua kuingilia kati bado ila nimemwambia wife, awe serious kidogo hiyo pesa ipatikane, na nimeanza kumfuatilia huyu jamaa ili nimfahamu zaidi uwezo wake ili nijue nikiingilia kati nitampa adhabu gani...

Huu ni utapeli, kwa kweli.
Nahitaji hekima na busara zenu juu ya hili jambo wadau.

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.