Kuna baadhi ya wanaume tuna roho za kishetani, leo mpaka nimetoa machozi kwa huyu dada

Kuna baadhi ya wanaume tuna roho za kishetani, leo mpaka nimetoa machozi kwa huyu dada

Hey Pals,,,

I hope mko good Ryt,,,,

okay Freshhhhh

Leo niliamua nipite Igunga kumsalimia Bibi nikiwa nimetoka zangu Dar,

Hapa kwa bibi naweza sema ni sehemu ambayo nimefanyia likizo zangu zote,kuanzia primary,O-Levo,Advance na Chuo,Hapa kwa bibi kulikuwa na wapangaji kibao,Ila alikuwepo jamaa mmoja ambaye alikuwa na mke wake,kipindi hicho walikuwa hawaja bahatika kupata Mtoto,

Huyu jamaa na mke wake licha ya kuwa wapangaji hapa kwa bibi ila bibi yangu aliamua kuwafanya kama watoto wake,Hali iliyo pelekea kuzoeana na Mimi,

Huyu jamaa alikuwa na maisha magumu sana,kuna kipindi walikuwa wanashinda bila kula,si chai wala lunch,Mara nyingi walikuwa hawataki mtu ajue kama Wame shinda bila kula,Ila kama nipo nilikuwa namfikishia habari bibi na kuwapa kama ni debe la mahindi na dagaa au nswalu(kwa wakaz wa tabora wanajua nswalu),

Kuna kipindi maisha yalikuwa magumu Ikabidi huyu mke wa jamaa amwombe bibi mtaji ili aanze kutembeza mboga mboga,Alitembeza mboga mboga kwa muda wa wiki Ikabidi bibi amwonee huruma akampa baiskeli ili awe anaitumia kutembezea mboga mboga,

Baada ya kufanya kaz hyo ndani ya mwezi akamwomba bibi anunue mbuzi aweke kwenye zizi la hapa nyumbani,bila hiyana bibi akamkubalia,ndani ya miezi minne huyu Dada alikuwa kanunua mbuzi 6 wadogo wadogo,Ilikuwa kila akitoka kutembeza mboga ni lazima umkute anachunga mbuzi wake hapa kwenye uwanja wa bibi,

Ikumbukwe huyu jamaa hakuwa na kazi zaidi ya kupiga dei waka kwenye malori ya mchanga,na huku Igunga alikuja baada ya kuoa kwa dhumuni la kuja kutafuta maisha,

Baada ya Hao mbuzi kukua na kuwa wakubwa kidogo walishauriana wauze ili wafanye biashara ya kuuza matunda,na kweli walifanya hiyo biashara ya matunda,Ndani ya muda mfupi tu walifanikiwa,Ikabidi wagawane majukumu,Mume wake Ikabidi awe ananunua nguo na kupeleka vijijini kuuza huku mke wake akiendelea na biashara ya matunda kwa kutembeza na toroli,

Mimi niliishia hapo wakiwa wanafanya biashara hzo za matunda na nguo,sikuwahi kukutana nao tena mpaka ilipo fika 2016 baada ya kumaliza chuo ndo nikakutana nao pale Igunga sokoni wakiwa na Duka kubwa la vitambaa huku huyu dada akiwa ni fundi cherehani hapo hapo dukani,Kusema ukweli sikuamini kama wameweza kufikia hatua ile coz lilikuwa ni bonge la duka,na wauzaji walikuwa ni wao wenyewe mke na mume pamoja na Dada mwingine ambaye nilitambulishwa kama msaidizi wao,

Baada ya kutoka pale dukani nilirudi kwa bibi ndo akanihadithia mkanda mzima mpaka kupelekea hawa wana ndoa kufanikiwa,Bibi yeye anadai mafanikio Yale ni mwanamke ndo kafanya,na hili halina ubishi kwa kweli,

Toka mwaka huo 2016 sikuwahi Kupita Igunga na kulala,ila nilikuwa napita na kumpitishia bibi mazaga then mimi nanyanyua chuma naondoka zangu,

Jana nikiwa nimetoka zangu Dar,Nimefika Dom chuma kikaleta uchokozi,So Ikabidi nilale Dom,Niliamka alfajiri ili niendelee na safari,Lakini nilivyo fika Igunga Ikabidi bibi anilazimishe kulala cz nimefika mapema so ni lazima nitie baraka,Ikabidi nikubali kulala ili kesho ndo niendelee na safari ya Mwanza,

Mida ya saa kumi jioni Ikabidi bibi anambie twende sokoni,bila kutegemea akawa amenipeleka kwa hawa wapangaji,Nilisalimiana nao vizuri tu ila nilimwona huyu mke wa jamaa kachakaa huku aki endelea na kazi ya cherehani yake,Lakini licha ya kuchakaa ila jamaa yeye yuko smart tu na Duka ndo limezidi kuwa kubwa zaidi,

Tukiwa tumekaa pale kwenye kiti na bibi yangu,Huyu Dada aliletewa nguo na Mteja amwekee kiraka,Kabla hajapokea nguo hyo nilishangaa mume wake ana ropoka "Una endelea kupokea hayo manguo,Sisi tunataka tufunge tuondoke" Nikajiuliza huyu jamaa hii jeuri katoa wapi! Huyu Dada akamsihi mume wake amvumilie angalau Hata dakika tano ili amwekee kiraka mteja wake angalau apate hela ya kuhemea watoto wale,Huyu dada cherehani huwa anahifadhi dukan ndo mana akaomba avumiliwe,Jamaa alikataa na kufunga duka na kutuacha huku tumekaa pale,Huyu Dada kalia kama Mtoto mdogo huku akitulaumu wanaume.

Tumekaa pale Ikabidi bibi amwulize,Mbona umesema akupe dakika tano ili ushone kiraka upate hela ya kuhemea watoto wale,ina maana bila kushona watoto hawali? huyu Dada katoa jibu lililo ambatana na kilio kizito "Kaoa mwanamke mwingine yule ambaye kaondoka naye" Huyu Dada kaongea vitu vingi mpaka Mimi mwenyew nimelia kama Mtoto mdogo,Imagine huyu jamaa kaoa mwanamke mwingine kamjengea jumba kubwa na huyu mke mkubwa anaishi kwenye kajumba kadogo ka-Slope na watoto wake wawili,in short katelekezwa,

Huyu mke mkubwa kwenye hilo duka haingii tena,yeye anaishia hapo mbele kwenye cherehani yake,na Huyo mke mdogo ndo anasimamia kila kitu saivi,na tayari huyu mke mdogo ana Mtoto tayari,

Kilicho kuja kuniliza zaidi ni baada ya kumwona huyu Dada na Mtoto wake mgongoni akienda kuomba duka la jirani ahifadhiwe cherehani,Mtoto wa watu karudi kubeba cherehani huku analia na makamasi juu,Ikabidi nimsaidie kubeba,huyu Dada kaliza kila mtu aliyekuwepo pale,Bibi kaamua amchukue tu aanze upya tena maisha yake.

Wanaume kwa hili hapana aisee,Nimeumia sana.

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.