Mahusiano ya kimapenzi kwa wanafunzi wa sekondari

Wakuu, hii imekaaje?


Ni kwanini wanafunzi wa sekondari hasa kuanzia kidato cha nne, tano na sita wasifundishwe kuwa na mahusiano salama huko mashuleni?

Kuna rafiki yangu na ndugu yangu wa karibu, aliniomba nipite shule anayosoma binti yake Lushoto, nimefika shuleni binti ndio yuko kidato cha sita. Nikajitambulisha kama mzazi wake. Akaulizwa mimi ni nani akasema baba mdogo, tukaingia kwenye kikao cha nidhamu.

Binti akasomewa mashtaka kuwa ana mahusiano na mwanafunzi mwenzake wa kiume wa kidato hicho hicho ila michepuo tofauti, ilikuwa kinyume na taratibu za shule. Binti akakubali makosa yake, na akaelezea namna walivyoanza kuhusiana.

Ilibidi kwa pale niwe upande wa walimu ili kubalance mambo, ila baada ya kutangaziwa adhabu, niliomba kuzungumza na hiyo kamati. Binafsi nilishangaa sana walimu kukomaa na kesi ya mahusiano kwa vijana wakubwa.

Ni kwanini isitafutwe njia nzuri za kuweza kuwa na mahusiano yasiyokuwa na hasara kwa hawa vijana wetu?

Na kama hizi shule hazitaki wahusiane mbona wanawachanganya wavulana na wasichana?

Zamani tulipigwa vita sana kwenye hizi habari za pair, naona kwa sasa mambo yamebadilika sana, ni vizuri hawa vijana wakafundishwa tu, kutokujihusisha na vitendo vya uasherati, ila haya mambo ya girlfriend na boyfriend wawaachie tu!!

Au mimi ndio sielewi?

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.