HIZI HAPA HATUA ZA KUZUNGUMZA NA MPENZI WAKO ALIYEKASILIKA


Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana,,kukasilishana,,katika hali ya kawaida kipindi hiki huwa ni za hatari kwasababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha,,,sote tunajua watu hupigana,huachana,,hujeruhiana,hutukanana,,hudhalilishana,wakiwa na hasira,,wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya,,, 
Msomaji wangu emu jaribu ugomvi mmoja uliowahi kutokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza,,,utabaini kuwa mlianza kama matani na mwisho mkafura kwa hasira,mkatwangana makonde,,mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana,, 
Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo,,ingekuwa mmoja wenu hasa yule wa pili kukasilika  anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasilika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi 
TAZAMA HATUA ZA KUZUNGUMZA NA MPENZI ALIYEKASILIKA. 
MPUNGUZE MHEMKO 
Hasira hujaza kifua,,huathiri mzunguko wa damu na ufahamu,,mtu aliyekasilika huwa ni vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu,,mwenye hasira huwa hafikiri matokeo yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au mapambano 
Katika hali ya namna hiyo,akija mtu mwingine mwenye busara kutaka kumgeuzaharaka haraka hawezi kumuelewa,,muhimu hapo ni kuacha kumwandama,,kuacha kujibizana nae,,Kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo,,abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake"basi mpenzi mwenye makosa ni Mimi "kauli za namna hii zitampunguza hasira kwani atajiona mshindi. 
MSOME SAIKOLOJIA YAKE 
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kama amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida,,,,ukishafahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikolojia ili kujua kama yupo kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati akiwa na hasira .



(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.