SIMULIZI; Sitaisahau Tanga (sehemu Ya 13)
Nikawa nimenyong'onyea kupita maelezo, nikaanza kujisogeza
pale alipo yule mtu mwenye panga. Huku nikizidi kutetemeka.
Nilipofika pale nikajilaza chini yani tayari kwa kuchinjwa,
nikashangaa muda unapita bila ya kusikia panga likipita kwenye shingo yangu,
mara gafla nikashikwa kichwa kugeuka nakutana uso kwa uso na mwanamke mrembo
sana, akaniamuru niinuke pale machinjioni nami nikainuka akaniamuru nimfate
nami nikafanya hivyo.
Nilienda naye mpaka kwenye chumba ambacho hakikuwa na kitu
chochote ndani, akaniuliza,
"unajua kwanini nimekuleta humu?"
Nikatikisa kichwa nikiashiria kwamba sijui sababu ya mimi
kuwa humo, mara gafla yule mwanamke akayeyuka na kupotea nikabaki peke yangu
kwenye kile chumba.
Nikawa natetemeka kwani chumba chenyewe hakikueleweka mara
kiwe na rangi nyekundu mara blue mara nyeusi ila ilikuwa ikija rangi nyeusi
mule ndani kunatisha sana.
Nikiwa bado sijielewi elewi akaja yule binti wa kitanga na
kuanza kuniongelesha,
BINTI: Je unajutia kuwa na mimi?
Nikaonyesha ishara ya ndio kuwa najutia.
BINTI: Unadhani unaweza kuniepuka maishani mwako?
Sikujua kama nikubalia au nikatae nikabaki kutoa macho tu.
Akanishika mkono nikatoka nae nje, akanipeleka mahali kwenye
dimbwi ila dimbwi hilo lilijaa damu, akaonyesha kwa kidole,
"umeona juisi ninayopenda?"
Nikatikisa kichwa kuwa nimeona, basi akanishika mkono na
tukarudi tulipotoka, akaniambia,
"nataka ukaniletee ile juisi ninywe"
Akanikabidhi kikabu nikabebee ile juisi, akanionyesha ndoo
iliyokaribu nae kuwa niijaze, sikuweza kuhoji zaidi ya kubeba kile kikapu hadi
kwenye lile dimbwi, nikataka kuchota nikakutana na tangazo,
"HAIRUHUSIWI KUANGUSHA HATA TONE MOJA CHINI"
Nikawaza sasa nitabebaje na kile kikapu maana kila
nikikijaza na kukiinua juu damu ile ambayo ilikuwa nyepesi kama maji
ilimwagika.
Nikaamua kurudi na hata kikapu nikakiacha hapo kwa kuogopa
kuangusha hayo matone.
Nilipofika kwa yule binti akachukia sana,
"mbona hujaleta nilichokuagiza?"
Nilimuangalia tu na ukizingatia mahali hapo sikuwa na uwezo
wa kuzungumza, gafla mambo hapo hapo yakabadilika kwani nikajikuta nipo peke
yangu sehemu yenye giza nene sina pa kwenda wala kupapasa wakati nashangaa hayo
mara kukabadilika tena nikamuona mmama mbele yangu akipika chakula ila mkono
wake ndio aliutumia kama mwiko wa kupikia chakula, nikawa nimetoa macho naye
akaniuliza,
"unashangaa nini? Jishangae wewe unaetaka kujitoa
kafara mwenyewe"
Bado nilikuwa nikishangaa laiti kama ningekuwa na uwezo wa
kuongea hapo ningesema mengi.
Nikamwona yule mama akiwa makini na kazi zake na wala
hakuogopa moto, akaniuliza,
"unahitaji chakula?"
Nikaitikia kwa kichwa kuwa nahitaji, akaenda na kuniletea
sinia ambalo limejaa minyoo, mmh nilipatwa na kinyaa cha ajabu huku nikijisemea
moyoni mmh hadi minyoo ni chakula! Sikuweza kula kwakweli.
Yule mama akawa anacheka sana, akaniuliza tena,
"unapapenda huku?"
Nikatikisha kichwa kuashiria kuwa kule sipapendi, yule mama
akacheka sana, na akauliza tena
"unataka kurudi ulipotoka?"
Nikaonyesha ishara kuwa nahitaji kurudi, akaniambia tena,
"nikuonyeshe njia?"
Nikaonyesha ishara ya ndio. Akauliza tena,
"je utaweza kukwepa vishawishi?"
Nikaonyesha ishara kuwa naweza, akachukua yale mavitu
anayopika na kunimwagia usoni, nilihisi kama vile sura inatoka, maumivu
niliyoyapata hayaelezeki nilijikuta nikigalagala chini kama mtoto mdogo.
Nililia sana huku yule mmama akicheka sana.
Maumivu yalipopungua yule mmama alinishika mkono na
kunipeleka mpaka pale kwenye dimbwi la damu akaniamuru ninawe ile damu usoni
nami nikafanya hivyo kuja kushtukia nilijikuta nipo kwenye chumba na yule mdada
mrembo aliyeniokoa kwenye kuchinjwa.
Nikiwa naye mule ndani, akawa ananifanyia visa kama vile
mwanamke afanyavyo mitego kwa mwanaume kwakweli sikutamani hata mwanamke wa
aina yoyote, alifanya vitu vingi ila nilimwangalia tu.
Akanisogelea na kuniuliza,
"unanienda au hunipendi?"
Nikabaki nimemkodolea macho tu hata nisijue cha kumwambia.
Naye akazidi kuniangalia nahisi alikuwa akiipima akili yangu, akaniuliza tena,
"unanipenda?"
Nikamwangalia tu, nikaamua kutikisa kichwa nikiashiria
simpendi, mara yule mdada akageuka kuwa joka kubwa, nikaanza kuogopa na
kukimbia, nikakimbia sana ila kila nikiangalia nyuma lile joka nalo lilizidi
kunikimbiza, nilikimbia hadi nguvu ziliniishia nikaanguka kuangalia naona lile
joka limekuwa na vichwa saba tena likizidi kunikaribia
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: