Mambo Ya Kufanya Na Kuepuka Ukipata Boyfriend Mpya
Kuingia katika mahusiano si jambo rahisi. Na sasa kwa kuwa umepata boyfriend mpya, si jambo zuri kuharibu kila kitu kwa wakati mmoja.
Lakini kwa kuwa Nesi Mapenzi iko hapa, naamini kuwa hutakuwa na changamoto zozote ambazo zinaweza kukukumba.
Kuwa na boyfriend mpya kuna raha zake. Huwa ni raha tupu. Utakuwa na muda mwingi wa kuweza kujuana na yeye na kila kitu kipya kumhusu. Na iwapo utagundua kuwa unampenda basi utataka kuishi na yeye kwa muda mrefu.
Mambo ya kufanya ukipata mwanaume ama boyfriend mpya
Kwa kawaida huwa tunapenda kuyafanya mahusiano yetu mapya kama ni mayai, tunaogopa yasije yakavunjika. Lakini ukweli ni kuwa ukiwa katika mahusiano mapya hupaswi kubadilika na kutatiza maisha yako ya kawaida. Wengi wetu wakiingia katika mahusiano mapya wanaogopa kuongea ama kufanya mambo ambayo wamezoea. Huwa wanaogopa kuwa wanaweza kuvunja mahusiano. Lakini ukibadilisha maisha yako kuna furaha gani ndani yake?
Halafu pia kama hutakuwa na uwezo wa kuwa huru katika mahusiano mapya utakuwa unaleta shida. So leo katika chapisho hili tumekuja na mwongozo wa mambo ya kufanya na kuepuka ukipata boyfriend mpya.
Usiwe na woga. Fuata huu mwongozo.
#1 Usiharakishe.
Najua hili si jambo rahisi kutimiza. Pindi mtu anapoingia katika mahusiano mapya huwa anataka kurukia ndani mzima mzima bila hata kufikiria chochote zaidi. Lakini swali linakuja pale pa, “mbona uharakishe?”
Shikilia pale pa mahusiano ya kudeti kwanza. Itafikia wakati ambapo mtalalana hadi mchoke. So ngojea kwanza. Usimvulie chochote. Huu ni mwanzo tu. Kwanza jenga mapenzi yenu yawe ya nguvu zaidi.
#2 Usimakinike na kumbadilisha.
Najua utakuwa unampenda, na unatamani umfanye wako daima. Lakini huu si wakati wake. Muda bado uko wa kufanya hayo. Kwa sasa wewe jifurahishe na yale ambayo ni muhimu. Cheka naye na umzuzue kadri uwezavyo. [Soma: Hatua za kutambua kama mpenzi wako amekamilika]
#3 Wasiliana na yeye vizuri.
Mawasiliano ni muhimu kama unataka kujenga nguzo thabiti katika mahusiano yenu ambayo bado ni machanga. Hivyo basi kama unataka kumueleza jambo lolote ambalo linakutatiza, ni vizuri umweleze ana kwa ana na wala usimtumie sms ama kumpigia simu. Jaribu kutafuta mbinu ya mawasiliano ambayo yanafaa.
#4 Usizungumze kuhusu mpenzi wako wa zamani.
Kutakuwa na wakati wake wa kuongea kuhusu ex wako. Lakini kwa sasa hili si jambo muhimu. Kumbuka huyu ni boyfriend wako mpya. Na ukiwa unaongea kuhusu mahusiano yako yaliyotangulia basi anaweza kushuku kuwa bado akili yako iko kwa mwingine. Jambo la kufanya ni kuepuka kabisia na mazungumzo haya.
#5 Usiwasahau marafiki zako na familia yako.
Jambo hili hufanyika. Pindi unapokuwa katika mahusiano mapya, kila kitu kingine kinasahaulika. Lakini haifai kuwa hivi. Marafiki zako na familia yako iko na itabaki kuwapo. So usiwapuuze. Kwa kuwa tayari umeingia katika mahusiano mapya, unapaswa angalau uspend asilia 50% ukiwa na boyfriend wako mpya halafu hizo nyingine zitumie kwa marafiki na familia yako.
#6 Weka mipaka.
Kila mtu anakuwa na mipaka yake na kila mtu huheshimu mipaka ya wengine. Iwapo unajihisi kuwa hujisikii huru wakati boyfriend wako amevamia mipaka yako basi unapaswa umwambie ajue. Kwa mfano kama hujazoea boyfriend wako mpya aguse ama ashike vitu vyako basi unamwambia na mapema ili ajue kuwa unahitaji aheshimu baadhi ya mambo yako. [Soma: Dalili za kuonyesha kuwa hatakuwa boyfriend wako]
#7 Jua lengo la mahusiano yenu.
Unapaswa kujua lengo la mahusiano yenu. Kama ni mahusiano ya mlalano ama ya kudumu lazima ujue. Hii itakusaidia usiweze kupoteza muda wako katika mahusiano ambayo hayatakupeleka mahali popote. Lazima uwe mkweli katika kujua lengo lako kwa kuwa mambo yakiharibika ni wewe ambaye utakuja kuumia.
#8 Jienjoy
Huu ni wakati wako wa kuinjoy muda wako. Mvumbue boyfriend wako mpya. Tembeeni sehemu mpya, jaribuni hoteli mpya, tembeleeni miji mipya na kadhalika. Huyu ni mtu ambaye unapaswa kuvumbua mapya na yeye. Na kama hauwezi kufanya mambo mapya ukiwa na yeye basi kuna umuhimu gani wa kuwa na yeye kimahusiano?
#9 Usijeuze tabia.
Wanawake wengi hukosea na hapa. Wanabadilisha tabia zao ili ziwaridhishe wapenzi wao. Haya ni makosa makubwa ambayo unapaswa kuyaepuka. Hufai kubadilisha tabia ili uridhishe mwanaume yeyote. Unahitaji kuwa na maoni yako binafsi. Hii ni muhimu kwa kuwa itafikia mahali utataka kurudi kwa tabia zako za awali ilhali amekuzoea na tabia nyingine. Upo?
#10 Usiharakishe kukutana na wazazi.
Kukutana na wazazi huwa ni jambo zito ambalo linahitaji moyo. Lakini usilazimishe ukutane na wazazi katika deti ya pili. Chukua muda wako kwanza. Haina haraka. Muhimu ni kwanza uweze kumjua huyu boyfriend wako mpya kabla fikra za kukutana wazazi hazijakujia.
#11 Usimfanye kila wakati alipe.
Huyu ni boyfriend wako na wala si shimo la pesa ama ATM. Ukweli ni kuwa wanaume huwa wanakuwa na presha nyingi wakati wanapojiingiza katika mahusiano na mwanamke. Hii ni kwa sababu wanawake wengi hupenda kuwaomba pesa kupindukia. So hapa usimpe presha mpenzi wako. Ukiwa na pesa toa. Lipa bili za hoteli ama lipia yale mambo madogo madogo.
#12 Kuwa mkweli.
Ukitaka mahusiano yenu yaende sawa, basi lazima uwe mkweli kwa mambo yako. Usitumie uongo kutaka kufanikisha jambo. Umejuana naye tu juzi. Hivyo tabia zako za mara ya kwanza ndizo ambazo atazichukua kama hulka yako. Lakini usisahau kuwa hupaswi kumwambia kila kitu hadi siri zako za kuzimu. Hizo baki nazo.
Umeona sasa? Haya si mambo magumu ya kuzingatia unapopata boyfriend mpya. Zingatia mambo ya kufanya na kutofanya ili uweze kufaulu katika mahusiano yako.
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: