KUNA MWANAUME AMBAYE HACHEPUKI BONGO..MAJIBU HAYA MAZURI SANA SOMA MPAKA MWISHO




Dada mmoja aliniuliza, hivi kuna mwanaume kweli ambaye hachepuki! Nilimuuliza kwanini unasema hivyo akaniambia kuwa mume wake amekua msiri sana, simu yake kaweka Passwed anashindwa kujua kuwa anachat na kina nani? nilitulia kidogo kisha nikamuuliza “Mbona hulii wakati kuna msiba?” Alishangaa na kuniuliza msiba wa nani?

Nilitoa simu yangu na kuingia Facebook, kisha nikaandika R.I.P nika search kisha zikaja picha za watu wengi ambao walifariki sioku ile na zamani. Nilimuonyesha moja wapo tena ya katoto kazuri, nikamuambia unaona haka katoto kamefariki mbona hulii. Aliniambia nitaliaje wakati sikafahamu, nikamuambia lakini kamefariki, akaniambia sawa ila sikajui ningekua najua basi ndiyo ningeumia.

Nikamuambia ni kweli, watu tunaumizwa na vitui mabavyo tunavijua na si vile amabvyo hatuvijui, tumaumizwa na misiba ya watu wa karibu kwakua tunawajua na tunajua imetokea, lakini kila siku kuna watu mamilioni wanakufa ila hatulii. Nikamuambia hata wewe mume wako, inawezekana anachepuka lakini kama wewe hujui basi huwezi kuumia kwakua ni msiba usio kuhusu, atachepuka huko weee lakini akirudi hujui unaona kawaid aunafurahia maisha.

Nikamuambia, kama unataka kulia kila siku basi fuatilia simu yake. Utajua anachepuka na kila akitoka utakua wewe ni mtu wa kulia kwakua tu unajua anachepuka, nikamuambia hiyo ni misiba ya watu itakua inakuliza kila siku. Subiri ulie na msiba wako, lia akikuletea mwanamke mwingine ndani, lia ukiona picha, lakini kama anaficha ukichunguza ni kama kwenda kutafuta misiba ambayo haikuhusu!

Aliniambia lakini kuna magonjwa, nilimuuliza hivi kama ukimfumania uanweza kumaucha, akajibu hapana, unaweza kumlazimisha kutumia condom akasema hapana, nikamuambia kwahiyo unataka nini sasa! Akasema nataka nijue tu, nikamuambia ukishajua! Alibaki kimya, nikamuambia dada yangu kama huwezi kumaucha, huwezi kulazimisha condom basia cha kuchunguza, acha kutafuta misiba na visirani ambavyo havikuhusu, kama hakuonyeshi anayofanya huko duniani hayakuhusu ni misiba ya watu usiikalie matanga!

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.