JE UNAMPENDA SANA ILA YEYE HAJALI WALA HAKUONESHI UPENDO WALA KUJALI

Umdhaniaye ndiye kumbe siye, Ni kweli kuwa mahusiano yamekuwa mzigo kwako, yamekuwa magumu na machungu kiasi cha kulia na kukosa la kufanya, unampenda na haoni thamani yako, umempa moyo na kila wema lakini malipo yamekuwa kilio na kutaabika,
Imefika mahali unawaza kwani Mahusiano ni pilipili au kitunguu? Unajiuliza hivi ni wewe tu au hata rafiki yako anayetolewa out na mwenzi wake naye humpata haya? Unahisi unaonewa na hauna bahati ya kupendwa.
Inafika mahali unaamua kujifungia ndani na kulia kwa sauti ili moyo upumue, ukihisi umelia imetosha umeridhika, lakini unapochukua simu ili kumtafuta hapokei simu, sms hajibu, yupo online na hajishughulishi kukutafuta, moyo unajaa hasira, unaanza kulia tena, unakata tamaa na kuona heri uwe single.
Mtia Moyo leo ninalo jambo la kukufumbua macho, kamwe usilazimishe upendo, usipopendwa huwezi papenda, tia mkakati wa kuamua maamuzi magumu ili uwe huru.
Neno la Mungu linasema
"Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Yeremia 33 
Mkabidhi Mungu mahusiano yako, naye atafanya njia pasipo njia, atatenda nawe utaipata amani na machozi mazito ya furaha yatabubujika machoni mwako.
Mungu ndiye Njia, Njia ya amani kwa wale wote wanaomtegemea kwa kila jambo hata katika Mahusiano yao pia.
Mungu akutie Nguvu. ðŸ˜˜
Share na rafiki zako wapone
UTAMU KITANDANI APP


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.