STORY:PENZI LA MJEDA EP 21 (FINAL EPISODE)







Omary akamwambia yule alionekana kama ndo msimamizi pale.. "wakiwa tayari utanipigia simu" akasema "Sawa boss" Omary akasema "Nitakuja kuwachukua" Alivo ondoka tu Omary nikamwambia Martha "Martha hebu twambie kinacho endelea hapa" akasema "Kwaiyo mko serious hamjui chochote?" Nikasema "Hatujui" Martha akasema "Kmaa wiki moja nyuma Omary alikuja kule nyumbani akaomba nimuelekeze kwenu kwa baba yako,akasema anataka kutoa mahali ila hataki kukusumbua maana wewe ni mja mzito na uki panda magari unatapika kwaiyo yeye atamaliza yote peke yake mimi nilimuelekeza mpaka kwa baba yako lakini alimkuta kalewa sana akasema atarudi kesho yake hivyo kazi yangu ilikua ni kuhakikisha mzee halewi mpaka Omary aje waongee akiwa hajanywa siku iloyo fata Omary alikuja na mimi nilikuepo ila kwenye swala la mahali niliona hayanihusu mie nikatoka nje walikukubaliana na Baadae Omary alileta mahari ila alipewa sharti na mzee kwamba wewe usibadilishe dini na ndoa ifungwe kikristu Omary alikubali ila na yeye aliomba ndoa ifungwe mala mbili kikristu na kiislamu mzee hakuwa na shida ila kilicho tushangaza ni aliharakisha sna ndoa kusema kwamba anataka ifungwe wiki ijayo kwasababu wewe una mimba ndo mana anataka mambo yaende haraka"  nikasema "hee mbona hujawahi kuniambia?" Akasema "Omary alisema anataka afanye surprise ambayo haijawahi tokea na ukiangalia ni kweli.. nani aliwahi kuolewa bila kujua? Na pia alisema tualike watu wote tunaotaka kwaiyo usinilaumu nimealika mpka tuliosoma nao primary kwanza alisema hataki mchango wala pesa ya aina yoyote"

Nilibaki nimeduwaa sijui hata nisemeje nikachukua simu nimpigie Omary mama akasema "Wacha fanya kama alivyo panga nimefurahi sana"
Yule dada alie kua ananipamba akasema "Dada una haribu make up" watu wote wakanigeukia na mimi ndo nashtuka najiangalia kwenye kioo kumbe machozi yananitoka Martha akasema "Usilie bwana make up itakaa vibaya" mama nae akasema "Unataka picha zitoke vibaya macho yakiwa yamevimba?" Nikasema "Samahani" yule dada akanipamba tena vizuri kumaliza pale tukavalishwa nguo nzuri mimi ndo lilikua lile shera na viatu pamoja na crown aliyo niletea Omary. Mama na Martha pia walipendeza sana.

Omary akapigiwa simu baada ya mda tukaambiwa kuna gari inatusubiri nje tukaingia lakini hakua Omary tukaenda mpaka kanisani tukakuta gari la Omary lipo nje na kuna watu wengi hatari mpaka naona aibu kulikua na ndugu zangu kulikua na marafiki kulikua na wajeda kibao yaani nilikua naona hata aibu kushuka kwenye gari nikiwa bado naona aibu Martha alishuka akanifungulia mlango nataka kushuka Omary kafika kanishika mkono kanishusha matarumbeta yaka anza kupigwa tunapanda ngazi kuelekea kanisani Omary kanishika mkono anasema "Umependeza sna mke wangu" mimi siamini kinacho tokea machozi yananilenga akasema kwa sauti ya chini "Kama unataka kulia mama lia ukitaka kucheka cheka leo ni siku yako" machozi yalinishinda kuzuia.. Nilijikuta nalia tu mpaka nafika pale altaleni naona baba yangu shangazi zangu mama wadogo wamekaa siti ya mbele na wamependeza balaa..

Tulifungishwa ndoa..Tukabadilishana pete.. Baada ya kubadilishana pete nilijikuta namkumbatia kwa nguvu mme wangu halali sasa Omary yani nilimkumbatia huku nalia Omary nae alikua ananituliza huku ananipiga piga mgongoni.. Akaninyanyua akanikiss bila kujali ni kanisani kuna watu kuna nini..

Baada ya pale tulienda kupumzika na usiku tulienda ukumbini sherehe ilifana wallah yaani iliwaka ilipendeza baada ya pale Omary alinambia "Samahani mke wangu tutaenda honeymoon soon saiv si unajua kuna tatizo tunatakiwa tutatue" nikasema "sawa haina shida mme wangu" waaaaiiii ni mwendo wa mahaba tu tulirudi nyumbani tukiwa tumechoka kila mtu alikua amelala mama alienda kuoga na kulala maana bado alikua analala sebleni mimi na Omary pia tulienda kuoga tukapasha kwanza hivi nani anaujua ule wimbo wa Gnako na Maua sama unaimbwa gusaaa..Gusanisha..Nyama kwa nyama gusanisha..hasi na chanya gusanisha..

Baaasi sisi tuligusanishaaaaa mpaka tukachokaaa tukalala.. Simu ya asubuhi kutoka kwa mchumba wa Omary ilitushtua yule dada alikua amechafukwa sana alitukana mno akasema kwanini amefunga ndoa wakati yeye ni mchumba wa mtu sijui nini mambo kibao. Omary akasema aiseeh taarifa zinasambaa fasta mno..

Tumeamka baba alikua bado amelala.. Wakati tunakunywa chai baba alitoka huko chumbani kwa hasira alimkamata Omary alimpiga vibaya mno.. alimpiga mpaka basi akasema "Huwezi kuniaibisha kiasi hicho kisa mwanamke huyo namuua leo" baba mkwe katoka kuelekea chumbani wifi akaja anakimbia anasema "Tina toka ondoka" yani tupo kwenye taharuki nini tena hapa Wifi kanivuta kunitoa nje baba mkwe nae anakuja mbio mama na Omary wapo kwenye taharuki mm nashangaa nini kinatokea ile wifi ananisukuma naskia chuma inalia Booooom!!! Risasi mzee wifi kanisukuma bila kuangalia ananisukumia wapi nilidondoke kopo la maua lilikua pale kumbe kwa bahati mbaya bastola iliyo takiwa kunipiga mimi ikampiga wifi eneo la bega baba mkwe baada ya kushtuka tukio alilo fanya nguvu zilimuisha bastola ikamdondoka Omary akaiwahi akapiga simu jeshini wakaja pale wakamchukua baba mkwe mimi pamoja na wifi mama mkwe nae alipoteza fahamu kwaiyo wote tulichukuliwa kupelekwa jeshini kwa huduma baba mkwe alikua chini ya ulinzi..

Mimi nilikuja kushutuka nimeweka dripu ya damu. Nashangaa nini mbona naogezewa damu nataka kunyanyuka naskia huku kwa bibi kama kunauma alafu mbona kama najihisi tumbo jepesi? Natahamaki usikute mimba yangu imetoka.. ndo  dactari ananiambia "pole mimba imeharibika" nilishtuka sana.. "Whaaat? Mimba imeharibika? Mtoto wangu amekufa?" Nilipo vuta kumbu kumbu ndo nikakumbuka ilivo kua nauliza "Wifi? Wifi je? Wifi amepona? Wifi amekufa? Hapana wifi yuko wapi?" Yaani maswali yote namaliza mimi..

Dakika chache naona Omary anaingia nguo yake ina damu yani yupo vile vile alivo amka kavaa pensi na t-shirt lakini zinadamu kaingia anaonekana amechoka sana madactari wakampisha akaja mpaka pale nilipo akanikumbatia wote tukawa tunalia anasema tu "Mwanangu Tina,Tina mtoto wetu amekufa" pale sasa ikabidi mimi ndo niwe jasiri nikamwambia "Tutapata mwingine mme wangu usilie" nikamuuliza "Vipi kuhusu wifi?" Akasema "Ndo natoka saiv kwenye chumba walicho kua wanamfanyia upasuaji kutoa risasi ila bado hajapata fahamu ila hali yake haiko kwenye hatari sana"  nikamuuliza "na mama je?" Akasema "Mama alipoteza fahamu kwa sababu ya mshtuko na sasa amepumzishwa tu hana tatizo" nikamkumbatia maana kweli alikua na wakati mgumu.

Sote tulipona tukaruhusiwa kwenda nyumbani ila baba mkwe alikua chini ya ulinzi na alianza kufatiliwa kwanzia mambo ya mwanzo ambayo mama alikua anasema na sasa amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kufanya mauaji kwa kukusudia..Kufanya biashara haramu na kutumia cheo chake kufanya uharifu.

Wifi aliomba msamaha kwa yote aliyo mkosea mama na mama alimsamehe mimi sikua hata na haja ya msamaha maana tayari alisha okoa maisha yangu. Tulianza upya na tulipendana kweli kweli mama na wifi walitaka tuendele kuishi nao pale lakini Omary alisistiza anataka aishi na mke wake peke yetu ila wakitumiss tutaenda kukaa hata mwezi tulirudi tukawa tunaishi pamoja kwa Omary na mapenz ni motroooo..

Tupo kwenye harakati za kutafta mtoto mwingine kwaiyo mpwipwi fulldose.. hakuna masaaa yaani mda wowote tunapiga mpwipwi..
_________THE END________

FUNZO:
1;Mapenzi haya lazimishwi wala hayataftwi. Mapenzi yanakuja yenyewe ukiyalazimisha yatakutokea puani.

2;Kila ubaya unao ufanya hata ufanye gizani jua una kua recorded hata kama si leo jua ipo siku utaumbuka.

3;Mama anapo kujali na kukuthamini kmaa mwanae hebu na wewe mpe thamani anayo stahili haijalishi ana mapungufu gani mama ni mama tu aiseeh there's no place you'll find a better mom as yours.. kila mtu ana mama yake ila trust me wako ni bora zaidi ya wote.

4;Baba ana nafasi yake na mama ana nafasi yake na wote ni wa muhimu kila mtu kwa nafasi yake unapo onyesha kumpenda mmoja zaidi ya mwingine fikiria wewe watoto wako wakubague.

5;Midomo mda mwingine inatuponza kuna mda tunatakiwa tujue jinsi ya kunyamaza sio kila kinacho kuja mdomoni mwako lazima uropoke. (Mwanzo wa mgogoro kati ya Tina na wifi ake ni mdomo tina alivo kua anaropoka bila kufkiria)

6;Mpe nafasi mwenza wako ajielezee..Pale unapohisi kitu hakipo sawa Don't assume uliza.. Usianze kuwaza labda hiki labda hiki uliza na mpe nafasi ya kujibu mpe nafasi ya kuelezea. (Tina hakumpa nafasi Omary ya kuelezea kuwa yule mwanamke ni nani na ku assume kwamba ni sugar mammy wake which was wrong)

Nawapenda sana..





(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.