Njia 60 za kufanya Mpenzi wako awe na furaha zaidi


1. Mfanye ahisi kuwa yuko salama; acha kuwa mbabe na mgomvi!
2. Unapoingia nyumbani ‘toa salamu' Salamu humfukuza shetani nyumbani kwako!

3. Mke ni mfano wa chombo laini na lazima kukitunza. Kumbuka kuwa kuna mambo mazuri utakayoyapata kwake, hivyo amiliana naye kwa ulaini wa moyo.
4. Unapomshauri jambo, basi kaa naye faragha na katika mazingira yenye utulivu. Usifanye hivyo hadharani, kwa maana hiyo ni sawa na kumkashifu.
5. Kuwa mkarimu kwa mkeo- humfanya azidi kuwa na hisia ya upendo na kuhisi kuendelea kuhisi kuwa anapendwa.
6. Mpishe akae kwenye kiti chako. Hilo litaupoza moyo wake.
7. Epuka ghadhabu na hasira. unapokuwa na hasira kaa chini, kama ulikuwa umekaa basi lala.
8. Jitahidi kuonekana maridadi na unukie vyema kwa ajili ya mkeo. Huimarisha MAHABA!
9. Usiwe mgumu. Hilo litakuangusha. Kuwa mgumu na mkali haitakufanya kuwa mume bora.
10. Msikilize mkeo – KUWA MSIKILIZAJI MZURI.
11. Kubali kusifiwa na kubembelezwa, kataa mabishano na majibizano. Mabishano ni kama sumu katika ndoa.
12.Tuwaite wake zetu kwa majina mazuri kabisa, jina lolote ambalo mke anapenda kulisikia.
Mfano sweet ......
13. Mshangaze kwa mambo yenye kumvutia. Kama anapenda kitu fulani, mshtukize kwa kumletea kitu hicho bila yeye mwenye kutarajia. Itastawisha mahaba moyoni mwake.
14. Udhibiti ulimi wako
15. Sisi sote tuna mapungufu. Yakubali mapungufu yake na Mungu ataweka baraka katika ndoa yenu.
16. Mwambie kuwa unamthamini. Muoneshe kuwa unamthamini na kutambua umuhimu wa uwepo wake katika maisha yako.
17. Mhamasishe kuendeleza uhusiano mzuri na ndugu na wazazi wake.
18. Zungumza naye mada anayoipenda.
19. Mkiwa mbele ya ndugu zake msifu. Waambie kuwa ni mtu mzuri sana, na kwamba ni mtu mwema na unamshukuru Mungu kwa kumfanya kuwa mwenza wako.
20. Peaneni zawadi, mtazidi kupendana. Zawadi huongeza mahaba.
21. Achana na mambo yale yale ya kila siku angalau kwa muda fulani, mshangaze na kitu tofauti
kabisa, hilo litaondosha kutu katika mahaba yenu na kuling’arisha penzi lenu.
22. kuwadhania vizuri wenzetu. Msimdhanie vibaya mkeo.
23. Yapuuze baadhi ya makosa yake…. Jifanye kuwa hujayaona. Usiyaingize akilini mwako.
24. Ongeza matone ya subira yako, hususan anapokuwa mjamzito au akiwa katika siku zake.
25. Tarajia na heshimu wivu wake.
26. Kuwa mnyenyekevu. Iwapo kazi yako ni nzuri, heshimu kwamba anawatunza watoto, anakuhudumia, anaihudumia nyumba yako unapokuwa haupo, nguvu yake ndio nguvu yako, na mafanikio yake ndio mafanikio yako.
27. Usiwafanye marafiki kuwa bora zaidi ya mkeo.
28. Msaidie mkeo kazi za nyumbani.
29. Msaidie kuwaheshimu wazazi wako, huwezi kumlazimisha kuwapenda, lakini unaweza kumsaidia kuwapenda hatua kwa hatua.
30. Muonesha kuwa yeye ni mke bora, ni mke wa mfano.
31. Mkumbuke mkeo katika dua zako. Itaongeza mahaba na ulinziw a ndoa yenu.
32. Yaache yaliyopita. Hayana msaada tena kwako zaidi ya kukuongezea maumivu na uchungu.
33. Usijaribu kuonesha kwamba unamfanyia hisani pindi unapofanya kitu, kama vile kununua chakula cha nyumbani, kwa sababu wewe sio mtoa riziki bali ni mfikishaji wa hiyo riziki
34. Shetani ndiye adui yako, sio mkeo. Wakati fulani mke na mume wanapozungumza shetani huingilia kati na kuchochea ugomvi, hivyo shetani ndiye adui wa kweli. Haitoshi tu kumchukia shetani, bali unatakiwa kumuona kama adui . Shetani anapenda talaka. Kila siku anakutana na jeshi lake la maibilisi na kuwauliza kazi walizofanya, baadhi husema kuwa wamemshawishi mtu fulani kuiba na kadhalika. Yule anayesema kuwa amemfanya mtu fulani amtaliki mkewe husifiwa kuwa amefanya kazi bora kabisa.
35. Mlishe chakula kwa mikono yako
hili Ni jambo lenye baraka. Chakula hicho hakiishii tumboni tu, bali huenda moja kwa moja moyoni mwake. Huongeza mahaba na kuhurumiana baina yenu.
36. Mlinde mkeo dhidi ya shari za shetani na wanadamu. Yeye ni kama lulu ghali ambayo inatakiwa kulindwa dhidi ya hasadi za iblisi na shetani.
37. Muoneshe tabasamu lako. Tabasamu mbele yake. Kumbuka: TABASAMU NI SADAKA.
38. Matatizo na changamoto ndogo ndogo zinaweza kuwa tatizo kubwa. Kama una mambo madogo ambayo hayapendi nawe ukaendelea kuyarudiarudia, yatatengeneza ukuta mkubwa kati yenu. Usiyapuuze, yanaweza kuja kuwa makubwa.
39. Epuka kuwa mkali.
40. Heshimu fikra zake, muoneshe kwamba unapenda fikra na mawazo yake.
41. Msaidie kufikia mafanikio yake, kwa maana mafanikio yake ndio mafanikio yako.
42. Heshimu uhusiano wa ndoa na mipaka yake. Wakati fulani anaweza kuwa hajisikii vizuri; basi heshimu na uthamini hisia zake.
43. Msaidie katika utunzaji wa watoto. Baadhi ya wanaume hudhani kuwa jambo hilo linapunguza uanaume wao, lakini ukweli ni kwamba linakufanya uzidi kuheshimika.
44. Tumia tunu za ulimi na mazungumzo matamu. Mwambie anaonekana mrembo, maridhawa na maridadi. Tumia sanaa ya ulimi kuliboresha penzi lako.
45. Keti ushirikiane chakula na mkeo.
46. Mjulishe kuwa unasafiri. Usimshtukize, Mwambie tarehe na muda utakaorudi kutoka safarini.
47. Usiondoke nyumbani pindi matatizo yanapoibuka.
48. Nyumba ina siri na faragha zake. Ukizipeleka siri hizi kwa marafiki na jamaa zako utakuwa unaweka shimo hatari sana katika ndoa yako. Siri ya nyumba hubaki nyumbani. Ni vibaya kuyaanika mambo yenu kwa kila mtu kana kwamba ni bidhaa inayotakiwa kununuliwa.
49. Hamasishaneni kufanya ibada; Mnaposaidiana kufanya mambo mema pamoja huzidisha na kuimarisha mahaba baina yenu.
50. Zitambue na uzijue haki zake, sio tu kuziandika bali kuziingiza ndani ya moyo na akili yako.
51. ‘Ishini na mke wako kwa wema’. Amiliana naye kwa wema. Katika nyakati za raha na nyakati za shida ishi naye na uamiliane naye kwa wema na mahaba.
52. Wakati wa mahusiano ya kimapenzi tunapaswa kuonesha heshima na kuwajali wake zetu.
53. Unapokuwa na khitilafu na mkeo usimwambie kila mtu. Ni kama kuliacha wazi jeraha lako, hivyo kuwa mwangalifu kwa wale unaowaelezea matatizo na khitilafu zenu.
54. Muoneshe mkeo kuwa unajali sana afya yake. Afya njema ya mkeo ni faida kwako na uzima wake ndio uzima wako. Kujali afya yake humuonesha kuwa unampenda kwa dhati.
55. Usidhani kuwa siku zote utakuwa sahihi. Hata uwe mwema kiasi gani lazima utakuwa na mapungufu. Wewe sio mkamilifu
Ondokana na maradhi ya dhana hiyo.
56. Mhusishe katika matatizo, furaha na huzuni zako.
57. Mhurumie kwa udhaifu wake. Mhurumie wakati wote. 58. Kumbuka kuwa wewe ndo nguvu yake, wewe ndiye mtu anayemuegemea wakati wa tabu na dhiki.
59. Mkubali kama alivyo.
wanawake wameumbwa kutokana na ubavu uliopinda. Ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na hiyo itakuwa sababu ya talaka.
unaweza usiipende tabia yake moja lakini utaipenda tabia nyingine,
60.ANGALIZO ITUMIKE KWA WENYE NDOA TU






(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.